- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Vichwa vya Habari 31/03/2021
Vichwa vya Habari:
Saudi Arabia Yatumia kwa Uchache $1.5bilioni 'Kuuza Sura Yake kupitia Michezo'
Taliban Yaamini kuwa Tayari Wameshinda
Uzembe wa Sisi
Maelezo:
Saudi Arabia Yatumia kwa Uchache $1.5 bilioni 'Kuuza Sura Yake kupitia Michezo'
Saudi Arabia imetumia kwa uchache $ 1.5 bilioni kwa hafla za hali ya juu za michezo ya kimataifa kwa lengo la kuimarisha sura yake, ripoti mpya inafichua. Taifa hilo lenye utajiri wa mafuta limewekeza mamilioni katika ulimwengu wa michezo, ripoti ya shirika la haki za binadamu Grant Liberty inasema, kuanzia kwa mashindano ya chesi hadi gofu, tenisi na $ 60 milioni peke yake kwenye Kombe la Saudi, hafla ya kitajiri zaidi ya mbio za farasi na tuzo ya pesa ya $ 20 milioni. Ripoti hiyo, pia inaelezea mpango wa miaka kumi wa Ufalme huo wa $ 650 milioni pamoja na mbio za magari ya Formula One, ambayo mashindano yake ya kiulimwengu yanaanza Jumapili hii na kwa mara ya kwanza yatajumuisha mbio katika mji wa bandari wa Jeddah. Uchambuzi wa Grant Liberty unaelezea kiwango kikubwa cha uwekezaji wa Saudi Arabia katika kile wanachokiita "kuuza sura kupitia michezo," mazoezi ya kuwekeza au kuandaa hafla za michezo kwa nia ya kuficha rekodi mbaya ya haki za binadamu ya Ufalme huu, na kujipigia debe kama eneo jipya la kiulimwengu linaloongoza kwa utalii na tamasha.
Taliban Yaamini Tayari Wameshinda
Katika wiki ambayo naibu kiongozi wa Taliban, Sirajuddin Haqqani, alisema kuwa Taliban imemshinda adui Habari za Tolo za Afghanistan ziliripoti kwamba utawala wa Biden umewataka Taliban kukubali kuendelea kuwepo kwa Amerika nchini Afghanistan kwa miezi mitatu au sita baada ya Mei 1. Baada ya maoni ya Biden, Taliban walijibu na kuonya ikiwa wanajeshi wa Amerika watabaki nchini humo baada ya Mei 1 kwamba watalengwa. Tangu Mkataba wa Doha utiwe saini, Taliban imetimiza ahadi yake ya kutoyashambulia majeshi ya Amerika. Februari 8 iliashiria mwaka kamili wa kwanza kwamba hakuna vikosi vya Amerika vilivyo kufa katika vita nchini Afghanistan tangu vita vianze. Swali ni ikiwa Biden atachagua kukaa baada ya Mei 1 bila idhini ya Taliban, ambayo inaweza kumaanisha kuongezeka kwa vita vya karibu miaka 20. Kilicho hakika ni kwamba sio Amerika, bali Taliban ndio walio na nguvu katika mazungumzo yoyote.
Uzembe wa Sisi
Huku sehemu kubwa ya ulimwengu ikitazama matatizo yaliyosababishwa na kufungwa kwa Mkondo wa Suez kutokana na meli kubwa kukwama ardhini wakati dhoruba ya vumbi ilipokuwa ikifanyika. Jibu la serikali halikuonekana. Nchini Misri kwa masaa 26, hakukuwa na neno lolote kuhusu mkondo huo uliofungwa, usaidizi wa usafirishaji wa meli katika Bahari ya Mediterania na Bahari Nyekundu. Badala yake, Mamlaka ya Mkondo wa Suez (SCA) ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikitangaza kufanikiwa kwa safari ya meli ya Italia na kesi 65 za Covid-19 ndani yake. Kulikuwa na giza la vyombo vya habari. Na siku moja baadaye uongo ulianza, na taarifa rasmi ya kwanza ikataja kwamba juhudi "zinaendelea kufungua mkondo". SCA ilidharau athari kwa usafiri, ikituma "ujumbe wa uhakikisho kuwa usafiri utaendelea kama kawaida". Mamlaka hiyo iliwaonya waandishi wa habari kutozingatia habari yoyote au uvumi juu ya tukio baya zaidi la kufungwa kwa mkondo huo tangu Vita vya Waarabu na Israeli vya 1973. Siku ya Alhamisi, siku mbili baada ya machafuko kuanza, SCA ilitangaza rasmi kwamba usafiri umesimamishwa. Uzembe wa utawala wa Sisi tayari umeifanya Misri kuwa mahali pagumu kuishi, lakini sasa uzembe wake unatishia njia kuu ya maji ya kimataifa.