- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Mauaji ya Wasichana ni Matunda ya Mfumo wa Kibepari Unaofadhilisha Matamanio na Kujiingiza katika Anasa za Muda Mfupi
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mauaji ya wanawake wawili Wakenya mwezi uliopita yanaangazia hali inayotia wasiwasi katika unyanyasaji wa kijinsia katika nchi hii ya Afrika Mashariki, huku wanaharakati wakitaka hatua zaidi za serikali kuwalinda wanawake. Rita Wean, mwanafunzi wa umri wa miaka 20 aliuawa na kukatwa vipande vipande katika nyumba ya upangaji mfupi katika mji mkuu Nairobi mnamo Januari 14. Siku chache kabla, mtu maarufu katika mtandao wa Instagram, Starlet Wahu, 26, alipatikana amekufa katika chumba cha Airbnb, akivuja damu kutokana na jeraha baya la kuchomwa kisu lililosababishwa na mwanamume mmoja aliyekutana naye mtandaoni.
Maoni:
Mnamo 2022, kulikuwa na jumla ya vifo 46 vya mauaji ya wanawake vilivyorekodiwa nchini Kenya, kulingana na mtoa data za afya, Africa Data Hub. Mnamo 2023, idadi ya mauaji ya wanawake nchini iliongezeka hadi angalau 75. "Yaani, kila siku ya pili, mwanamke amekuwa akitendewa unyama na kuuawa kwa sababu ya kitambulisho chake," shirika la Amnesty International Kenya lilisema.
Kila mfumo wa kibepari wa kikoloni na nidhamu yake ya utawala ya kidemokrasia unapoendelea kustawi, matokeo yake ya kuchukiza huendelea kujitokeza katika nyanja zote za maisha. Mfumo huu wa ukoloni mamboleo, ndiyo mhimili wa kukithiri kwa ufukara, mfumko wa bei, maisha ya juu, ufisadi pamoja na ubadhirifu.
Matatizo haya yote, kwa hakika yamechangia katika kuwa na jamii inayougua vibaya maradhi ya kiakili kama vile mfadhaiko. Zaidi ya yote, kuna ongezeko kubwa la unyanyasaji na mauaji ya kikatili kati ya wanandoa ambayo yamesababisha hali ya kutisha. Ni hivi majuzi tu ambapo tumekuwa tukishuhudia vitendo viovu vya mauaji ya kutisha ya wasichana wadogo katika nyumba za upangaji mfupi (airbnbs).
Wasichana wanaaminika kutoweka katika mazingira ya kutatanisha kutoka vyuo vikuu.
Mauaji haya ya kikatili na ya kinyama, yamepelekea kugunduliwa kwa miili ya wanawake iliyokatwakatwa na kuchinjwa kikatili na wahalifu wanaosadikiwa kuwarubuni kwa pesa, anasa kisha kuwabaka na hatimaye kuwauwa. Baada ya kuwaua, kisha hukimbia kutoka eneo la tukio kwa nia ya kukwepa hofu na kufikishwa mahakamani.
Wasichana hao, waliotarajiwa kuwa katika vyuo vikuu wakisoma, wamegeuzwa kuwa mawindo rahisi kwa kushawishiwa na maisha ya anasa na vivutio.
Kwa hivyo wahalifu wanaowaua, hutumia kile wasichana wanachokosa: pesa na anasa ili kuwadanganya. Hiki ni kielelezo tosha kwamba mfumo wa kibepari na nidhamu yake ya utawala ya kidemokrasia ambao, mbali na kushindwa kuondoa umaskini, unatumika kama mshipi wa kubembeleza wasichana na wanawake kwa ujumla na kuwageuza kuwa vinyago vya ngono kwa ajili ya kujiridhisha tu. Uchu wa pesa, unatumiwa kama ahadi ya uwongo ya njia rahisi ya utajiri kwa wasichana wachanga kujikomboa kutoka kwa ufukara ambao unachangia kushindwa kwao kulipa ada ya masomo kama vile kutunza wapendwa wao nyumbani. Ufukara umekuwa mtego wa uovu na uhalifu. Uislamu pekee, kama mfumo kamili wa maisha, ndio wenye suluhisho la kimaumbile la kudumu juu ya matukio haya ya kutisha.
Kwanza, Uislamu umeweka mfumo mzuri wa maisha, kwa vile mfumo wa elimu ambao unazaa watu wenye shakhsia ya kipekee ambayo inashikamana na uwepo wa Mwenyezi Mungu (swt), hivyo basi kumzuia mtu yeyote kujiingiza katika ufisadi. Kwa maana hii, tendo la kujamiiana, halichukuliwi tu kama njia ya kujiridhisha kimwili, kama ilivyo kawaida ya mfumo wa kidemokrasia wa kibepari; hata hivyo, lengo lake kuu ni kuzaa hivyo kuthibitisha kuendelea kwa vizazi vya mwanadamu, kiasi cha kuleta uhusiano wa kibiolojia kati ya familia mbili tofauti.
Pili, majukumu kati ya mwanamume na mwanamke yameainishwa kwa utukufu; kila mmoja akipata anachostahili kulingana na msimamo wake katika jamii. Yote hayo yanadhamini mambo makuu matatu:
1) UCHAMUNGU. Utetezi wa kwanza unaolinda dhidi ya kujiingiza katika urafiki wowote usiofaa au uhalifu na uovu.
2) Jukumu la jumuiya la kukumbushana yaliyo mema na kukatazana yaliyo mabaya.
3) Hatua ya Dola. Serikali ndicho chombo imara kinachozuia maovu kwa kuweka mazingira mazuri na kutekeleza kanuni za adhabu kwa wahalifu wote. Kwa hiyo, chini ya kivuli cha Khilafah ya Kiislamu ambayo itaibuka hivi karibuni, maovu yote yatatupwa kwenye kaburi la sahau hivyo wanawake watalindwa kutokana na aina zote za ukatili.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Hussein Muhammad Hussein – Kenya