Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Umma wa Muhammad Umeachwa Unazama kwenye Mafuriko ya Matope na Takataka Bila ya Khilafah

(Imetafsiriwa)

Habari:

Gazeti la ‘The Guardian’ liliripoti kuwa baadhi ya maeneo ya Gaza yanakabiliwa na mafuriko makubwa wakati wa msimu huu wa baridi baada ya usiku wa mvua kubwa na upepo mkali.  Maeneo yaliyoathiriwa ni pamoja na kambi za wakimbizi za Jabalia. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya 85% ya raia wa Gaza sasa wamekimbia makaazi yao; wengi wao ni wanawake na watoto. Maji ya mvua yaliloweka na kuharibu mahema ya vikosi vya watu kuondoka majumbani mwao kutokana na kulipuliwa na umbile la Kiyahudi. Hali ya hewa inazidi kusukuma mgogoro wa kibinadamu katika mzunguko hatari unaozidi kuongezeka.

 Maoni:

Takriban 85% ya wakaazi milioni 2 wa Gaza wamekimbia makaazi yao tangu mapigano yalipoanza mwezi Oktoba. Kuanza kwa msimu wa majira ya baridi kali, ambayo inaweza kulinganishwa na nchi nyingi za Ulaya katika hali ya baridi, mvua na hali mbaya, ina maana kwamba kuenea kwa magonjwa na uhaba wa maji, umeme na chakula kutaongeza vifo vya watu wasio na uwezo.

Kwa vile mahema yote yamo ndani ya maji, kanda za video za kusikitisha kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha kina mama wa Ummah wakionyesha nguo na mali za watoto wao.  Kwa kukosa njia ya kukauka, watoto wanalala kwenye vitanda vyao vyenye unyevunyevu na nguo zao zilizolowa na wanaugua.

Uchumi wa Gaza umesimama huku kila sehemu ya kufikia msaada ikizibwa na maadui wa Uislamu. Udhibiti wa uhai na kifo cha Ummah huu hatimaye umekabidhiwa umbile la Kiyahudi na wafuasi wake na viongozi wa Kiislamu wanaosherehekea sikukuu yao ya "Krismasi" na msimu wa "Mwaka Mpya" na kutumikia thaqafa ya Kimagharibi katika ardhi za Kiislamu.

Je, unyama huu unawezaje kutotambuliwa na majeshi makubwa ya waumini? Wanaume wako wapi? Tunaweza tu kubadilisha janga hili kwa kurudi kwa mtawala wa Kiislamu ambaye hatawaacha wanawake na watoto wazame kwenye maji machafu ya ardhi ambayo ni haki yao ya kuzaliwa.

[وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنْتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُمْ بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنْتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍ مِنَ النَّارِ فَأَنْقَذَكُمْ مِنْهَا كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ]

“Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka.” [3;103]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

 Imrana Muhammad

 Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu