Jumatatu, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Sudan ina Idadi Kubwa zaidi ya Watu Waliokimbia Makaazi yao Duniani na matrilioni ya Utajiri wa Waislamu Unatumiwa kwa Miradi ya Anasa ya Kiburi cha Kitaifa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 25 Januari 2024, gazeti la Sudan Tribune liliripoti kuhusu Mpango wa Mahitaji na Muitikio wa Kibinadamu wa 2024 kwa ajili ya kusimamia idadi kubwa zaidi ya watu waliokimbia makaazi yao. Kwa sasa, Wasudan milioni 14.7 wamelazimika kuyahama makaazi yao kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyozuka mwaka wa 2023. Mashirika ya kibinadamu yanasema kuwa hii inahitaji gharama ya dolari za Marekani bilioni 2.7 ili kusimamia ipasavyo.

Afisa wa Umoja wa Mataifa, Nkweta-Salami alisema anataka kutoa kipaumbele kwa msaada wa vikundi vingi, wa kuokoa maisha kwa watu walio hatarini zaidi kama miaka iliyopita. Mpango huu utakuwa juhudi za pamoja za watendaji na washikadau wote wa kibinadamu nchini. Utashughulikia mahitaji maalum ya wanawake, watoto, walemavu, na vikundi vingine vilivyo katika hatari kubwa. Mpango wa Muitiko wa Kibinadamu wa 2024 (HRP) utapanga kufanya yafuatayo, kulingana na serikali ya Sudan;

“Umoja wa Mataifa na mashirika ya washirika yanathamini msaada wa ukarimu kutoka kwa wafadhili na kuwataka kuendelea kuunga mkono hatua za kibinadamu nchini Sudan; inahitajika sasa kuliko wakati mwingine wowote”

Maoni:

Maombi kwa mashirika na mashirika yale yale ambayo yamewezesha vita na kuendelea kuweka janga hilo kufanya kazi nchini Sudan ni hatua ya kipumbavu ya serikali ya Sudan. Mtume (saw) kamwe hakukubali masharti ya kitaifa ya Dola na yeye (saw) alisema kwamba «لَيْسَ مِنَّا مَنْ دَعَا إِلَى عَصَبِيَّةٍ» “Si katika sisi yule atakayelingania utaifa (‘asabiyya)”

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wao yanaweza kuwafanya Waislamu wengi kuwa wakimbizi na katika hali ya mkanganyiko usio na utulivu, hivyo mali ya eneo inatumikia ajenda ya mkoloni. Kamwe hakutakuwa na masuluhisho yaliyofikiwa na chombo cha adui ambacho kinanufaika na udhaifu wa Ummah.

Hakungekuwa na hali ya mkanganyiko kama huo lau matrilioni hayo ya dolari katika utajiri wetu na rasilimali za majeshi hayangetumika katika miradi ya anasa jangwani au majengo ya juu kwa ajili ya kuishi mamilionea. Wanajeshi wanaambia kupigana tu dhidi ya Waislamu wanaosimama dhidi ya watawala vibaraka wa watumwa chini ya wito wa mabwana zao wa kikoloni.

Sisi kama Umma tunao wengi wa mama na watoto wetu wachamungu wanaounda idadi hii ya watu wasio na makaazi, na tuna ardhi ambayo iko tayari kuwa mahali salama kwa ndugu na dada zetu, na bado wamepigwa marufuku kutoka mipakani kwa sababu ya hati za kusafiria na maadili batili.

Tutaona tu mwisho wa vita hivi vinavyotokea mara kwa mara na kuukimbiza Ummah wakati Dola ya kweli na Amiri atakapokuwepo kwa ajili ya kulinda maslahi ya Waislamu kwa kujitegemea bila ya ufisadi wa madhalimu wanaofanya kazi kwa ajili ya Shetani.

[وَإِنْ يُرِيدُوا خِيَانَتَكَ فَقَدْ خَانُوا اللهَ مِنْ قَبْلُ فَأَمْكَنَ مِنْهُمْ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ]

“Ikiwa wanataka kukufanyia khiana, wao walikwisha mfanyia khiana Mwenyezi Mungu kabla yake, na Yeye akakuwezesha kuwashinda. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima.” [Al-Anfal;71].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu