- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kyrgyzstan iko kwenye Njia ya Udikteta
(Imetafsiriwa)
Habari:
Serikali nchini Kyrgyzstan iliamua hatimaye kukomesha uandishi huru wa habari. Kwa hivyo, mnamo Januari 15, Kamati ya Serikali ya maafisa wa Usalama wa Kitaifa ilifanya upekuzi katika afisi ya wavuti wa mtandao wa 24.kg, ikichukua vifaa na kuwaweka kizuizini mkurugenzi mkuu Asel Otorbaeva, pamoja na wahariri wakuu Makhinur Niyazova na Anton Lymar. Mnamo Januari 16, maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani walifanya upekuzi katika afisi ya Temirov Live, walichukua vifaa, na pia waliwakamata wafanyikazi 11 wa sasa na wa zamani na kupekua nyumba zao. Baada ya kuhojiwa, wafungwa 11 kati ya 14 waliwekwa katika kizuizi cha kabla ya kesi kwa miezi miwili. Waandishi wa habari kutoka shirika la 24.kg wanatuhumiwa kwa madai ya "propaganda za vita," na vikosi vya usalama vinajaribu kuwashtaki wafanyikazi wa sasa na wa zamani wa miradi ya mpelelezi Bolot Temirov kwa "kuitisha machafuko ya umma."
Bolot Temirov ni mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka Kyrgyzstan na mwanahabari mashuhuri, mpelelezi wa ufisadi, mwanzilishi wa chaneli ya YouTube ya "Temirov LIVE", ambapo uchunguzi kuhusu njama za ufisadi katika mashirika ya serikali ya Kyrgyzstan ulichapishwa. Mnamo 2022, mamlaka ilivamia afisi ya Temirov Live na kumfukuza Temirov kutoka Urusi, ingawa yeye ni mzaliwa wa Kyrgyzstan. Bolot Temirov anachukulia kuzuiliwa kwa wafanyikazi wake wa zamani na wa sasa kama kulipiza kisasi kwa waandishi wa habari wachunguzi waliochapisha miradi yake. "Kwa kuzingatia kwamba wafanyikazi ambao hawajatufanyia kazi kwa mwaka mmoja na nusu wamezuiliwa, tunaweza kusema kwamba lengo ni uharibifu kamili wa kila kitu kilichounganishwa na Temirov Live na Ait Ait Dese." Miaka miwili iliyopita pia walidhani kwamba matendo yao yalikuwa yanaharibu timu yetu. Lakini walishindwa. Sasa inaonekana zaidi kama kulipiza kisasi kwa ukweli kwamba tunafichua uwongo wao na kuonyesha ukweli ", - Temirov anaamini.
Maoni:
Kuhusu mtandao wa 24.kg, sababu halisi ya kuteswa kwake inaweza kuhusishwa na uvamizi wake wa Urusi nchini Ukraine: mnamo Septemba 2023, mamlaka ya Urusi ilizuia ufikiaji wa mtandao huo kwenye eneo lao kwa sababu ya kuripoti kwake juu ya vita hivi.
Sadyr Japarov anafanya vitendo kulingana na hali ambayo tayari imefanywa na Putin nchini Urusi ili kuimarisha nguvu zake na kuigeuza nchi hiyo hadi udikteta - kuandaa vita, kuangamiza vyombo huru vya habari, kukamata wapinzani wa kisiasa, yale yanayoitwa, mapambano dhidi ya "ugaidi" na baadaye kuimarishwa kwa Huduma Maalum. Na hii haishangazi: vyanzo mbalimbali vimeripoti kwa muda mrefu kwamba Moscow ilituma wanamkakati wa kisiasa wa Urusi huko Japarov "kuregesha utulivu" nchini Kyrgyzstan, kuhakikisha udhibiti thabiti wa Urusi juu yake kupitia rais mtumwa.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansour