Jumapili, 15 Muharram 1446 | 2024/07/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Srebrenica Miaka 25 Baadaye... Lini Tutakoma Kusema 'Kamwe Haitatokea Tena' kwa Mauwaji ya Halaiki Dhidi ya Ummah Wetu?

Habari:

Julai 2020 inakamilisha miaka 25 ya kumbukumbu ya mauwaji ya halaiki ya Srebrenica, ambapo majeshi ya Serbia yaliingia katika eneo la Srebrenica, lililotengwa kama 'eneo salama' na Umoja wa Mataifa wakati wa vita vya Bosnia, na matokeo yake wakawauwa kinyama wanaume na wavulana wa Kiislamu 8000 katika maeneo yaliyo pambizoni mwa kaskazini mashariki mwa Bosnia. Kufuatia mauwaji hayo, yaliyosifiwa kuwa tukio baya zaidi la mauwaji ya halaiki barani Ulaya baada ya Vita vya Pili vya Dunia, ulimwengu uliweka ahadi: kamwe haitatokea tena. Lakini, tunaishi katika ulimwengu ambao mauwaji ya halaiki ya Waislamu mjini Srebrenica yanajirudia katika ardhi kote duniani – kuanzia Syria hadi Myanmar, Gaza hadi Kashmir, Yemen hadi Afrika ya Kati; na ambako kampeni za mauwaji ya kimbari na mateso ya kidini yameshamiri dhidi ya Waislamu eneo la Turkestan Mashariki, India, Urusi, Crimea na kwengineko. Sasa lini tutasema kwa dhati, "Kamwe Haitatokea Tena" kwa uchinjaji na ukandamizaji wa halaiki wa Ummah wetu wa Kiislamu? 

Maoni:

"Kamwe Haitatokea Tena" inamaanisha… kumaliza kile kilichoruhusu maelfu ya wanaume, wanawake na watoto wa Kiislamu kuuwawa nchini Bosnia, na ambacho kiliwezesha kutokea kwa mauwaji ya halaiki dhidi ya Waislamu – kukosekana kwa nidhamu ya Mwenyezi Mungu (swt), Khilafah, ulimwenguni, ngao na mlinzi wa Waumini inayo wajibishwa kuhami damu ya Waumini na kusimama kwa ajili ya maslahi ya Uislamu na mahitaji ya wanadamu. Ni nidhamu hii ya Kiislamu ndio iliyoweka amani, maendeleo na umoja baina ya watu wa makabila, mbari na dini tofauti tofauti katika Balkan kwa zaidi ya miaka 500 kutokana na uadilifu wa sharia za Kiislamu. Hii ndio sababu mwanahistoria wa Kiingereza T.W. Arnold katika kitabu chake, 'The Preaching of Islam', aliandika kuhusu muamala wa wasiokuwa Waislamu walioishi chini ya Khilafah Uthmani: "…japokuwa Wagiriki kiidadi walikuwa wengi kuliko Waturuki katika mikoa yote ya Ulaya ya himaya hii, uvumilivu wa kidini waliopewa, na ulinzi wa uhai na mali walioufurahia, punde tu uliwaowanisha kufadhilisha utawala wa Sultan kuliko ule wa dola yoyote ya Kikristo". Ni dola hii ndio ambayo haukuwahami tu Waislamu waliokandamizwa pekee kama Uislamu unavyo wajibisha, na kama tulivyoona katika matendo ya karne ya 12 ya Khalifah wa Kiuthmani Suleyman, wa kwanza, aliyetuma msururu wa manuari 36 kuwaokoa Waislamu 70,000 wa Al-Andalus ambao walikuwa wakiteswa na watawala wa Kikristo na kuwapa makao katika ardhi za Khilafah… bali ilikuwa ni dola ambayo pia iliitikia vilio vya wasiokuwa Waislamu waliokuwa wanakandamizwa, kama tulivyoona mnamo 1492, chini ya Khilafah Uthmani, Khalifah Bayezid wa pili, aliyetuma zana zake zote za majini ili kuwaokoa Mayahudi 150,000 wa Ulaya waliokuwa wakiteswa na watawala Wakristo wa Uhispania na pia kuwapa makao ndani ya Khilafah.

"Kamwe Haitatokea Tena" inamaanisha… kupinga fahamu yenye sumu ya utaifa na siasa zenye muundo wa dola za kitaifa zilizopekea Balkan kuwa tanuri la uhasama na mizozo ya kikabila, na ambazo ziliwatia msukumo Waserbia kutekeleza kampeni ya mauwaji ya kimbari dhidi ya Waislamu wa Bosnia ili kuunda ruwaza yao ya Serbia Kuu katika eneo lililotakasika kutokana na yeyote asiye Mserbia kando kando ya Mto Drina.

Ni fahamu hii yenye sumu ya utaifa na kupandikizwa kwa vitambulisho na mipaka bandia ya kitaifa iliyo lazimishwa na Wamagharibi baina ya ardhi zetu za Kiislamu ndizo zinazo sababisha Saudi Arabia kuwaacha na njaa hadi kufa ndugu zao wa Kiislamu nchini Yemen – kutokana na maslahi yao ya kitaifa na maslahi ya kitaifa ya mabwana zao wa Kimagharibi; na ndizo zinazozisukuma nchi za Waislamu kama vile Bangladesh, Malaysia, na Indonesia kuwafukuza Waislamu wa Rohingya wanaotapata katika ardhi zao, na kuwatazama wakizama baharini kwa sababu wanawaona kama madhara kwa maslahi yao ya kitaifa na uchumi wao; na ndizo zinazo sababisha serikali za Waislamu kama Uturuki, Misri, Jordan, Pakistan na nyenginezo kuwatazama kaka zao na dada zao wa Kiislamu wakiuwawa eneo la Ash-Sham au Waislamu wa Uyghur milioni 1 wakifungwa katika kambi za uhamasishaji eneo la Turkestan Mashariki – na kutofanya lolote kuwahami kwa sababu si katika maslahi yao ya kitaifa kufanya hivyo! Ni fahamu ovu na ya kuchukiza iliyoje hii! Mtume (saw) amesema:

«لَيْسَ مِنَّا مَنْ دَعَا إِلَى عَصَبِيَّةٍ وَلَيْسَ مِنَّا مَنْ قَاتَلَ عَلَى عَصَبِيَّةٍ وَلَيْسَ مِنَّا مَنْ مَاتَ عَلَى عَصَبِيَّةٍ»

“Si katika sisi anayelingania Assabiyah (Ukabila na Utaifa), na si katika sisi anayepigana kwa ajili ya Assabiyah na si katika sisi anayekufa kwa ajili ya Assabiyah.” (Abu Dawud)

 Na "Kamwe Haitatokea Tena" inamaanisha… kukataa kuzitegemea serikali za kigeni kututatulia matatizo yetu kama Ummah – ima iwe ni kupitia Umoja wa Mataifa (UN) au serikali za kimagharibi kibinafsi. Kiwango cha kuhusika dola hizo katika uhalifu dhidi ya Waislamu kilidhihirika katika vita vya Bosnia kama ilivyo kuwa katika mizozo ya zamani na ya sasa. Tumeona kwa mfano, jinsi gani Umoja wa Mataifa ulivyo wapokonya silaha wapiganaji wa Bosnia mjini Srebrenica huku ukiwaacha Waserbia wakiwa na silaha na kuweza kupata zana za kijeshi kutoka kwa washirika wao, na jinsi gani Umoja wa Mataifa ulivyo watelekeza Waislamu wa Srebrenica kwa wachinjaji wa Kiserbia, licha ya kuahidi kuwalinda. Raisi wa Zamani wa Baraza la Uraisi nchini Bosnia na Herzegovina, Dkt. Harith Siladic alizungumzia kuhusu dori chafu ambayo dola kuu ziliicheza katika vita hivi na kuegemea kwa Umoja wa Mataifa upande wa Waserbia, na jinsi gani Waserbia walikuwa wakipokea usaidizi kutoka kwa dola kuu kama Ufaransa na Uingereza. Sylvie Matton, mwandishi wa kitabu kimoja kuhusiana na khiyana ya Srebrenica, "Srebrenica: An announced Genocide", aliandika kuhusu namna dola kuu zilivyo shirikiana kumpa kiongozi wa Serbia, Slobodan Milosevic, kile alichotaka: maeneo matatu ya Bosnia ya Srebrenica, Zepa na Gorazde. Mwenyezi Mungu (swt) anatwambia:

 (وَالَّذينَ كَفَرُواْ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ إِلاَّ تَفْعَلُوهُ تَكُن فِتْنَةٌ فِي الأَرْضِ وَفَسَادٌ كَبِيرٌ)

“Na wale walio kufuru ni marafiki wenyewe kwa wenyewe. Msipo fanya hivi itakuwako fitna katika nchi na fisadi kubwa.” [Al-Anfal: 73] Na hakika, mara kwa mara tunashuhudia muungano huu wa serikali za kikafiri dhidi ya Waislamu na Uislamu – kuanzia kushirikiana kwao dhidi ya mapinduzi ya Kiislamu nchini, Syria, hadi usaidizi wao na ulinzi wao kwa umbile la 'Kizayuni', hadi kuzuia ushindi wa jeshi la Pakistan dhidi ya India eneo la Kashmir kama tulivyoona kipindi cha mzozo wa milima ya Kargil.

Urithi huu wa kuvunja moyo wa mauwaji ya halaiki yaliyousibu Ummah wetu kamwe hauwezi kukomeshwa isipokuwa tujifunze mafunzo ya kweli kutoka katika historia na kutoka katika dini yetu… nayo ni kuwa usalama na ulinzi wa Waislamu kamwe hauwezi kupatikana mpaka tuyakataye machimbuko yote yasiokuwa ya Kiislamu ya masuluhisho ya matatizo yetu na upangiliaji wa ardhi zetu, na badala yake kuweka umakinifu na juhuzi zetu zote katika kusimamisha kwa haraka dola na nidhamu inayounganisha itokayo kwa Mwenyezi Mungu (swt) iwe ndio ngao yetu, mlinzi wetu na mlezi wetu: Khilafah!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

#Srebrenica25YearsOn  #Srebrenitsa25Yıl   #SrebrenicaMiaka25Baadaye سربرنيتشا_جرح_لم_يندمل#

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 26 Julai 2020 17:54

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu