Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kifurushi Kipya cha Ushuru Kinathibitisha Jinsi Wale Wanaojipamba kwa Neno “Uadilifu” Walivyo Wakatili

(Imetafsiriwa)

Habari:

Waziri wa Fedha wa Uturuki Mehmet Şimşek: “Lengo letu ni kuhakikisha kuwa hakuna eneo ambalo halijatozwa ushuru ili kufikia uadilifu na ufanisi katika utozaji ushuru.”

Kifurushi cha mageuzi kilichotayarishwa na Wizara ya Hazina na Fedha ya Uturuki ni pamoja na vipengee muhimu vya kuimarisha usawa wa ushuru na kuanzisha kanuni za ushuru zinazolenga mtaji. Kifurushi hicho kipya kinaweza kuashiria moja ya marekebisho makubwa zaidi ya ushuru katika miongo miwili na mipango yake inatarajiwa kutoa mapato ya ziada ya dolari bilioni 7, kulingana na ripoti ya Bloomberg. (mashirika)

Maoni:

Kifurushi kipya cha ushuru kinajumuisha masharti ya kina kuanzia mapato ya bahashishi hadi mapato ya upangishaji, kuongeza faini, kuondoa misamaha ya VAT kwenye malisho na mbolea, na kuongeza ada ya kuondoka kwa kusafiri nje ya nchi kwa angalau mara 10. Miundo mipya ya ushuru, kama vile kiwango cha chini cha ushuru wa kampuni na kodi ya kima cha chini cha mapato, itaanzishwa ili kuongeza sehemu ya kodi za moja kwa moja ili kuondoa kile kinachoitwa dhulma ya kodi. Kodi hizi kimsingi zitaathiri biashara ndogo ndogo, sekta ya kilimo, wajasiriamali huru na wafanyikazi. Hata kodi ya lazima ya 20% itatozwa kwa bahashishi zilizopokewa na wafanyikazi wa kima cha chini cha mshahara. Kanuni mpya za ushuru pia zitaanzishwa kwa vifaa vya POS. Ukaguzi wa kila mwezi, robo mwaka na mwaka utafanywa ili kuhakikisha hakuna ushuru unaokwepwa. Malipo ya upangishaji nyumba lazima yafanywe kupitia benki, ambao watatoa 20% moja kwa moja. Adhabu kubwa zitatolewa kwa miamala bila ankara (invoices), huku zawadi kwa watoa taarifa zitaongezwa. Adhabu za kuchelewa kwa malipo zitatumika kwa faini zote za usimamizi. Ushuru utatozwa kwa kila kipengele na umbo linalohusisha pesa. Kwa mukhtasari, ushuru huu utatozwa karibu kila pumzi ambayo watu wanavuta. Ingawa haya yote yanadaiwa kufanywa ili kupunguza mfumko wa bei, bila shaka itaongeza gharama ya maisha hata zaidi.

Mwaka huu, ilibainika kuwa deni la benki, taasisi na makampuni hayo, ambalo kwa jumla limefikia zaidi ya bilioni 3 YTL, lilifutwa kwa asilimia 97.6 - yaani, karibu kufutwa kabisa. Miongoni mwao, kuna makampuni yanayounga mkono ya Mayahudi, na Wazayuni, kama vile UNILEVER (madeni ya kodi yamefutwa kwa 100%).

Uadilifu ni fahamu tupu katika nchi hii ambayo ipo tu kwa jina la chama tawala na kwa jina la mfumo wa mahakama unaowakandamiza Waislamu.

Uadilifu katika uchumi hufanya kazi kwa benki na mali zenye msingi wa mitaji ya magharibi pekee. Dhana ya maendeleo ya adilifu/sawa ya kiuchumi ni mdogo katika kuridhia mikataba ya kimataifa kama malipo ya mikopo ya mabilioni ya dolari kutoka IMF na Benki ya Dunia, ambayo hutolewa kwa kubadilishana na kuuza rasilimali za madini za nchi kwa makampuni ya kigeni, na kuharibu kilimo na ufugaji na hivyo kuishutumu nchi kwa njaa kupitia kutunga sheria kama vile Sheria ya Tabianchi... Na makubaliano ya kimataifa, ambayo yanaagiza marekebisho ya mfumo wa elimu, mfumo wa sheria, na kanuni za kiraia, ambayo yanalenga kutia umagharibi na kufisidi maadili na akhlaki za jamii. Ili kulipa madeni haya, ambayo husababisha ongezeko la nakisi ya bajeti, rasilimali za nishati hubinafsishwa, ambayo matokeo yake huongeza bei kwa njia ya kodi ya moja kwa moja kwa bidhaa za watumiaji, na hivyo kuweka mzigo tena kwenye mabega ya watu wa kipato cha kati na cha chini, na huongeza umaskini.

Sehemu yake pia ni kufuta madeni ya kodi ya mabilioni ya dolari ya makampuni yanayowaunga mkono Wazayuni na makampuni yanayounga mkono Wazayuni ili kuhujumu juhudi za Waislamu wanaosusia kufanya biashara na umbile linalokalia kwa mabavu la Kizayuni. Kwa hakika, kuongeza biashara huria na umbile vamizi la Kizayuni lenye kutekeleza mauaji ya halaiki kwa kusema “Tunauza 6 na tunanunua 1” ndivyo namna sera za ulafi za “uadilifu na maendeleo” zinavyotafsiri fahamu ya uadilifu.

Uadilifu katika siasa ni kulaani tu kuchomwa moto kwa watoto wachanga wa Gaza wakiwa hai, na kutoa wito wa suluhisho la dola mbili na kutekeleza sera za uhalalishaji mahusiano.

Ufahamu wa mfumo wa mahakama wa Uturuki kuhusu uadilifu ni kuwaadhibu Waislamu wanaopinga ukatili unaofanywa dhidi ya Waislamu nchini Uturuki na duniani kote, na kuwaachilia huru wanasiasa wanaolaghai umma, na kuwaachilia kwa umma kupitia adhabu za kejeli, wale wanaojihusisha na ukahaba unaolipa ushuru, na wanaouza pombe na madawa ya kulevya, na wanaoiba, na wanaobaka wanawake na wasichana. Na, ni kuwatangaza Waislamu wenye fikra za Kiislamu, na wanaotamani maisha ya Kiislamu, ambao hawajatenda jinai yoyote, kuwa ni magaidi na kuwahukumu kwenye dhulma, mateso na kifungo...

Huu ni ufahamu wa kilafi wa uadilifu na maendeleo wa “Muislamu poa” lakini serikali imara ya kisekula ya kidemokrasia. Kwa kumalizia, kifurushi hiki kipya cha ushuru ni uthibitisho wa jinsi wale wanaojipamba kwa neno uadilifu walivyo wakatili.

Kwa maneno na matendo ya watumishi hawa wa kibepari na watawala wasaliti, neno uadilifu ni kibandiko tu kinachotumika kuwahadaa watu wao. Hata hivyo, “uadilifu” ni sifa mojawapo ya Mwenyezi Mungu (swt), ambaye ni “Al-Adl”, Muumba, Mmiliki (Malik) na Mola wa walimwengu wote, na ni fahamu ambayo inaweza tu kuwa hai kwa wanadamu wote kwa kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa Uislamu; kukusanya kodi mfululizo, moja kwa moja na kwa njia isiyo ya moja kwa moja, ni dhulma. Ikiwa mapato ya serikali hayakidhi mahitaji ya raia, hapo tu ndio kodi inaweza kutozwa. Kodi hii inaweza tu kukusanywa kutoka kwa watu matajiri na Waislamu, ambao wanaweza kukidhi mahitaji yao wenyewe. Kutoka kwa wasiokuwa Waislamu, ni jizya pekee inayoweza kukusanywa. Ikiwa kuna ziada katika mapato ya Bayt al-Mal (hazina ya dola), ushuru huu hupunguzwa au kukomeshwa.

Kwa maana nyengine, bila ya kuufanya Uislamu kuwa wenye kuongoza, kuhukumu na kutawala tena juu ya ardhi, na bila ya kuwaondoa hawa watawala wa Ruwaybidha na kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itaregesha maisha kamili ya Kiislamu kwa kutekeleza mfumo wa Uislamu, wanadamu hawataweza kuonja uadilifu katika nyanja yoyote ya maisha.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zehra Malik

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu