Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uchaguzi wa Urais 2024 na Dosari za Demokrasia nchini Indonesia:

Ni wakati wa Kuregea kwenye Uislamu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Uchaguzi wa urais nchini Indonesia ulifanyika mnamo Februari 14, 2024, na kufikia sasa, kuhesabu kura rasmi kunaendelea na Tume ya Uchaguzi Mkuu. Kulingana na hesabu ya haraka ya matokeo, kuna uwezekano mkubwa kwamba wawili Prabowo Subianto na mwanawe Rais, Gibran, wataibuka washindi.

Maoni:

Wawili hao Prabowo-Gibran wamekuwa na utata nchini Indonesia kwa sababu makamu wa rais ni mtoto wa rais wa sasa. Baadhi ya matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa wale waliokuwa madarakani walipendelea ushindi wa mtoto wa rais kupitia juhudi za kusukuma mbele ugombezi wa Gibran kama makamu wa rais, ambayo mwanzoni inaweza kuwa haikuwa halali. Hili liliafikiwa kupitia mabadiliko ya sheria katika Mahakama ya Kikatiba inayoongozwa na mjombake Gibran, na kuifanya iwe rahisi kwa Gibran kujiandikisha. Zaidi ya hayo, serikali inashukiwa kuchangia mafanikio ya Prabowo-Gibran kwa kuhamasisha watumishi wa umma, maafisa kutoka ngazi mbalimbali za serikali, na kusambaza programu mbalimbali za usaidizi wa kijamii katika miezi ya kabla ya uchaguzi wa rais. Mawaziri wengi pia wanadaiwa kumuunga mkono kwa dhati mgombea huyu.

Kuna wasiwasi mkubwa kwamba kuchaguliwa kwa jozi inayoungwa mkono na rais anayetawala kunaweza kusababisha demokrasia ya Indonesia kuelekea vitendo vya kimabavu. Hasa ikizingatiwa kuwa Rais Joko Widodo amekosolewa kwa kuchangia kushuka kwa ubora wa kidemokrasia wa Indonesia katika muongo mmoja uliopita.

Hadithi hii katika siasa za kidemokrasia si mpya, ambapo viongozi waliochaguliwa hutumia mamlaka yao kwa maslahi binafsi au ya kikundi. Nchini Indonesia, matumizi mabaya ya madaraka na kipote cha wachache kwa ajili ya ubadhirifu kupitia ufisadi limekuwa suala la muda mrefu.

Sio tu kuwa na viongozi wabaya, bali mfumo wa kidemokrasia wenyewe unatoa fursa nyingi kwa watu wasio waadilifu kuingia madarakani na kufanya mambo kiholela. Tangu awali, demokrasia imeundwa kwa njia ambayo wale walio na mamlaka na pesa wanaweza kushinda uchaguzi, na ubora wa viongozi sio kigezo cha msingi. Zaidi ya hayo, usekula kama kanuni ya kidemokrasia hufungua milango kwa wanasiasa wasio waadilifu kujihusisha na siasa chafu. Hatimaye, inaonekana kwamba nguvu za uovu huelekea kutawala katika nchi za demokrasia.

Uislamu umefundisha aina bora ya uongozi unaoegemezwa kwenye imani, unaolenga kuunda jamii inayotenda mema na kukataza maovu, kuanzia watawala hadi mahusiano baina ya watu. Mfumo wa Kiislamu pia unaweza kuwakuza wanasiasa waadilifu wanaomcha Mwenyezi Mungu na kuwajali watu wao kikweli. Umefika wakati kwa Waislamu kukataa demokrasia na kuushikilia Uislamu kama msingi pekee wa kuliongoza taifa.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdullah Aswar

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu