Alhamisi, 16 Rajab 1446 | 2025/01/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 18/04/2021

Vichwa vya habari:

Amerika Yaionya China Dhidi ya Vitendo vya Kichokozi katika Eneo Linalozozaniwa la Bahari ya Kusini mwa China

Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa India na Pakistan Wakutana Nchini Imarati

Hali ya Sintofahamu Yaenea Kufuatia Kujiondoa kwa Amerika katika Nchini Afghanistan

Maelezo:

Amerika Yaionya China Dhidi ya Vitendo  vya Kichokozi katika Eneo Linalozozaniwa la Bahari ya Kusini mwa China

Wiki iliyopita, Amerika iliionya China dhidi kile ambacho Ufilipino na Taiwan wanakiona kama vitendo endelevu vya kichokozi, ikiikimbusha Beijing majukumu yake kwa washirika wake. "shambulizi dhidi ya vikosi vya Ufilipino, meli au ndege za umma katika eneo la Pasifiki, ikiwemo bahari ya kusini mwa China, itachochea wajibu wetu chini ya Mkataba wa Pamoja wa Ulinzi wa Amerika na Ufilipino" Msemaji wa Wizara ya Kigeni Ned Price aliwaambia waandishi wa habari. "Tunashirikiana katika wasiwasi wa washirika wetu Ufilipino kuhusiana na kuendelea kuripotiwa kupotea kwa nyambizi ya kijeshi ya PRC  karibu na eneo la Whitsun Reef," Price alisema,  akiikusudia Jamhuri ya Watu ya China.  Zaidi ya boti 200 za Kichina zilionekana kwa mara ya kwanza mnamo tarehe 7 mwezi Machi katika eneo la  Whitsun Reef, takriban kilomita 320 (maili 200) magharibi mwa Kisiwa cha Palawan katika Bahari ya Kusini mwa China inayozozaniwa, japokuwa mengi tangu wakati huo yametawanyika katika Visiwa vya Spratly. China, inayodai umiliki wa wa bahari hiyo yenye utajiri mkubwa wa rasilimali, imekataa wiki nyingi za maombi ya Ufilipino ya kuondoa meli zake za kivita, ambazo Manila inasema zimeingia kinyume na sheria katika ukanda maalumu wa kiuchumi. Sauti ya Price "Imelenga zaidi" kuhusu shughuli za China, amesema: "Amerika inatumia kila juhudi kuhakikisha inazuia kila kitendo kitakacho hatarisha usalama au jamii au mfumo wa kiuchumi wa watu wa Taiwan." Alikuwa akitumia lugha kutoka katika Kifungu cha Sheria cha Mahusiano cha Taiwan, ambacho kwacho Amerika inalazimika kukipatia kisiwa hicho mbinu za kujihami dhidi ya Beijing. Raisi Joe Biden ameapa kuwapa ulinzi imara washirika wake na, katika nukta nadra ya muendelezo wa mtangulizi wake Donald Trump, ameunga mkono majibu makali dhidi ya uchokozi wa China. [chanzo: France24]

Amerika inaitia shinikizo China kwa pande zote. Amerika inaitumia India katika upande wa magharibi wa mpaka na China kuunda matatizo kwa Beijing, na inaitumia Japan, Ufilipino na Taiwan ili kuizuia China kujitanua katika eneo la Asia ya pasifiki na Bahari ya Atlantiki

Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa India na Pakistan Wakutana Nchini Imarati

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Nchi ya India na Pakistan watakutana Abu Dhabi siku ya Jumapili kwa mualiko wa serikali ya Imarati. Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Shah Mahmood Qureshi tayari ameshafika Imarati, wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa India Jaishankar akitarajiwa kufika siku ya Jumapili. Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ndiye atakaye simamia mazungumzo hayo kati yake na washirika wake kutoka India na Pakistan. “Katika mualiko wa pande hizo mbili, EAM Dkt S Jaishankar atatembelea Abu Dhabi mnamo tarehe 18/04/ 2021. Mazungumzo yake yataegemea zaidi katika ushrikiano wa kiuchumi na ustawi wa jamii,” Arindam Bagchi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya India, aliandika tweet mnamo siku ya Jumamosi. Haya yamejiri baada Yousef Al Otaiba, balozi wa Imarati nchini Amerika, kuthibitisha Jumatano iliyopita kwamba Imarati inasimamia mazungumzo kati ya India na Pakistan ili kuunda uhusiano imara kati ya majirani hao wawili ambao ni mahasimu. India na Pakistan zimenufaika na urafiki wao wa dhati na Imarati uliojengwa kwa miongo kadhaa ya mikataba ya kiuchumi na uhusiano wa mtu kwa mtu. Otaiba alisema kwamba ingawa India na Pakistan hazitakuwa “marafiki wa dhati”, Imarati ilitaka uhusiano wa pande mbili baina ya majirani hao ule ambao utawawezesha kila mmoja kuzungumza na mwenzake. “hatudhanii kama watakuwa... ‘Mataifa Yanayopendelewa Zaidi' baina yao kwa wao, lakini nadhani ni muhimu kwao kuwa na uhusiano imara wenye natija, ambalo ndilo lengo letu haswa,” Al Otaiba alisema. [Chanzo: Khaleej Times]

Imarati inataka kufanikisha mazungumzo baina India na Pakistan juu ya Kashmir. Huu ni mpango wa Amerika kuilazimisha Pakistan kutelekeza eneo lake la kimkakati ili kupata eneo la kiuchumi.

Hali ya Sintofahamu Yaenea Kufuatia Kujiondoa kwa Amerika katika Nchini Afghanistan

Masiku baada ya Raisi wa Joe Biden kutangaza maamuzi yake ya kujindoa kutoka Afghanistan na kumalizika kwa vita vya muda mrefu vya Amerika, wanamipango wa kijeshi, ingawa wamekuwa na wakati mgumu lakini bado wanafanya kazi kuona ni namna gani wanaweza kufanikisha. Mnamo siku ya Ijumaa, Idara ya Ulinzi ilitangaza kuhusu kubadilishana taarifa zinazohusu kuondoka kwa askari 2,500 hadi 3,500 kutoka Afghanistan, ilisema kwamba mpango mkakati tayari umeshaimarishwa na kile kinachoitwa maagizo ya kiutendaji yatafuata "hivi karibuni." Maafisa wameweka wazi uwezekano kwamba wanajeshi zaidi wanaweza kutumwa, katika kazi za muda mfupi, ili kuhakikisha uondokaji salama.  "Tutafahamu zaidi tukiwa karibu zaidi," katibu mkuu wa habari John Kirby aliwaambia waandishi siku ya Ijumaa, katika taarifa fupi kutoka Pentagon tangu tangazo lilipotoka. "Leo siwezi kuzungumzia kwa uhakika jambo hilo litaendaje," Kirby aliongeza. "Ni lazima kufahamu kwamba kutakuwa na uhitaji wa msaada. Unaweza kuongeza msaada wa wataalamu, mfano msaada wa wahandisi." Biden alitangaza Jumatano kwamba tutaanza kuondoa wanajeshi ifikapo Mei tarehe moja kutoka Afghanistan — tarehe ambayo kwa mujibu wa makabaliano yaliotiwa saini mwaka uliopita ilibidi zoezi hilo liwe limekwisha kati ya utwala wa Raisi Donald Trump na Taliban. Katika muda uliopangwa, vikosi vyote vya Amerika pamoja na wanajeshi 7000 wa NATO, wataondoka katika nchi hiyo mnamo Juni tarehe 11, ambapo ni kumbukumbu ya mwaka wa 20 ya mashambulizi ya Kituo cha Biashara cha Kiulimwengu jijini New York na Makao Makuu ya Jeshi Pentagon, ambayo yalipangwa katika ardhi ya Afghan.  Katika kauli iliotolewa Jumatano, Taliban walitaka kuondoka kwa vikosi vyote vya kigeni katika tarehe iliyopangwa mwaka uliopita katika makubaliano ya Doha. Msemaji Zabihullah Mujahid alienda mbali zaidi kwa kutishia kujiondoa katika makubaliano hayo, akisema katika mtandao wa Twitter, "Endapo makubaliano hayo yatavurugwa na vikosi vya kigeni kushindwa kuondoka katika nchi yetu katika tarehe iliyopangwa, kutakuwa na matatizo na wale watakaoshindwa kutii makubaliano hayo watabeba dhimmi hiyo." Siku ya Ijumaa Pentagon ilitambua hatari hiyo na kujibu kwa onyo la kivyake. [Chanzo: voanews]

Baada ya miaka 20 ya uvamizi, Amerika imeshindwa na wapiganaji dhaifu wa Taliban na kuamua kuondoka. Amerika ina mabilioni ya dolari na ina kichache mno cha kuonyesha katika uvamizi wa Afghanistan. Amerika imeshindwa kuitumia Afghanistan kama kambi yake dhidi ya ushawishi unaoongezeka wa Urusi na China. Kindani, Amerika haikuweza kuwarudisha nyuma Al Qaeda na sasa imekubali Taliban kurudi mamlakani baada ya kuwafurusha mwaka wa 2001.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu