- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Marekani kwa mara Nyengine tena Imelila Sanamu la "Sheria ya Kimataifa"
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mnamo Jumapili usiku, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza "mafanikio ya mashambulizi ya mabomu" ya Jeshi la Anga la Marekani katika maeneo matatu muhimu katika mpango wa nyuklia wa Iran. (BBC)
Maoni:
Mashambulizi haya ya Marekani dhidi ya ardhi ya Iran, bila ya kujali kisingizio ambacho yalifanyika chini yake, ni kielelezo tosha kwamba ile inayoitwa sheria ya kimataifa si chochote zaidi ya udanganyifu; ambayo madhumuni yake ni kuhalalisha ukoloni wa dola dhaifu na na dola kuu.
Wakati kunapokuwa na maafikiano kati ya wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya suluhisho la tatizo fulani la kimataifa, wanapitisha azimio linalolingana na Baraza hili na kutekeleza kwa nguvu utashi wao chini ya kivuli cha uhalali. Katika hali kama hiyo, kila mtu anazungumza juu ya ukuu wa sheria ya kimataifa.
Hili lilitokea, kwa mfano, kwa Azimio Na. 1973, ambalo liliruhusu kupinduliwa kwa dikteta wa Libya Muammar Gaddafi.
Ikiwa dola kuu hazikubaliani kati yao wenyewe na haziwezi kukubaliana juu ya msimamo uliounganishwa na uratibu wa matumizi ya nguvu za kijeshi, basi sheria ya kimataifa mara moja inageuka kuwa kauli mbiu tupu ambayo inaweza kupuuzwa kwa urahisi.
Chengine mithili ya hiki kilitokea mwaka wa 2003, wakati Marekani, baada ya kushindwa kulifanya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio sawia, iliamua kuivamia nchi huru ya Iraq kipeke yake. Kabla ya hapo, mnamo 1999, NATO iliivamia Yugoslavia, Urusi iliivamia Georgia mnamo 2008, na Ukraine mnamo 2014 na 2022.
Kila wakati jambo kama hili linapotokea, nchi hiyo vamizi hujaribu kuwasilisha jinai zake katika pazia nzuri ya kuwajali raia, kuregesha haki iliyokanyagwa na kauli mbiu nzuri nyenginezo.
Kwa mfano, mgogoro wa Ukraine ni mfano wa mapambano makali na ushindani kati ya dola kuu ndani ya mfumo wa kile kinachoitwa "tatizo la Ulaya". Urusi, kwa kuzingatia kwamba kufuata sheria za kimataifa kunaleta tishio kwa uwepo wake, iliamua kuivamia Ukraine, ikipuuza mikataba na majukumu yake yote ya kimataifa.
Ama kuhusu mashambulizi ya Iran, sasa Marekani kwa mara nyengine tena imeitupilia mbali "sheria ya kimataifa" chini ya miguu yake. Kwa kweli, dola ya kinyuklia Marekani, pamoja na umbile la Kiyahudi, ambalo hadhi yake ya kinyuklia inapuuziwa, wanalazimisha kiupande mmoja matakwa yao kwa nchi nyengine huru. Ni muhimu kuashiria kuwa, ninachukua zaidi ya upeo wa makala haya ukweli kwamba hujuma hii ya Marekani dhidi ya Iran inafanyika licha ya ukweli kwamba katika miongo kadhaa iliyopita Iran imekuwa kwa hakika mmoja wa wasimamizi wakuu wa sera za Marekani katika Mashariki ya Kati.
Kwa upande mmoja, Marekani inapinga azimio lolote la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalolaani umbile la Kiyahudi, licha ya ukweli kwamba "mtoto huyo aliyeharibika wa Marekani" anafanya kila uhalifu wa kivita unaowezekana dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Kwa upande mwingine, kwa kutambua kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kutokana na haki ya kura ya turufu, mara hii ya Urusi, kamwe haitapitisha azimio la kuidhinisha matumizi ya nguvu za kijeshi dhidi ya Iran; inashambulia kipeke yake vituo vyake vya nyuklia.
Hoja ni kwamba fahamu ya "sheria ya kimataifa" haiwezi kuwepo, kwa sababu fahamu za "kimataifa" na "sheria" haziwezi kuendana. Kuna sababu tatu za hili:
1. Sheria ni kifungu cha kisheria cha kawaida ambacho kinapitishwa na chombo wakilishi (cha sheria), yaani mtawala. Mtawala wa kimataifa hawezi kuwepo kabla.
2. Sheria lazima itekelezwe, yaani kuwe na chombo cha kutekeleza sheria. Ndani ya dola, chombo kama hicho ni asasi za kutekeleza sheria. Kwa kiwango cha kimataifa, hili haliwezekani, kwa kuwa "vikosi vya kulinda amani" vya leo ni muundo unaojumuisha vikosi vya kijeshi vya dola binafsi binafsi. Navyo, kwa upande wao, hawatalinda sheria ya kimataifa au, kwa mfano, ubwana na maslahi ya dola nyenginezo, ikiwa ulinzi huu utakuwa kuwa tishio kwa serikali zao au kugongana na maslahi yao, kama, kwa mfano, katika mzozo wa Ukraine na ukiukaji wa mkataba wa Budapest na mvamizi - Shirikisho la Urusi, na watiaji saini wengine wa makubaliano haya.
3. Sheria hii inasimamia (inaunganisha) mahusiano. Udhibiti huu unafaa katika mahusiano kati ya wawakilishi wa jamii moja maalum, na hauwezi kutumika wakati wawakilishi hawa ni dola tofauti tofauti, kwa kuwa kila dola ina haki ya ubwana wa kuanzisha mahusiano au kuyaepuka na dola fulani kulingana na maslahi yake.
Tangu kuibuka kwa wazo la sheria ya kimataifa, kumekuwa na kutokubaliana kati ya wasomi wa sheria wa Magharibi kuhusu dhati ya sheria zake. Wengi walitilia shaka nguvu yake ya kufungamanisha. Kwa mfano, wanasheria na wanafikra wa Magharibi I. Kant, T. Hobbes, J. Austin na G. Hegel walikanusha uwepo wa sheria jumla ya kimataifa.
Hata hivyo, baadaye, chini ya shinikizo la kushawishi wazo hili na dola kubwa, likaanzishwa katika mahusiano ya kimataifa.
Matokeo yake, sheria ya kimataifa pamoja na taasisi zake zote zimekuwa chombo cha ushindani na mapambano kati ya dola kama vile Marekani, Urusi, Uingereza, Ufaransa na China. Dola nyenginezo, watu wao, rasilimali na maeneo zimekuwa wahasiriwa wa matumizi ya kihalifu ya chombo hiki wa dola hizi.
Hii ndiyo hasa sababu kuu ya ukosefu wa utulivu uliogubika pembe nyingi za dunia hivi sasa, ambapo mateso ya watu wa Palestina; Iran au Ukraine ni sehemu ndogo tu ya silsila isiyo na mwisho ya uhalifu wa dola kubwa zenye nguvu.
Imetafsiriwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fazil Amzaev
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine