Jumapili, 29 Shawwal 1443 | 2022/05/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 07/11/2021

Vichwa vya Habari:

  • Cop26: Kongamano ni Hafla ya Uhusiano tu wa Umma
  • Amerika Yaruhusu Mauzo ya Makombora ya Anga-hadi-Anga kwa Saudi Arabia
  • Afisa wa Usalama wa Ngazi ya Juu wa Pakistan Akashifu Sera ya Magharibi ya Afghanistan kama Utelekezaji

Maelezo:

Cop26: Kongamano ni Hafla ya Uhusiano tu wa Umma

Greta Thunberg sasa ameondoka kwenye jukwaa baada ya ukosoaji mfupi lakini mkali wa Cop26. "Viongozi hawafanyi lolote, wanatengeneza mianya na kutengeneza mifumo ili kujinufaisha wao wenyewe na kuendelea kufaidika na mfumo huu angamivu," alisema. "Cop imegeuka kuwa tukio la Uhusiano wa Umma," aliongeza. [Chanzo: The Guardian]

Matamshi ya mwanaharakati huyo mchanga ni sahihi lakini hayaendi mbali vya kutosha. Isipokuwa chanzo cha nyuma ya mabadiliko ya hali ya hewa kishughulikiwe, kuchukua mkakati wa zero carbon hakuna uwezekano wa kuiokoa sayari hii. Kama ilivyo kwa masuala mengi ya kiulimwengu chanzo cha ongezeko la joto duniani ni Urasilimali. Urasilimali unaweka mkazo katika uzalishaji, ukuaji wa kielelezo na faida juu ya kila kitu chengine chochote. Kutokana na haya, uzingatiaji wa kuendelea juu ya ukuaji kwa gharama ya ugavi wa mali imeongeza ovyo gesi za greenhouse angani. Bila ya kuupiga marufuku milele Urasilimali, mabadiliko ya hali ya hewa kama vile umalizaji umaskini kabla yake kamwe hautafanya kazi.

Amerika Yaruhusu Mauzo ya Makombora ya Anga-hadi-Anga kwa Saudi Arabia

Wizara ya Mambo ya Nje ya Amerika iliidhinisha uuzaji wake wa kwanza wa silaha kwa Ufalme wa Saudi Arabia chini ya Rais wa Amerika Joe Biden kwa mauzo ya makombora 280 ya anga-hadi-anga yenye thamani ya hadi dolari milioni 650, Pentagon ilisema mnamo Alhamisi. Wakati Saudi Arabia ni mshirika muhimu katika Mashariki ya Kati, wabunge wa Amerika wameikosoa Riyadh kwa kuhusika katika vita vya Yemen, mzozo unaozingatiwa kuwa moja ya maafa mabaya zaidi ya kibinadamu duniani. Wamekataa kuidhinisha mauzo mengi ya kijeshi kwa ufalme huo bila hakikisho kuwa vifaa vya Amerika havitatumika kuua raia. Pentagon ililiarifu bunge la Congress kuhusu uuzaji huo siku ya Alhamisi. Iwapo utaidhinishwa, mkataba huo utakuwa wa kwanza kuiuzia Saudi Arabia tangu utawala wa Biden upitishe sera ya kuuza silaha za kujihami pekee kwa mshirika huyo wa Ghuba. Wizara ya Mambo ya Nje iliidhinisha mauzo hayo mnamo tarehe 26 Oktoba, msemaji mmoja alisema, akiongeza kuwa mauzo ya makombora ya anga-hadi-anga yanajiri baada ya "kuongezeka kwa mashambulizi ya mpakani dhidi ya Saudi Arabia katika mwaka uliopita." Baada ya uhusiano wa kirafiki wa utawala wa Trump na Riyadh, utawala wa Biden ulikagua upya mtazamo wake kwa Saudi Arabia, nchi ambayo ina wasiwasi mkubwa wa haki za binadamu lakini ambayo pia ni moja ya washirika wa karibu wa Amerika katika kukabiliana na tishio la Iran. Kifurushi hicho kitajumuisha makombora 280 AIM-120C-7/C-8 Advanced Medium Range Air-to-Air (AMRAAM), 596 LAU-128 Missile Rail Launchers (MRL) pamoja na makontena na vifaa vya kusaidia, vipuri, Serikali ya Amerika na uhandisi wa mkandarasi na msaada wa kiufundi. Licha ya kuidhinishwa na Wizara ya Kigeni, arifa hiyo haikuashiria kuwa mkataba umetiwa saini au kwamba mazungumzo yamekamilika. [Chanzo: Reuters]

Ni nini maana ya kununua silaha kutoka Amerika, wakati lengo lao kuu ni kuimarisha Ufalme huo dhidi ya nchi nyengine za Kiislamu?

Afisa wa Usalama wa Ngazi ya Juu wa Pakistan Akashifu Sera ya Magharibi ya Afghanistan kama Utelekezaji

Jumuiya ya kimataifa iko katika hatari ya kuchochea janga la kibinadamu nchini Afghanistan isipokuwa ishirikiane na serikali mpya ya Taliban na kuondoa vikwazo vya ufadhili na misaada jijini Kabul, Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Pakistan Moeed Yusuf alisema mnamo Alhamisi. Mataifa ya Magharibi yamekuwa yakisita kujihusisha na Taliban tangu kundi hilo lichukue udhibiti wa Afghanistan mwezi Agosti na yamepunguza usaidizi kwa taifa hilo linalotegemea misaada huku yakihatarisha uchumi wake kwa kuzuia ufikiaji hifadhi ya pesa zilizo nje ya nchi na kuweka hatua kali za kibiashara. Mataifa lazima "yajihusishe na uhalisia mpya wa kisiasa mara moja na kwa njia yenye manufaa", Bw Yusuf aliiambia Taasisi ya Mashariki ya Kati. "[Sababu] nambari moja ni kwa ajili ya msaada wa kibinadamu, kwa sababu kama hakuna msaada wa kibinadamu wakati majira ya baridi yanakaribia, ni nani atakayeteseka? Mwanamume na mwanamke wastani ambao sote tunadai kutaka kuwalinda,” alisema. Mtazamo wa sasa wa "ngoja-tuone" kutoka Magharibi, aliongeza, "ni sawa na kutelekezwa" ambapo inahatarisha kusababisha dhurufu zilezile za kuanguka kwa uchumi na uongozi uliochanika ambao uliiruhusu Taliban kupata umaarufu mwanzoni mwa miaka ya tisiini. Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa ya chakula hivi karibuni yalisema watu milioni 22.8 watakabiliwa na "uhaba mkubwa wa chakula" nchini Afghanistan mwezi Novemba, wakiwemo milioni 8.7 wanaoweza kukabiliwa na "kiwango cha dharura" cha uhaba wa chakula. Tayari, ripoti kutoka maeneo ya vijijini zinaonyesha baadhi ya watoto wachanga wana utapiamlo na hata kufa kwa njaa. Pakistan kwa muda mrefu imekuwa ikishirikiana na Taliban na ilikuwa moja ya mataifa matatu kulitambua kundi hilo walipotawala mara ya mwisho Afghanistan kuanzia 1996-2001. Mataifa ya Magharibi kwa miongo kadhaa yameishutumu Islamabad kwa kucheza mchezo wa pande mbili nchini Afghanistan kwa kutoa msaada wa kifedha na vifaa kwa Taliban huku pia ikikubali msaada wa kijeshi wa Amerika. Islamabad kwa muda mrefu imekanusha madai hayo. Bwana Yusuf alisema haikuwa kwa manufaa ya nchi yake kuwa na utawala wa Taliban pekee mjini Kabul na badala yake akatoa wito wa kuwepo kwa utawala "jumuishi" na "wa wastani". Alisema Pakistan italazimika kuwa na "wazimu" wa kutaka matokeo ambapo ina "jirani asiye na pesa za kuendesha nchi, hana uzoefu wa kweli wa kutawala na nimeachwa na mpaka wa maili 1,600 ambao kwa miongo minne umenigharimu mamilioni ya wakimbizi, tatizo la ugaidi, wakimbizi wa ndani na tangu tarehe 9/11, zaidi ya majeruhi 80,000." “[Wazo] kwamba hili ndilo ambalo Pakistan ingetarajia halina mantiki, haliingia akilini kabisa.” Nchi zote kuu, ikiwemo Amerika, zinahitaji kuhakikisha uthabiti wa Afghanistan au vyenginevyo makundi kama washirika wa ISIS wa nchi hiyo watapanua upeo wao na kuyashambulia mataifa mengine. [Chanzo: The National]

Amerika inataka Pakistan ikielekeza nguvu zake katika kuidhibiti China. Hata hivyo, Yusuf iokote vipande vyake nchini Afghanistan, huku Washington amekasirishwa kwamba Pakistan italazimika kulipia gharama ya kuifanya Afghanistan iolee na pia kulisha watu wake. Je, isingekuwa bora kwa Pakistan kuiunganisha rasmi Afghanistan, ili rasilimali za nchi zote mbili zitumike kujenga mustakabali mzuri zaidi?

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu