Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Vichwa vya Habari 22/08/2021

Vichwa vya Habari:

Uturuki Yaisifu Sekta ya Ulinzi Inayonawiri katika Maonyesho ya Silaha ya Kimataifa

Afghanistan Yakabiliwa na Mtazamo Mzito wa Kifedha, Mkuu wa Zamani wa Benki Kuu Aonya

Udhalilishaji Mkubwa wa Sera ya Kigeni: Trump

Maelezo:

Uturuki Yaisifu Sekta ya Ulinzi Inayonawiri katika Maonyesho ya Silaha ya Kimataifa

Ndege ya aina ya TF inayotengenezwa na kampuni ya Kituruki ya Aerospace inasemekana kuwa kito cha taji la sekta ambayo inachukuliwa sana kuwa mojawapo ya sekta kuu za Uturuki. Ilijitokeza sana katika Maonyesho ya Sekta ya Ulinzi ya Kimataifa jijini Istanbul wiki hii. Ndege hiyo ya kivita, ambayo itachukua nafasi ya ndege kongwe aina ya F-4 na F-16 za Jeshi la Anga la Uturuki, inatarajiwa kuzinduliwa kwa umma mnamo 2023, miaka mia moja ya kuanzishwa kwa jamhuri ya Uturuki, na inatarajiwa kufanya kazi miaka miwili baadaye . "Mifumo yote ya makombora itatoka kwa kampuni za hapa hapa," alisema Zengin, akiashiria safu ya makombora yaliyotengenezwa na Roketsan na Tubitak chini ya mabawa ya ndege. "Lengo la mwisho ni kuwa na ndege ambayo imetengenezwa Uturuki kwa asilimia 100, ingawa mwanzoni itatumia injini ya F110," akaongeza, akimaanisha injini iliyoundwa ya GE Aviation iliyoundwa chini ya leseni nchini Uturuki. Kuanzishwa kwa TF - iliyojulikana hapo awali kama TF-X hadi kupita hatua ya majaribio - imepata uharaka zaidi baada ya Uturuki kuanza mradi wa ndege za kivita aina F-35 stealth fighter unaoongozwa na Amerika. Ankara iliondolewa kwenye mpango huo mnamo 2019 baada ya kupata mifumo ya ulinzi wa makombora ya S-400 ambayo Amerika ilidai ilitishia siri za F-35. Imeagiza ndege aina ya jet zaidi ya 100 na imewekeza kwa uchache $ 1.2 bilioni katika kuunda ndege hiyo ya kivita pamoja na washirika wengine wa Kimagharibi. Washington baadaye iliweka vikwazo vilivyoilenga sekta ya ulinzi ya Uturuki kutokana na ununuzi wa S-400, ingawa haya yanaonekana kutofanya chochote kutuliza mbio za Uturuki kutengeza silaha za kisasa. [Chanzo: Al Jazeera]

Uturuki inapenda kujinaki uwezo wake mpya kwa waangalizi wa kimataifa, lakini haitumii silaha kama hizo kuwalinda Wasyria kutokana na Assad, Wapalestina kutokana na ukatili wa serikali ya Kiyahudi au kuwalinda Wakashmiri kutokana na kunyongeshwa na watawala wa kiimla wa Kibaniani. Basi, kuna haja gani ya kuwa na silaha hizo?

Afghanistan Yakabiliwa na Mtazamo Mzito wa Kifedha, Mkuu wa Zamani wa Benki Kuu Aonya

Washington imezuia ufikiaji akiba katika benki za Amerika huku IMF ikizuia $ 460 milioni katika ufadhili wa majanga. Watu wa Afghanistan wanakabiliwa na makadirio "mabaya" ya kifedha, mkuu wa zamani wa benki kuu ameonya, akitahadharisha kuwa uhaba mkubwa wa dolari na mfumko mkubwa wa bei utachochea mtiririko wa wahamiaji kutoka nchini. Ajmal Ahmady, ambaye alitoroka Kabul mnamo Jumapili, aliiambia Financial Times kwamba Afghanistan ilikuwa ikitegemea usafirishaji mwingi wa akiba ya dolari kutoka Amerika na sasa kwa haraka inakumbwa na uhaba, na kusababisha uwezekano wa bei kubwa ya chakula na udhibiti wa mitaji. "Ikiwa watu wanafikiria, hali ni mbaya lakini imekwisha, nadhani wanadharau athari yake ... tumemaliza awamu ya kijeshi na sasa tutaanza awamu ya kiuchumi ya athari yake," Ahmady alisema katika mahojiano ya simu mnamo Jumatano. "hali itakuwa mbaya sana" pindi "watu hatakaposhindwa kupata fedha wanazohitaji kutoka kwa sekta ya benki", alionya. Uchumi wa Afghanistan una nakisi kubwa ya akaunti ya biashara na unategemea matumizi ya jeshi, misaada ya nje na ufikiaji wa karibu $ 9 bilioni za akiba ya sarafu. Vyanzo vyote hivyo vya fedha vimezimwa au vinakauka, Ahmady alisema, akiongeza kuwa viwango vya maisha sasa vitashuka "kwa kiasi kikubwa". Ikiwa unafikiria kuwa hali ya uwanja wa ndege sasa ni mbaya, nadhani kwa muda wa kipindi cha kati utaona mitiririko ya uhamiaji mkubwa kutoka Afghanistan na, kwa bahati mbaya, ikiwa Ulaya au nchi zingine zinafikiria kuwa zinaweza kuzuia hilo, hunawezi hata kidogo," alisema. Maoni ya Ahmady yamejiri huku uongozi wa Taliban ukikimbilia kutafuta jinsi ya kuiendesha Afghanistan baada ya viongozi wa wanamgambo wa kundi hilo la Waislam waliokuwa uhamishoni katika nchini ambayo ilikuwa imebadilika sana tangu ilipoondolewa madarakani miaka 20 iliyopita. Afghanistan ilikuwa na $ 9 bilioni katika akiba za kigeni wiki iliyopita, lakini nyingi ya hizi zinashikiliwa katika akaunti za kimataifa ambazo zimefungiwa, Ahmady alisema. Utawala wa Biden umezuia ufikiaji wa Taliban kwa akiba ya benki kuu ya Afghanistan iliyowekwa katika benki za Amerika, afisa mmoja wa Amerika aliiambia Financial Times. Baadhi ya wanachama wa Taliban wako kwenye orodha ya vikwazo vya Amerika. Mnamo siku ya Jumatano, IMF pia ilitangaza kuwa serikali ya Afghanistan haitapokea malipo ya awali ya haki maalum za kuchukua pesa, ambazo ni aina ya mali ya akiba sawa na pesa mpya. Nchi hiyo ilitarajiwa kupokea kiasi cha dolari milioni 460 mnamo Jumatatu kama sehemu ya mpango wa kiulimwengu wa mfuko huo ili kukabiliana na janga la virusi vya korona, lakini upinzani dhidi ya kuitambua serikali inayoongozwa na Taliban ulizuia mgao huo. "Hivi sasa kuna ukosefu wa uwazi ndani ya jamii ya kimataifa kuhusu kutambuliwa kwa serikali nchini Afghanistan, matokeo yake nchi hiyo haiwezi kupata SDRs au rasilimali zengine za IMF," msemaji mmoja wa IMF alisema. "Kama daima ilivyo kawaida, IMF inaongozwa na maoni ya jamii ya kimataifa." [Chanzo: Financial Times]

Amerika inazuia kimakusudi fedha kama njia ya kuishinikiza Taliban kufanya makubaliano katika suluhu ijayo ya kisiasa. Dili kubwa Itategemea jinsi Taliban itakavyo jibu. Hadi sasa, Taliban hawajaelezea maono kwa nchi hiyo au kuwasilisha katiba ya kina. Tangazo limefungwa tu kuifanya Afghanistan kuwa imarati ya Kiislamu bila ya maelezo zaidi kutolewa.

Udhalilishaji Mkubwa wa Sera ya Kigeni: Trump

Rais wa zamani wa Amerika Donald Trump mnamo Jumamosi alitoa shambulizi endelevu kwa jinsi Rais Joe Biden anavyoshughulikia kurudi nyuma kwa vikosi vya Amerika kutoka Afghanistan, ambapo aliuita "udhalilishaji mkubwa wa sera ya kigeni" katika historia ya nchi hiyo. Trump, mwana Republican ambaye ameondolea mbali uwezekano wa kugombea tena urais mnamo 2024, amemlaumu mara kwa mara Biden, Mwanademokrasia, kwa kuanduka kwa Afghanistan kwa wanamgambo wa Kiislamu Taliban, ingawa uondoaji wa Amerika uliochochea kuanguka huko ulijadiliwa na utawala wake mwenyewe. "Kuondoka kwa Biden kutoka Afghanistan ni mandhari ya kushangaza zaidi ya utepetevu mkubwa kwa kiongozi wa taifa, labda haujawahi kuonekapo wakati wowote," Trump alisema kwenye mkutano wenye ghasia uliojaa wafuasi wake karibu na Cullman, Alabama. Viongozi wa Taliban wanajaribu kuunda serikali mpya baada ya vikosi vyao kusambaa kote nchini huku vikosi vinavyoongozwa na Amerika vikijitoa baada ya miongo miwili, na serikali inayoungwa mkono na Magharibi na jeshi kuporomoka. Kwa upande wake, Biden amekosoa jeshi la Afghanistan kwa kukataa kupigana, aliishutumu serikali ambayo sasa imeng'olewa ya Afghanistan na kutangaza alirithi makubaliano mabaya ya kujiondoa kutoka kwa Trump. Katika mkutano huo, Trump alilaumu hali hiyo kwa Biden kutofuata mpango ambao utawala wake ulikuja nao na kulalamikia kuachwa nyuma kwa wafanyikazi na zana za Amerika wakati wanajeshi wakijiondoa. "Huku siko kujiondoa. Huku ni kujisalimisha kikamilifu," alisema. Trump alisema Taliban, ambayo alikuwa amezungumza nayo, ilimheshimu. Alipendekeza kuchukuliwa kwa haraka kwa Afghanistan hakungefanyika lau kama angekuwa bado yuko afisini. "Tungeweza kutoka kwa heshima," Trump aliongeza. "Tulipaswa kutoka kwa heshima. Na badala yake tulitoka na kinyume kabisa cha heshima." [Chanzo: Dawn]

Trump anaweza kumkosoa Biden vyovyote anavyotaka. Ukweli ni kwamba Amerika ilikuwa inaziba mapungufu yake nchini Afghanistan kwa muongo mmoja uliopita na kutoka kwa Amerika kulifichua mapungufu ya tawala mtawalia za Amerika. Karne ya Amerika imekwisha.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 25 Agosti 2021 09:38

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu