Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 07/04/2021

  • Vichwa vya Habari:
  • Ufaransa Yahitaji Kuweka Sawa Vipaumbele Vyake
  • Erdogan Aligeukia Jeshi Lake la Wana Maji
  • Mkate na Sarakasi Nchini Misri

Maelezo:

Ufaransa Yahitaji Kuweka Sawa Vipaumbele Vyake

Ufaransa ilipiga marufuku Niqab katika shule za umma mnamo 2004, sasa Bunge la Seneti la Ufaransa limepiga kura kupiga marufuku hijab kwa mtu yeyote chini ya umri wa miaka 18. Hatua hiyo ilipendekezwa mnamo Machi 30, 2021 ikiangukia chini ya Mswada wa Utengano uliopendekezwa. Kwa kuongezea, kina mama wanaovaa Hijab watakatazwa kuandamana na safari za shule za kujivinjari na burkini zitapigwa marufuku kwenye mabwawa ya kuogelea ya umma. Ufaransa kwa sasa inapambana na mfumo wa kisiasa ambao umevunjika, uchumi wake umetekwa nyara na utawala wa wachache (oligarchy) na nchi hiyo imeshuhudia kufeli kwa serikali yake kukabiliana na janga la Covid. Pamoja na matatizo haya yote Ufaransa inazingatia tu 3% ya idadi ya watu wake ambao wanaonekana kuwa ni tatizo kubwa kuliko maswala mengine yote ambayo taifa limegubikwa nayo.

Erdogan Aligeukia Jeshi Lake la Wanamaji

Mamlaka za Uturuki zimewaweka kizuizini maafisa wastaafu 10 wa jeshi la wanamaji waliotia saini, pamoja na wafanyikazi wengine wa zamani wa kijeshi wa ngazi ya juu, taarifa iliyoelezea wasiwasi wao juu ya vitendo ambavyo vinaweza kukiuka mkataba wa baharini wa miaka 85 uitwao Mkataba wa Montreux. Kukamatwa kwa wanamaji hao ni kitendo kipya katika ukandamizaji wa Erdogan wa wapinzani. Huku ikiwa haiwezekani kwamba Uturuki itajiondoa kwenye Mkataba wa Montreux, suala hilo limekuwa nukta mpya ya msuguano kati ya Erdogan na viongozi wa jeshi la Uturuki, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipingana.

Mkate na Sarakasi Nchini Misri

Huku utawala wake ukiwa katika machafuko, na mgororo mwingi wa hivi karibuni nchini Misri, serikali ya Sisi iliunda mkate wake na sarakasi yake wiki hii kupitia maandamano ya watawala wa zamani wa nchi hiyo kupitia mji mkuu, Cairo. Katika nchi ambayo vijana hawana kazi na umaskini uko zaidi ya 30% tamasha la kifahari, la mamilioni ya dolari la kutazama maiti 22 zilizo kaushwa (mummies) - wafalme 18 na malkia wanne - wakisafirishwa kutoka makavazi ya Misri, hadi mahali pao papya pa kupumzika penye umbali wa kilomita 5 kutoka makavazi hayo.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu