Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Suluhisho Pekee na Thabiti kwa Kadhia ya Palestina ni Kusimamishwa kwa Dola ya Khilafah katika Ardhi Nzima ya Palestina!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Wakati wa ziara yake nchini Malta, Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan alisema katika tangazo la pamoja kwa vyombo vya habari na Waziri wa Mambo ya Nje, Masuala ya Ulaya na Biashara wa Malta Ian Borg kwamba suluhisho bora kwa Palestina ni suluhisho la dola mbili ndani ya mipaka ya 1967. (Mashirika ya Habari)

Maoni:

Waziri wa mambo ya nje Hakan Fidan ametamka maneno kama hayo mara nyingi mbeleni. Katika kipindi cha hivi majuzi cha televisheni, alirudia mambo yale yale kama rekodi iliyovunjwa. Katika tangazo la pamoja kwa vyombo vya habari lililofanyika wakati wa ziara yake ya hivi karibuni nchini Malta, Hakan Fidan alisema kwamba wanataka kuleta amani ya kudumu katika eneo hilo kwa msingi wa suluhisho la dola mbili, na hivyo kuweka usalama na amani ya kudumu kwa Israel na Palestina na kuzuia tatizo hili kutokana na kuleta hatari zaidi kwa eneo.

Hakan Fidan alijadiliana na Ismail Haniyeh, mwenyekiti wa afisi ya kisiasa ya Hamas ambaye alipokea mnamo Januari, kuanzishwa mara moja kwa usitishaji mapigano huko Gaza, kuongeza misaada ya kibinadamu, kuachiliwa kwa mateka na suluhisho la dola mbili kwa amani ya kudumu. Suala la meli ya wadhamini pia liliibuka wakati wa mkutano huo. Kuhusu suala la meli ya wadhamini, Fidan alisema, "Hii inajumuisha pia Uturuki. Acha nchi zengine ziwe wadhamini wa "Israel".

Baada ya kufikia makubaliano ambayo pande zote mbili zitakubaliana juu yake, nchi zilizotoa dhamana zinapaswa kuwajibika kutimiza mahitaji yake. Ni wazi kwamba Fidan anafanya kazi kwa njia ya kuhuzunisha ili kuhakikisha mpango wa Marekani wa suluhisho la dola mbili na usalama wa umbile la Kiyahudi. Wakati huo huo, Hamas imezitaja Uturuki, Qatar, Misri na Urusi kuwa nchi zilizotoa dhamana ya utekelezaji wa makubaliano ya hatua tatu ya kusitisha mapigano kati ya Hamas na umbile la Kiyahudi, ambayo yaliwezeshwa na Misri na Qatar ili kukomesha kile kinachodaiwa kuwa vita kati ya Hamas na "Israel".

Ama Uturuki, ikiwa na kazi iliopewa na Marekani, ilitumia nguvu juu ya baadhi ya makundi yanayopinga utawala wa Syria na kuyapotosha, sasa inafuata sera ya kutumia shinikizo la kisiasa kwa Hamas ili kuishawishi juu ya mipango michafu ya Marekani.

Majaribio haya yote ya kupotosha na hatua zote za kidiplomasia zilizochukuliwa katika suala hili yanajumuisha silaha za kulilinda umbile vamizi. Hatua hizi za uhaini ni kwa ajili ya umbile vamizi la Kiyahudi. Uturuki na tawala zengine za Kiarabu zinatilia maanani sana usalama wa umbile la Kiyahudi. Wanatoa msaada wote wawezao kulidumisha umbile ovu ambalo linachinja na kutekeleza mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu. Kiasi kwamba umbile hilo la Kiyahudi linanunua 60% ya mafuta yake kutoka Azerbaijan na Kazakhstan. Mnamo Oktoba 7 na kabla, zaidi ya mapipa milioni 1 ya mafuta yalisafirishwa hadi umbile la Kiyahudi kupitia Uturuki. Mafuta haya husafirishwa kupitia bomba la Baku–Tbilisi–Ceyhan hadi bandari ya Uturuki ya Ceyhan na kutoka hapo hadi bandari ya Eilat kwa meli za mafuta.

Bila misaada kama hii na usaliti wa dola hizi na watawala wao, umbile la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu halingeweza kuikamata Ardhi Iliyobarikiwa. Umbile la Kiyahudi linapata nguvu ya mauaji yake kutokana na ukimya na uoga wa vyombo hivi vya Marekani. Linaendeleza mauaji huko Gaza lipendavyo kwa sababu lina uhakika kabisa kwamba viongozi wa nchi za Kiislamu hawatachukua hata hatua ndogo dhidi yake. Kwa hivyo, hata kama makumi ya maelfu ya Waislamu watakufa huko Gaza, umbile la Kiyahudi litaendelea kuua na kuangamiza viumbe vyote vilivyo hai na visivyo hai ili kufikia malengo yake ya kijeshi na kisiasa. Wakati huo huo, lina imani kwamba ikiwa umbile la Kiyahudi litafikia malengo yake huko Gaza, watawala wataendelea kuhalalisha mahusiano nalo kana kwamba hakuna kilichotokea na hawatalihesabu kwa umwagaji damu na Waislamu waliouawa shahidi.

Kwa hivyo, suluhisho la dola mbili ndani ya mipaka ya 1967 ni mpango muovu wa Marekani. Utekelezaji mpango huu ni uhalifu na uharamu mkubwa. Suluhisho la kadhia ya Palestina si suluhisho la dola mbili ndani ya mipaka ya mwaka 1967 wala si kuanzishwa kwa dola ya kisekula katika ardhi yote ya Palestina.

Suluhisho thabiti na pekee la kadhia ya Palestina ni kusimamisha Dola ya Khilafah, inayotawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt)!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
YILMAZ ÇELİK

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu