- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Suluhisho Angamivu la Marekani la Dola Mbili Linahalalisha na Kuendeleza tu Jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina
(Imetafsiriwa)
Habari:
Huku mauaji ya halaiki huko Gaza yakiendelea, kumekuwa na ongezeko la wito kutoka kwa serikali ya Marekani na serikali zingine za Kimagharibi na vile vile Muungano wa Ulaya, Umoja wa Mataifa na watawala wa nchi za Waislamu ili kuongeza juhudi za kulifanya suluhisho la dola mbili kwa Palestina lizae matunda. Mnamo Jumamosi, Januari 6, wakati wa ziara ya Beirut, mkuu wa sera za kigeni za Muungano wa Ulaya alisema kwamba anakusudia kuanzisha mpango wa Ulaya-Arab kufufua mchakato wa amani ambao utasababisha suluhisho la dola mbili kwa mzozo wa 'Israel'-Palestina. Alisema: “Ni wakati sasa wa kulifanya wazo letu la suluhisho la dola mbili kuwa ukweli, vyenginevyo mzunguko wa vurugu utaendelea kizazi baada ya kizazi, mazishi baada ya mazishi, kwa sababu huwezi kuua wazo.” Wakati wa ziara ya hivi karibuni ya Wziri wa Masuala ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken, alikutana na Waziri wa Mambo ya nje wa Jordan Ayman Safadi ambaye alijadili hali ya baadaye ambayo ingeleta pamoja Ukingo wa Magharibi na Gaza kama msingi wa suluhisho la dola mbili kwa 'Waisraeli' na Wapalestina.
Maoni:
Lile linaloitwa suluhisho la dola mbili kwa Palestina limetangazwa kwa miongo kadhaa na serikali za Kimagharibi na serikali zao vibaraka katika nchi za Waislamu kama njia pekee ya kupata amani, usalama na haki kwa wote katika ardhi hiyo. Kwa kweli, hutumika tu kama njia ya kuendelea na kuimarisha uwepo na utawala wa vamizi wa Kizayuni. Robert F. Kennedy Junior, mgombea wa urais wa Marekani 2024, alisema katika mahojiano, “Israel ni ngome yetu ... inakaribia kuwa kama manuari yenye kubeba ndege katika Mashariki ya Kati. Ni mshirika wetu mkongwe. Ikiwa Israel itatoweka, Urusi, China na nchi za BRICS+ zitadhibiti 90% ya mafuta ulimwenguni na hilo linaweza kuwa baya kwa usalama wa kitaifa wa Marekani.” Ni wazi kwamba umbile la Kizayuni ni mbwa mtiifu wa ukoloni wa Marekani katika nchi za Waislamu. Kwa hivyo, suluhisho lolote lililokuzwa na serikali ya Marekani kwa eneo hilo litatumikia tu maslahi yake na yale ya uwanja wake wa Wazayuni badala ya kuleta kheri yoyote kwa Waislamu wa Palestina.
Kwa kuongezea, ni jinsi gani suluhisho la dola mbili linaloshauri kwamba dola ya Palestina iundwe juu ya mipaka ya 1967, ambayo kimsingi inalipa zawadi ya umbile la Kizayuni karibu 80% ya ardhi ya kihistoria ya Palestina, huku ikiwaacha Wapalestina na khumusi moja tu ya ardhi? Je! Kuna uadilifu gani kwa mpango wowote unaoruhusu mwizi kubakia na kile alichokiiba na hilo linahalalisha na kusafisha unyakuzi wa ardhi, kuvunja nyumba, mauaji ya halaiki, mauaji ya kimbari ya watu kutoka nchi yao na mlima wa uhalifu mwingine wa uvamizi huu wa kikatili ambao umeleta uwepo na kueneza utawala wake juu ya Ardhi Iliyobarikiwa? Je! HiLi halilipi uhasama, mauaji ya halaiki na ugaidi yaliyotungwa na umbile la Kizayuni na ukandamizaji wake wa kuendelea kwa watu wa Palestina? Kama mwandishi wa habari mmoja alivyoelezea-dola huria za Kimagharibi hutupa karibu na ibara ya suluhisho la 'dola mbili' kwa “karatasi juu ya uhalisia mbaya”.
Kwa kuongezea, dola hii inayoitwa Palestina itakuwaje? Je, itanyimwa nguvu za kijeshi, huku harakati zote za upinzani zikipokonywa silaha, na kuifanya iwe bila ya hifadhi na isiweze kujilinda kutokana na uchokozi wowote wa baadaye wa Kizayuni unaolenga kunyakua ardhi zaidi na zaidi. Katika mahojiano mnamo Februari mwaka jana, kiongozi wa umbile la Kizayuni, Benjamin Netanyahu, alisema kwamba dola ya mustakbali ya Palestina italazimika kukabidhi udhibiti wa usalama kwa 'Israel', akikubali kwamba huu sio "ubwana kamili." Kwa kweli, hii itakuwa dola ISIYO na uhuru - hakuna udhibiti wa mipaka yake, uwanja wa ndege, jeshi au uchumi; dola isiyo na rasilimali halisi ambayo inategemea umbile la Kizayuni kwa uhai wake. Je! Dola hii itakuwa ya aina gani?!! Kwa kuongezea, kuna walowezi zaidi ya 600,000 Kiyahudi na makaazi kadhaa ya Mayahudi katika Ukingo wa Magharibi, baadhi yao ni sawa na miji na majiji yakiwa na shule zao, hospitali na vyuo vikuu, na kufanya lengo la kuanzisha dola ya Palestina kwenye ardhi hiyo kivitendo kutowezekana. Hii ndio sababu Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa UN, Craig Mokhiber alielezea suluhisho la dola mbili kwa Palestina kama “Utani wazi katika vichochoro vya UN ... zote mbili kwa kutowezekana kwake na kwa kufeli kwake kikamilifu kuwajibisha utekelezwaji wa haki za binadamu zisizonyimika za Wapalestina.”
Na mwishowe, uanzishwaji wa dola ya Palestina juu ya ardhi ya Palestina haukubaliani kabisa na falsafa ya Kizayuni ambayo inaamini kuchukua udhibiti wa ardhi nzima ya Palestina ili kuunda kinachoitwa 'Nchi ya Kiyahudi'. Harry Truman, rais wa Marekani miaka ya arubaini na hamsini alisema kwenye video wakati huo, “Wazayuni wako dhidi ya kitu chochote kitakachofanywa endapo hawataweza kuwa na Palestina yote ... hakiwezi kufanywa. Inabidi tukifanye kwa vipimo vidogo vidogo… ” Waziri wa Mawasiliano wa Uvamizi huo, Shlomo Kahri alisema mnamo Disemba, “Hakutakuwa na dola ya Palestina hapa. Kamwe hatutaruhusu dola nyingine kuanzishwa kati ya Jordan na Bahari ya [Mediterrania]”, ikiakisi maneno ya Mkataba wa Likud. Na katika hotuba yake kwa Mkutano Mkuu wa UN Septemba iliyopita, Netanyahu aliweka ramani ya Mashariki ya Kati ambayo ilionyesha 'Israel' inayojumuisha Palestina yote, kutoka mtoni hadi baharini. Ni wazi kwamba umbile la Kizayuni halitakubali chochote chini ya udhibiti kamili juu ya ardhi nzima ya Palestina.
Lile linaloitwa suluhisho la dola mbili halitakuwa chochote ila udhalilifu kwa Waislamu wa Palestina. Watatilishwa saini kwa mustakbali wa maisha chini ya utawala wa umbile halifu la Kizayuni na chini ya utashi wake, pamoja na utakaso wa kikabila kutokana na Palestina yote. Kwa kuongezea, ni usaliti dhidi ya Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake (saw) na waumini, kwa kuwa ardhi nzima ya Palestina imetukuzwa na Mwenyezi Mungu (swt) na ikawa chini ya utawala wa Uislamu wakati wa Khilafah Rashida na kubaki hivyo kwa karne nyingi. Kwa hivyo, kulingana na Sharia, Ardhi yote Iliyobarikiwa ya Palestina iko chini ya umiliki wa Waislamu hadi siku ya Kiyama. Hakuna shubiri yake hata moja inayoweza kupeanwa! Badala yake, mamlaka ya Uislamu inahitaji kusimamishwa juu yake kupitia ukombozi wa ardhi nzima na majeshi ya Waislamu na utabikishaji wa utawala wa Kiislamu chini ya kivuli cha dola ya Khilafah kwa njia ya Utume. Kukubali kitu chochote kando na hili itamruhusu tu mchinjaji na uhalifu mwingine wa uvamizi huu wa kikatili kuendelea! Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَخُونُواْ اللّهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُواْ أَمَانَاتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ]
“Enyi mlio amini! Msimfanyie khiana Mwenyezi Mungu na Mtume, wala msikhini amana zenu, nanyi mnajua.” [Al-Anfal: 27].
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir