Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wanawake na Wasichana wa Gaza Wameachwa Kutelekezwa katika Udhalilifu na Hofu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Dominic Allen, anayefanya kazi katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu, alikuwa na mahojiano ambayo Middle East Eye iliyachapisha mnamo tarehe 15 Machi 2024. Alisisitiza kwamba alipomaliza muda wake wa huduma katika eneo hilo, "alikuwa na hofu kwa wanawake na wasichana mjini Gaza. Alisisitiza kuwa wanawake 650,000 walio katika umri wa kuzaa wanakabiliwa na tishio kubwa la matatizo na mahitaji ya matibabu kwa kuwa hakuna huduma zinazoweza kukidhi mahitaji ya afya ya wanawake. Hasa, wanawake wanaozaa bila uangalizi mzuri na wanawake waliokomaa ambao hawana bidhaa za usafi kila mwezi. Kizuizi hiki kilichowekwa kwa misaada na bidhaa zinazoingia na kutoka Gaza na umbile la Kiyahudi kimeleta athari mbaya kwa ustawi wa wanawake ambapo imekuwa na athari za kutishia maisha kwa maelfu.

Maoni:

Mateso ya dada zetu Waislamu hayavumiliki kwa viwango vyovyote vya kibinadamu. Ni lazima tutambue heshima kubwa na nafasi ya juu ya Mwanawake Muislamu katika Uislamu. Maisha yake, mali na utu wake vyote vinalindwa chini ya hukmu za Sharia na ukiukaji wake ni miongoni mwa haramu kubwa, kama alivyofafanulia Mwenyezi Mungu (swt). Ibn Majah amepokea kutoka kwa Mu’awiyah bin Jahimiah al-Sulamiy (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake):

أَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي كُنْتُ أَرَدْتُ الْجِهَادَ مَعَكَ أَبْتَغِي بِذَلِكَ وَجْهَ اللَّهِ وَالدَّارَ الْآخِرَةَ، قَالَ: «وَيْحَكَ أَحَيَّةٌ أُمُّكَ؟» قُلْتُ: نَعَمْ، قَالَ: «ارْجِعْ فَبَرَّهَا»، ثُمَّ أَتَيْتُهُ مِنْ الْجَانِبِ الْآخَرِ فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي كُنْتُ أَرَدْتُ الْجِهَادَ مَعَكَ أَبْتَغِي بِذَلِكَ وَجْهَ اللَّهِ وَالدَّارَ الْآخِرَةَ، قَالَ: «وَيْحَكَ، أَحَيَّةٌ أُمُّكَ؟» قُلْتُ: نَعَمْ يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالَ: «فَارْجِعْ إِلَيْهَا فَبَرَّهَا»، ثُمَّ أَتَيْتُهُ مِنْ أَمَامِهِ فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي كُنْتُ أَرَدْتُ الْجِهَادَ مَعَكَ أَبْتَغِي بِذَلِكَ وَجْهَ اللَّهِ وَالدَّارَ الْآخِرَةَ، قَالَ: «وَيْحَكَ، أَحَيَّةٌ أُمُّكَ؟» قُلْتُ: نَعَمْ يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالَ: «وَيْحَكَ، الْزَمْ رِجْلَهَا فَثَمَّ الْجَنَّةُ»

“Nilikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) nikasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nataka kwenda pamoja nawe kwa ajili ya jihad (vita) nikitafuta kwayo Radhi za Mwenyezi Mungu na Akhera. Akasema: “Ole wako! Je, mama yako bado yuko hai?” Nikasema, Ndiyo. Akasema, “Rudi ukamkirimu.” Kisha nikamwendea upande wa pili na nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nataka kwenda kwa ajili ya jihad pamoja nawe, kutafuta kwa njia hiyo Radhi za Mwenyezi Mungu na Akhera. Akasema: “Ole wako! Mama yako bado yuko hai?” Nikasema, Ndiyo. Akasema, “Rudi ukamkirimu.” Kisha nikamwendea kutoka mbele na nikasema, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nataka kwenda kwa ajili ya jihad pamoja nawe, kutafuta kwa njia hiyo Radhi za Mwenyezi Mungu na Akhera. Akasema: “Ole wako! Mama yako bado yuko hai?” Nikasema, Ndiyo. Akasema, “Rudi na ukamkirimu (kaa karibu na miguu yake), kwani hapo ndipo kwenye Pepo.

Wajibu wa kuwalinda wanawake na kuwaangalia si jambo la mtu binafsi tu bali ni suala la Khilafah na Amir wa Waislamu.

Kama tunavyoweza kuona katika kukosekana na ombwe la uongozi wa kweli, wenye nguvu wa Kiislamu ambao unatumikia tu ibada ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa mujibu wa Quran na Sunnah, tunaona jinsi uovu na udhalilishaji unavyotawala maisha ya dada zetu wapenzi, wasafi.

Hali yao mjini Gaza ni shambulizi la kutisha kwa shakhsiya zao kisaikolojia na kimwili.

Maadui wa Uislamu wanajua vyema kwamba mambo ya usafi ni nyeti kwa waumini, na kwa makusudi wanatumia mbinu hizi za kusitisha maji kwa ajili ya udhu, adabu za bafuni na ustawi wa mtu binafsi ili kuongeza fedheha kwa wafuasi wa Sunna ya Mohammad (saw). Ni lazima kuupe kipaumbele wahyi wa Uislamu kwa kusimamisha Khilafah, na hili halipaswi kuwekwa nafasi ya pili baada ya jambo jengine lolote. Hakika ni hitaji la dharura zaidi la wakati wetu kama waja wa Mwenyezi Mungu (swt).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu