Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kila Kilevi ni Khamr (Pombe) na kila Kilevi ni Haram

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Mei 22, 2024, kupitia agizo kuu, Gavana wa Mombasa Abdul Swamad Shariff Nassir alipiga marufuku uingiaji, usambazaji, uuzaji na ulaji wa muguka (aina ya kichocheo maarufu kinachojulikana kama Khat au Miraa) au bidhaa zake Mombasa. Agizo sawia na hilo lilitolewa na magavana wa kaunti za Kilifi na Taita Taveta ambao waliapa kukabiliana na uuzaji na matumizi yake. Baadaye, Rais William Ruto alibatilisha marufuku ya kutatanisha iliyowekwa katika baadhi ya maeneo ya nchi. Ulaji wa miche na majani hayo laini yamelaumiwa kwa ongezeko la masuala ya afya ya akili na kuongezeka kwa matatizo ya kijamii, ikiwemo uhalifu.

Maoni:

Kupigwa marufuku kwa muguka kumezua maandamano katika kaunti inayolima muguka ya Embu, huku wakulima na wafanyibiashara wakilaani hatari ya kufunga biashara kutokana na marufuku hiyo. Hata hivyo, marufuku hiyo imepata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa mashirika ya kidini huku viongozi wa dini ya Kiislamu wakitaka Muguka kuainishwa kama dawa za kulevya. Kichocheo hicho ni zao halali chini ya Sheria ya Mazao ya 2013 na Kanuni za Miraa 2023. Rais Ruto amesema Serikali yake imetenga $3.7m (£3m) katika mwaka huu wa kifedha ili kupanua kilimo cha mairungi nchini.

Katika mtazamo wa kisekula na kibepari, hakuna sababu kwa serikali yoyote kupiga marufuku muguka na vileo vyote. Maadamu viwanda vya kilimo cha mairungi na vileo vinazingatia sheria, basi vinahimizwa kujitanua ili viweze kuchangia kurudisha uchumi. Kwa vile ukulima wa Khat na muguka ni halali katika nchi hii, basi biashara, pamoja na matumizi yake inaruhusiwa kupanuka kama viwanda vyengine mradi tu vizingatie masharti yote ya kisheria yanayohusiana nayo. Ni katika muktadha huu, viongozi kutoka maeneo ya kilimo cha Muguka wamelia kwa kupigwa marufuku! Hili linaonyesha kipimo kibovu cha mfumo wa kibepari linapokuja suala la wema na ubaya kwani mfumo huo unazingatia tu manufaa unayopata. Katika suala hili, muguka ni hatari kwa maisha ya binadamu lakini mfumo wa kibepari unaruhusu kilimo na biashara yake kustawi kwa njia inayowezekana kwa njia rahisi zaidi. Kinyume na Uislamu, mtazamo na kipimo cha matendo ya mwanadamu kinategemea ima halali au haramu. Katika hali hii, ikiwa kitu ni haramu, basi kinaharamishwa kabisa bila kujali manufaa ambayo yanaweza kutoka kwayo.

Wengi wa wanaotafuna muguka na kunywa pombe ni miongoni mwa maskini na hata matajiri wanadai kufanya hivyo ili kupunguza msongo wa mawazo. Ingawa sababu hii haihalalishi binadamu mtukufu kujihusisha na vitendo hivyo, ni kweli kwamba Wakenya wengi maskini hujiingiza katika unywaji wa vileo kama ‘njia ya kutoka’ kwenye matatizo ya kiuchumi. Hii ndio tabanni ya mfumo mbovu wa kiuchumi wa kibepari unaotazama tu uzalishaji wa rasilimali zinazoishia mikononi mwa watu wachache wenye nguvu na kuwaacha wananchi wengine wakiyumba katika umaskini. Uislamu, kwa upande mwingine, umeharamisha wanadamu kupoteza matumaini ya maisha na mfumo wake wa kiuchumi unahakikisha ugavi sahihi na sawa wa rasilimali kwa wote na kutoruhusu watu wachache tu wenye nguvu kunufaika.

Kwa kumalizia, suluhisho la uovu huu liko katika Uislamu. Uislamu kama mfumo unakataza ulaji au matumizi ya kitu chochote kinachoathiri jamii ya wanadamu iwe kiafya au kijamii. Kwa mujibu wa Uislamu, unywaji wa kilevi chochote yaani pombe pamoja na kila kileo ni haram na huhesabiwa kuwa ni miongoni mwa matendo ya Shetani yanayopelekea kuchukiza katika jamii bila kusahau kuwapeleka wanadamu mbali na njia ya haki ya kufuata matamanio na matakwa ya Muumba wetu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu