Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Vichwa vya Habari 21/04/2021

Vichwa vya habari:

• Pakistan Yafikia Pabaya

• Jeshi la Wana Maji la Uturuki Ndilo Lenye Nguvu Zaidi katika Kanda Hiyo

Maelezo:

Pakistan Yafikia Pabaya

Nchini Pakistan hali imekuwa mbaya wiki hii baada ya TLP kuandamana mabarabarani baada ya utawala wa Imran Khan kuendelea kurefusha matakwa ya TLP ya kumfukuza balozi wa Ufaransa. Video inaendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii ikionyesha wanachama wa TLP wakiwa wamelowa damu baada ya makabiliano na polisi. Kura ya bunge ilikuwa mara nyingi ni kwa sababu ya tukio la tarehe 20 Aprili lakini serikali ya PTI bila kutarajiwa ilimkamakata kiongozi wa TLP - Saad Hussain Rizivi. Mgeuko huu wa serikali umepelekea TLP kuandamana mabarabarani na kupelekea na makabiliano kutokea jijini Lahore ambako ndiko yaliko makao makuu ya TLP. Serikali ya PTI kisha ikatangaza kuipiga marufuku TLP kama kundi la kigaidi jambo ambalo lilipelekea wafanyakazi wake kufanya maandamano na kufunga barabara. TLP iliundwa mwaka 2015 kufuatia mauaji ya gavana wa Punjab Salman Taseer juu ya sheria za kukufuru. Mbinu za TLP zimekuwa ni maandamano na kutoa matakwa kama vile kufurushwa kwa balozi wa Ufaransa kutokana na Ufaransa kuunga mkono vikaragosi vya Mtume (saw). Maagizo na mbinu hizo kali zimewashangaza wengi nchini Pakistan kwa kundi ambalo halijawahi kujihusisha na ghasia. Yote haya yamekuwa yakitendeka huku mtunga sheria wa PTI Amjad Ali Khan akiwasilisha mswada katika Bunge la Taifa ambao utalazimisha kwamba yeyote anayelikashifu atajikuta gerezani kwa miaka miwili, kando na fidia za Rupia 500,000 – au vyote kwa pamoja. Ni dhahiri kuwa matukio haya ni zaidi ya TLP na yenye kuelekeza upeo wa kadhia kubwa zaidi. Tangazo la hivi majuzi la mkuu wa jeshi Qamar Bajwa la kusawazisha mahusiano na India na kuachana na Kashmir inatarajiwa kuwa ndiyo kadhia halisi inayo endesha matukio haya ya hivi karibuni.

Jeshi la Wanamaji la Uturuki Ndilo Lenye Nguvu Zaidi katika Kanda Hiyo

Utafiti wa Chuo Kikuu cha Haifa umebaini kwamba nguvu ya jeshi la wanamaji la Uturuki ni wasiwasi unaoongezeka kwa ‘Israel’ na kuonyesha namna ambavyo Ankara imeboresha jeshi lake la majini kwa miaka michache iliyopita. Katika utafiti mmoja wa hivi karibuni, Kituo cha Sera ya Majini na Utafiti wa Kimkakati cha Chuo Kikuu cha Haifa cha Israel umetamatisha kwamba Jeshi la Wanamaji la Uturuki ndilo jeshi lenye nguvu zaidi katika kanda hiyo. Ripoti hiyo pia imeeleza kwamba ukuaji wa nguvu ya Jeshi la Wanamaji la Uturuki ni tishio kubwa na changamoto ya usoni kwa umbile la Kiyahudi. Utafiti huu wa Chuo Kikuu cha Haifa umeeleza kwamba nguvu ya majini ya Uturuki ni wasiwasi unaoongezeka kwa umbile la Kiyahudi na kuonyesha wazi namna Ankara ilivyoboresha jeshi hilo kwa miaka michache iliyopita. Pia utafiti huo umehitimisha kwamba hivi sasa jeshi la wanamaji la Uturuki ndilo lenye nguvu zaidi katika kanda hiyo.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu