- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Huwezi kuwa Mtetezi wa Jamhuri na wakati huo huo Mtetezi wa Sharia, Ewe Erdogan!
(Imetafsiriwa)
Habari:
Katika taarifa yake katika hafla ya kuhitimu kwa maafisa wa kidini na Uongozi wa Chuo cha Masuala ya Kidini, Rais Recep Tayyip Erdogan alisema yafuatayo: "Tunaona kwamba kampeni ya pande mbili inafanywa dhidi ya Uturuki na duru zinazoichukia Uturuki katika siku za hivi karibuni. La kwanza kati ya haya ni ufafanuzi wa 'Uturuki bila Uislamu' uliojaribu kuletwa na mafashisti wa lumpen. Hebu na niseme kwa uwazi kabisa, ufafanuzi na mradi wa Uturuki ambao haubebi roho ya Uislamu ni majaribio ya kuliweka taifa la Kituruki katika jumba la makumbusho, ili kuligeuza kuwa jambo la ngano. Katika mkondo wa pili wa kampeni, kuna uadui dhidi ya Sharia, unaofanywa chini ya vinyago tofauti. Uadui dhidi ya Sharia, ambao unawakilisha hukmu zote za maisha katika Uislamu, hakika ni uadui kwa dini yenyewe." (NTV, 01.02.2024)
Maoni:
Nchini Uturuki, kuna msemo maarufu ambao kila mtu anaujua, "Tumia dawa kulingana na mapigo." Maana yake ni kama ifuatavyo: "Kuishi kwa njia ambayo itampendeza mtu, kuitikia mielekeo yao, kupiga kiburi chao." Nahau hii, ambayo ina maana ya kutenda bila kanuni ili kupata manufaa, iko katika moyo wa uelewa wa kisiasa wa kidemokrasia unaozingatia maslahi, pamoja na kulingana kikamilifu na wasifu wa kisiasa wa Rais Erdogan, ambaye amekuwa akitumikia mapigo ya jamii kwa miaka 23. Kwa sababu unaweza kumuona Rais Erdogan kama mzalendo siku moja, mtetezi wa ummah siku inayofuata, mpingaji Magharibi siku moja, mtetezi wa Magharibi siku inayofuata, siku moja msekula, wenye dini siku inayofuata, mwana jamhuri siku moja, na mtetezi wa Sharia siku inayofuata. Hotuba zinazotolewa ili kushinda uchaguzi zinatabanni hali ya kisiasa katika jamii.
Matamshi ya hivi karibuni ya Erdogan akiikumbatia Sharia kwa kuilinganisha na Uislamu pia yanapaswa kusomwa katika muktadha huu. Inaweza pia kufasiriwa kama "neno la kweli linalotafutwa kwa nia ya uwongo." Kwa sababu taarifa yoyote ambayo haijathibitishwa kwa vitendo haiwezi kuaminiwa ndani ya mfumo wa ikhlasi. Laiti Rais Erdogan angeitetea Sharia sio tu kwa maneno yake bali pia kwa matendo yake, kwani anadai kuwa anawakilisha Uislamu wote. Laiti asingetekeleza Sharia tu bali pia Mfumo wa Kiuchumi wa Kiislamu, Mfumo wa Kijamii wa Kiislamu, Mfumo wa Adhabu wa Kiislamu, Mfumo wa Elimu wa Kiislamu na mengine yote, kuanzia mfumo wa utawala unaozingatia kuhukumu kwa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu kama msingi wa serikali. Laiti angetabanni na kutekeleza sera ya kigeni ya Uislamu, yenye lengo la kueneza Uislamu kuwa nuru na mwongozo kwa ulimwengu kwa njia ya da’wah na Jihad. Kisha maneno yake dhidi ya mradi wa uingizaji dhana ya Uturuki ambao haubebi roho ya Uislamu yangeweza kusadikika. Lau angelikusanya jeshi la Uturuki kuwanusuru ndugu zao Waislamu huko Gaza, basi tungeweza kufikiri kwamba Erdogan mwenyewe alikuwa anaegemea njia sahihi katika kutekeleza Sharia ya Kiislamu. Hata hivyo, kwa kutumia maneno "Lazima tukuuze kizazi ambacho hakitaanguka katika hali ile ile kama ya Palestina." katika hotuba hiyo hiyo, alionyesha kwamba anaitenganisha Palestina na Uturuki, akionyesha kwamba maregeo yake ya Sharia yalikuwa ni maneno matupu tu.
Kwa hivyo swali linabaki: kwa nini Erdogan ghafla alitoa taarifa inayounga mkono Sharia? Jibu la swali hili linapaswa kutafutwa katika nahau iliyotajwa mwanzoni mwa maandishi, "Tumia dawa kulingana na mapigo." Kwa sababu Erdogan huyo huyo, wiki mbili tu zilizopita, baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri, alimaliza mjadala kuhusu utawala wa Uturuki kwa kauli mbiu 'Uwe na Maisha Marefu Jamhuri' ikisema, "Shaka juu ya utawala wa Uturuki ilimalizika kwa kauli mbiu 'Uwe na Maisha marefu Jamhuri' mnamo Oktoba 29, 1923." na kuitetea jamhuri ya kisekula dhidi ya Sharia.
Kwanza, hadhira aliyohutubia Erdogan katika hotuba hiyo ni jumuiya ya Diyanet inayojumuisha maimamu na wahubiri. Maimamu, wawe wanatoa khutba siku ya Ijumaa au kuwakinaisha Waislamu, ni watu ambao Erdogan anaweza kufaidika zaidi nao wakati wa vipindi vya uchaguzi. Ukosoaji wowote watakaoutoa kwake utaathiri vibaya serikali, huku wakimsifu kutakuwa na athari chanya.
Pili, sababu ya kauli ya Erdogan ya Sharia ikiwemo Gaza ni kilele cha hisia za Kiislamu miongoni mwa Waislamu hasa wa Uturuki kutokana na mauaji ya Gaza. Hasira dhidi ya viongozi, akiwemo Rais Erdogan, ambaye haongozi nchi 57 za Kiislamu kama khalifa, inaongezeka kwa kasi. Ikiwa hasira hii haitalainishwa na kudhibitiwa, Kimbunga cha Aqsa kinaweza kugeuka kuwa kimbunga cha ummah. Kwa hiyo, kauli ya Erdogan kuhusu Sharia, ikiwa ni pamoja na Gaza, inalenga kuregesha imani ya rai jumla ya Kiislamu nchini Uturuki katika mkesha wa uchaguzi nchini mwezi Machi.
Zaidi ya hayo, kutarajia kusimamishwa kwa dola ya Kiislamu kutoka kwa wale wanaopuuza hukmu za Sharia wakati wanatawala, mahusiano kati ya watu ni upuuzi kiasi. Kwa sababu dola ya Kiislamu na mfumo wa maisha wa Kiislamu unaokuja nao unaweza tu kujengwa juu ya hukmu za Sharia na kuendelea kwa kudumisha umuhimu wa kushikamana na Sharia. Kwa hiyo, wale wanaodai Sharia ni lazima kwanza wafahamu ukweli huu kikamilifu na watende ipasavyo ili kustahiki msaada wa Mwenyezi Mungu duniani na Akhera.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ * كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ]
“Enyi mlio amini! Kwa nini mnasema msiyo yatenda? anachukiza vikubwa mno kwa Mwenyezi Mungu kuwa mnasema msiyo yatenda.” [Surah As-Saff: 2-3]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammed Emin Yıldırım