Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Firauni Rahmon Awawinda Vijana wa Kiislamu nchini Tajikistan

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Oktoba 1, shirika la habari la ‘Current Time’ liliripoti hivi: “Nchini Tajikistan, maafisa na watumishi wa umma wana kazi ya kufanya uchunguzi wa nyumba kwa nyumba na kuwaelimisha watu kuhusu itikadi kali na msimamo mkali. Katika jimbo la Khatlon kusini mwa nchi, uongozi umewateua watumishi wa umma 1,800 - wengi wao wakiwa wa elimu, huduma za afya na wajumbe wa baraza la mitaa – ili kufanya mazungumzo kama hayo.

Maafisa wanadai kuwa lengo pekee la mazungumzo hayo ni kuzuia misimamo mikali ya vijana. Katika mikutano pamoja na watu, wanajadili mada ya vazi la kitaifa la wanawake (mamlaka zinalipigia debe badala ya hijabu, wakiamini kwamba hijabu huvaliwa na watu wenye itikadi kali), wanauliza kuhusu jamaa wanaoishi nje ya nchi na wanaoweza kuwa watu wenye misimamo mikali ya kidini, na pia kuwachochea vijana kuhudumu jeshini.

Mkuu wa jimbo la Khatlon, Davlatali Said, aliripoti mapema kwamba maafisa wanaofanya mazungumzo ya kampeni wamepitia kozi maalum za kuwasiliana na watu. “Kutoa mafunzo kwa vikundi hivi katika wilaya zote, tulifanya semina kwa kushirikisha wataalamu. Mwongozo pia umeandaliwa,” alionyesha. “Katika miezi saba ya kwanza ya mwaka huu, vikundi hivyo vilitembelea karibu nyumba 622,000.”

Maoni:

Majaribio ya dhalimu Rahmon ya kusitisha mwamko wa Uislamu miongoni mwa watu yanafanana na wazimu wa Firauni wa Misri. Baada ya kujua juu ya utabiri kwamba maangamivu yake yangetoka kwa mwanamume aliyezaliwa kati ya wana wa Israeli, Firauni, akiwa ameshikwa na hofu, aliamuru wavulana wote wanaozaliwa wauawe. Askari wake waliwaua kikatili watoto wachanga wa kiume, bila kumsaza yeyote.

Leo, Firauni wa Tajikistan, Rahmon, akiwaona watu wakigeukia Uislamu, anaelekeza nguvu zake zote kuwatenganisha watu na Dini. Anatumia jeshi, polisi, maimamu walio chini yake, televisheni na vyombo vyote vya serikali. Sasa hivi anawatumia hata watumishi wa umma, kuwapeleka majumbani kuwakataza vijana kuusoma Uislamu na wanawake kuvaa hijabu. Wale wanaolingania Uislamu wanatuhumiwa kwa itikadi kali na ugaidi.

Utozaji faini nzito kwa kuvaa hijabu katika maeneo ya umma, mashtaka ya jinai kwa wazazi ambao watoto wao huhudhuria misikitini, vifungo vya jela kwa kuulingania Uislamu, mateso na unyanyasaji magerezani - yote haya hayawatishi Waislamu wa Tajikistan. Kinyume chake, watu wanavutwa kwenye Uislamu kwa hamu kubwa zaidi baada ya kila tishio jipya kutoka kwa Firauni Rahmon. Uhalisia huu unathibitisha tena kwamba Umma wa Kiislamu una shauku ya kuishi kwa mujibu wa sheria za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, na uko tayari kuhuisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu licha ya matatizo na vikwazo vyote.

[يُرِيدُونَ أَن يُطْفِؤُواْ نُورَ اللّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللّهُ إِلاَّ أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ]

“Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.” [9:32]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu