Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Sintofahamu ya Benki ya Maziwa ya Binadamu: Khilafah kwa Njia ya Utume Inatatua Matatizo ya Kibinadamu kwa Kuregelea Uislamu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Gazeti la ‘The Daily Times’ liliripoti kuwa, “Sindh anasimamisha benki ya maziwa ya binadamu, inauregesha mpango huo kwa Baraza la Itikadi la Kiislamu... Benki ya kwanza ya maziwa ya binadamu nchini Pakistan iliundwa mapema mwezi huu na Taasisi ya Sindh ya Afya ya Mtoto na Matibabu ya Watoto (Neonatology) ... Kituo kilianzishwa kwa ushirikiano na UNICEF, iliyosifiwa kama 'hatua muhimu katika afya ya uzazi'... “Fatwa iliyorekebishwa hivi majuzi iliyotolewa na Darul Uloom Karachi ya tarehe 16 Juni 2024 imetusukuma kusitisha utendakazi wa Benki ya Maziwa ya Binadamu. Uamuzi huu unazingatia mwongozo wa kidini uliosasishwa na unaoakisi kujitolea kwetu kunakoendelea kufanya kazi ndani ya mfumo wa fiqh ya Kiislamu,” SICHN ilisema katika taarifa ya Juni 21.” (Chanzo: https://dailytimes.com.pk/1202974/sindh-suspends-human-milk-bank-refers-initiative-to-islamic-ideology-council/)

Maoni:

Kama ilivyo katika Ulimwengu wote wa Kiislamu, serikali ya kisekula ya Pakistan inaendelea kuruhusu sheria na sera zinazokinzana na Quran Tukufu na Sunnah za Mtume. Kisha inawaangukia Waislamu kugundua migongano hii, kisha wanapaza sauti na kilio, mpaka kuwe na utenguzi. Ni pale tu Waislamu wanapotoa tetesi, ndipo serikali ya kisekula inaacha kimya chake, na kulazimika kuchukua hatua za kuwatuliza Waislamu. Katika kesi hiyo, Benki ya Maziwa ya Binadamu ilianzishwa chini ya pua ya serikali, na taasisi ya kikoloni, UNICEF. Kisha Waislamu wakaibua wasiwasi, kwani wanafahamu kwamba watoto wanaozaliwa na mama tofauti, lakini wakanyonyeshwa na mwanamke mmoja, ni marufuku kuoana, pindi masharti fulani yakitimizwa.

Kuna njia nyingi za Halaal za kutatua matatizo yetu, ndani ya yale ambayo Uislamu umetoa hukmu. Tunaweza kutengeneza sajili ya mayatima, na sajili ya wanawake ambao wako tayari kunyonyesha. Kisha tunaweza kupanga mawasiliano kati yao. Kwa njia hii mama anayetoa maziwa anajulikana kwa mtoto. Hivyo katika siku zijazo, ndoa inaweza kuamuliwa, kuepuka ndoa na ujamaa kupitia kunyonya. Hili linaweza kufanywa katika ngazi ya mtaa kupitia madaktari wa watoto na wauguzi, miongoni mwa wahudumu wengine wa afya. Kimsingi, mara nyingi tuna hekima, lakini Mwenyezi Mungu (swt) ni Al-Hakeem, Mwingi wa hekima.

Tofauti na serikali ya kisekula, Khilafah Rashida kamwe isingeruhusu kuanzishwa kwa Benki ya Maziwa ya Binadamu, ambapo maziwa yanayotolewa kutoka kwa kina mama wengi huchanganywa katika chombo kimoja, bila ya kutambua na kubainisha maziwa ya wachangiaji tofauti, katika vyombo tofauti. Inajulikana vyema kuwa muundo wa sasa wa benki ya maziwa ya binadamu, au (lactarium), unategemea wachangiaji wasiojulikana, huku michango ya maziwa ikichanganywa. Khilafah huchunguza mapendekezo ya kimatibabu kwa msingi wa nususi za Wahyi, kwa kutilia maanani maneno ya Maswahaba (ra) na Maulamaa wa Kale, wakati wa kupima rai yenye nguvu zaidi.

Unyonyeshaji, unaoharamisha ndoa, ni ule unaojaza tumbo. Mtume (saw) amesema,

«لَا يُحَرِّمُ مِنْ اَلرَّضَاعَةِ إِلَّا مَا فَتَقَ اَلْأَمْعَاءَ, وَكَانَ قَبْلَ اَلْفِطَامِ»

Unyonyeshaji unaoharamisha ndoa ni ule unaofika tumboni, na huchukuliwa kabla ya kumwachisha ziwa.” [Tirmidhi] Unyonyeshaji unaozingatiwa ni ule ulio ndani ya miaka miwili ya Hijria ya kuzaliwa, kabla ya kuachishwa kunyonya. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[حَوْلَيْنِ كَامِلَيْنِ لِمَنْ أَرَادَ أَنْ يُتِمَّ الرَّضَاعَةَ]

“Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kaamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha.” [Surah Al-Baqarah 2:233].

‘Aa’ishah (ra) amesema, “كَانَ فِيمَا أُنْزِلَ مِنْ الْقُرْآنِ عَشْرُ رَضَعَاتٍ مَعْلُومَاتٍ يُحَرِّمْنَ ثُمَّ نُسِخْنَ بِخَمْسٍ مَعْلُومَاتٍ” “Miongoni mwa mambo yaliyoteremshwa katika Qur’an ni kwamba kunyonyesha mara kumi kwa uhakika humfanya mtu kuwa Mahram, kisha ikafutwa na kubadilishwa kwa kunyonyesha mara tano.” [Muslim]

Ibn Qudaamah (rh) amesema, الرضاع الذي لا يشك في تحريمه، أن يكون خمس رضعات فصاعدا"” “Idadi ya kunyonyesha ambayo hapana shaka kuhusiana nayo kwamba inathibitisha uhusiano wa Mahram ni tano au zaidi.”

An-Nawawi (rh) amesema, اخْتَلَفَ الْعُلَمَاء فِي الْقَدْر الَّذِي يَثْبُت بِهِ حُكْم الرَّضَاع , فَقَالَتْ عَائِشَة وَالشَّافِعِيّ وَأَصْحَابه : لا يَثْبُت بِأَقَلّ مِنْ خَمْس رَضَعَات  “Ulamaa wengi wamekhitalifiana kuhusu idadi ya kunyonyesha ambayo hukmu yake ya kunyonyesha (radaa ́ah) inatumika. ‘Aaishah na al-Shaafa’i na maswahaba zake wamesema kwamba hakuna uthibitisho wa idadi yoyote chini ya tano.”

An-Nawawi (rh) akaongeza, وَقَالَ جُمْهُور الْعُلَمَاء يَثْبُت بِرَضْعَةٍ وَاحِدَة . حَكَاهُ اِبْن الْمُنْذِر عَنْ عَلِيّ وَابْن مَسْعُود وَابْن عُمَر وَابْن عَبَّاس وَعَطَاء وَطَاوُسٍ وَابْن الْمُسَيِّب وَالْحَسَن وَمَكْحُول وَالزُّهْرِيّ وَقَتَادَة وَالْحَكَم وَحَمَّاد وَمَالِك وَالأَوْزَاعِيّ وَالثَّوْرِيّ وَأَبِي حَنِيفَة رَضِيَ اللَّه عَنْهُمْ  “Wanazuoni wengi wamesema kuwa hukmu inatumika ikiwa kunyonyesha kutapatikana mara moja. Haya yamepokewa na Ibn al-Mundhir kutoka kwa Ali, Ibn Mas'uud, Ibn Umar, Ibn Abbaas, 'Ata', Tawoos, Ibn al-Musayyib, al-Hasan, Makhool, al-Zuhri, Qataadah, Hammaad, Maalik, al-Awzaa ́i, al-Thawri na Abu Hanifah – Allah awe radhi nao.”

Kwa hivyo katika Khilafah Rashida, mtawala atachunguza dalili na kuzingatia rai. Kisha atachukua rai yenye nguvu zaidi katika mtazamo wake, na itawafunga Waislamu chini ya utawala wake. Iwapo atatabanni hukmu ya Shariah, hukmu hii peke yake inakuwa ndio hukmu ya Shari’ah ambayo lazima itekelezwe. Inakuwa ndio sheria inayofunga ambapo kila raia lazima aitii kwa hadharani na kwa faragha.

Dalili ya kutabanni kwa Khalifah inatokana na Ijma’ (Makubaliano ya Jumla) ya Maswahaba (ra). Khalifa ana haki ya kutabanno hukmu maalum za Shari’ah. Vile vile imethubiti kwa namna hiyo hiyo kwamba ni wajibu kuzifanyia kazi hukmu zilizotabanniwa na Khalifa. Muislamu haruhusiwi kuifanyia kazi hukmu yoyote, isipokuwa ile iliyotabanniwa na Khalifa katika upande wa hukmu, hata kama hukmu hizo ni hukmu za Shari’ah zilizotabanniwa na mmoja wa Mujtahidina (Ulamaa wa Uislamu). Hii ni kwa sababu hukmu ya Mwenyezi Mungu (swt) ambayo inawafunga Waislamu wote ni ile ambayo Khalifa ameitabanni. Khulafah Rashidun (ra) waliendelea namna hii. Walitabanni idadi ya hukmu maalum na kuamuru utekelezaji wake.

Hakuna mchakato wowote wa sheria ya Kiislamu unaotokea katika dola ya kisekula, kwa sababu hukmu huamuliwa kwa rai ya walio wengi, bila kujali Dini ya Uislamu. Kisha tunateseka chini ya kile kinachoitwa hekima ya wanadamu, badala ya kuishi maisha ya utulivu chini ya hukmu za Mwingi wa hekima, Al-Hakeem, Mwenyezi Mungu (swt). Amesema Mwenyezi Mungu (swt),

[وَعَسَى أَنْ تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَكُمْ وَعَسَى أَنْ تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَكُمْ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ]

“Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.” [Surah Al-Baqarah 2:216]. Hivyo basi Waislamu wanaotaka kuishi chini ya Dini ya Uislamu, wafanye kazi ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musab Umair - Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu