Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki Wa Habari za Kimataifa 04/12/2021

EU Yatangaza Ufadhili kwa Mpango wa Global Gateway ili Kupambana na Mpango wa China wa BRI

Wiki hii, Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen alitangaza ufadhili wa Euro bilioni 300 kwa mpango wa Global Gateway ambao ni jibu la EU kwa Mpango wa Ukanda na Barabara wa China. Rais wa EC alisema, “Tutaunga mkono uwekezaji mahiri katika miundombinu bora, kwa kuheshimu viwango vya juu zaidi vya kijamii na kimazingira, sambamba na maadili ya kidemokrasia ya EU na ada na viwango vya kimataifa. Mkakati wa Global Gateway ni kiolezo cha jinsi Ulaya inaweza kujenga mafungamano thabiti zaidi na ulimwengu. Mwaka huu Amerika pia ilitangaza mpango wa kimataifa wa miundombinu, unaoitwa Build Back Better World, lakini bado haijatoa maelezo kamili au ahadi za ufadhili. Mpango mkubwa wa Uchina wa BRI ulitangazwa mwaka 2013 kuwekeza hadi dolari trilioni 1 katika miundombinu katika karibu nchi 70 na mashirika ya kimataifa na tangu wakati huo umekuwa ukipanuka zaidi. Mpango wa EU ni mdogo na hauna matarajio makubwa. Kulingana na gazeti la The Economist, ‘Euro bilioni 300 kimsingi ni mchanganyiko wa ahadi zilizopo, udhamini wa mkopo na dhana za kishujaa kuhusu uwezo wa klabu “kukusanya” uwekezaji wa kibinafsi, badala ya matumizi mapya halisi.’

Magharibi inashindwa kupambana na uwezo mkubwa wa kiuchumi wa China. Kwa kutabanni mfumo wa kiuchumi wa Kirasilimali, Magharibi kihakika imeharibu uwezo wake wa kiuchumi. Urasilimali unapoanza kutabikishwa, huleta ukuaji mkubwa wa uchumi, kwani wajasiriamali na wafanyibiashara wanakombolewa kutoka kwa vikwazo dhidi ya uzalishaji mali. Lakini kwa kushindwa kugawanya mali ipasavyo, uchumi wa Kirasilimali hatimaye hufukarisha na kudhoofisha jamii yoyote unaotabikishwa ndani yake. Utajiri hujilimbikizia mikononi mwa matajiri na wenye uwezo, haswa huzunguka miongoni mwao tu, hivyo kutengeneza uchumi sambamba wa vyombo vya fedha bandia na bidhaa na huduma za anasa, huku umma kwa jumla ukinyimwa pakubwa mitaji na rasilimali zinazohitajika kwa ajili ya ujasiriamali na uzalishaji wa wenyeji. Iwapo jamii ya Magharibi itaendelea kuonekana kuwa na mafanikio zaidi kuliko sehemu zengine za dunia zilizosalia, hii ni kutokana na unyonyaji wa kibeberu wa Magharibi wa rasilimali na utajiri wa kimataifa, na si kwa sababu ya pato lao la kiuchumi la ndani. Kwa hakika, Amerika haijashtushwa na uzalishaji wa China, lakini inatafuta kuitumia kwa manufaa yake yenyewe, kama vile Amerika ilivyotaka kufaidika na uzalishaji wa kiuchumi wa Ujerumani na Japan huko nyuma. Iwapo Amerika inaiogopa China, si kwa sababu ya uchumi wake bali ni kwa sababu ya siasa zake na nguvu zake za kijeshi zinazokuwa kwa kasi, ambazo zinasimama kinyume na sera za pacifist zilizo lazimishwa kwa Ujerumani na Japan wakati wa uvamizi wa kimabavu wa Amerika baada ya Vita vya Pili vya Dunia.

Iwapo Waislamu wanatafuta mwamko wa halisi, basi hautatokana na kunakili mawazo na ada za Kimagharibi ambazo hatimaye zinashindwa zenyewe. Umma wa Kiislamu ndani yake una chemchemi bora zaidi ya mwongozo kwa ulimwengu huu, ambayo ni Qur’an Tukufu na Sunnah, na fikra, hukmu na nidhamu inazotoa ambazo iliufanya Uislamu kuwa hadhara inayotawala duniani kwa zaidi ya miaka elfu moja. Ikiwa tulipoteza hadhi hiyo hapo awali, haikuwa kwa sababu ya kutabanni kwetu Uislamu bali kwa sababu tulishindwa kushikamana nao ipasavyo. Hata hivyo, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Umma wa Kiislamu sasa unaregea kwenye Dini yake, na hivi karibuni utasimamisha tena Dola ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Mtume (saw) ambayo itaziunganisha nchi zote za Waislamu, na kuzikomboa ardhi zake zilizokaliwa kimabavu, kutabikisha Sharia ya Kiislamu, kuregesha mfumo wa maisha wa Kiislamu na kubeba ulinganizi wa Uislamu kwa ulimwengu mzima.

Ubeberu wa Kiuchumi wa Kimagharibi na Wanawake wa Kiafghani

Juhudi za nchi za Magharibi za kutafuta ubeberu wa kiuchumi pia zinashuhudiwa nchini Afghanistan. Ingawa Amerika ililazimika kuondoa jeshi lake kutoka Afghanistan kwa mujibu wa wasiwasi mkubwa wa kisiasa wa kijiografia, Magharibi inaendelea kujaribu kwa njia nyingine zote ziwezekanazo kuweka udhibiti juu ya ardhi hii. Watu wa Afghanistan wamekuwa wakipigana kwa miongo kadhaa, na wanajua jinsi ya kudumisha shughuli zao za kiuchumi bila msaada mdogo kutoka nje. Zaidi ya hayo, Afghanistan ina utajiri mkubwa wa rasilimali na inawakilisha njia panda muhimu ya umuhimu mkubwa wa kibiashara kati ya Asia Magharibi, Asia ya Kati na Asia ya Kusini. Hata hivyo, nchi za Magharibi zinaangazia masaibu ya wale walio katika miji hiyo ambao walitegemea kwa namna moja au nyingine ufadhili wa nchi za Magharibi wakati wa kukalia kimabavu, na wakati huo huo wakikata serikali ya Afghanistan kupata fedha za kigeni. Wiki hii, Umoja wa Mataifa ulitoa ripoti inayojaribu kuunganisha uchumi wa Afghanistan na ukosoaji mwingine unaopendwa wa Magharibi, ambao ni kuhusu jinsi wanawake wanavyotendewa. Kwa mujibu wa ripoti ya Bloomberg, "Hatua ya Taliban ya kuwazuia wanawake kufanya kazi inaweza mara moja kugharimu uchumi wa Afghanistan hadi $1bn, au 5% ya Pato la Taifa," Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) ulisema katika ripoti moja huku kundi hilo la wanamgambo likitafuta msaada wa kiulimwengu kusaidia kuepusha mzozo unaozidi kuongezeka." Ripoti hiyo inaendelea kusema, "Ripoti ya Umoja wa Mataifa ilitoa picha mbaya ya uchumi wa Afghanistan, unaokabiliwa na matatizo ya mfumko wa bei na uhaba wa fedha unaoendelea. Wanawake wanachangia 20% ya nguvu kazi ya nchi na kuwazuia kufanya kazi kunaweza kunyoa dolari nusu bilioni pekee kutoka kwa matumizi ya familia, ilisema.

Uislamu unaruhusu kikamilifu wanawake kufanya kazi na kujihusisha na shughuli za kiuchumi na kibiashara. Lakini hii sio kukuza 'GDP', ambayo ni kipimo kibaya, kilichoundwa kimakosa na potofu cha shughuli za kiuchumi za nchi. Uislamu hauhitaji kuziambatanisha juhudi na pesa ili kuzipa thamani. Kwa kuwasukuma wanawake kufanya kazi, nchi za Magharibi zimedhoofisha sana familia na nyumba, na hivyo kuzalisha utegemezi mkubwa wa kiuchumi na kijamii ambao huzilemea serikali za Kimagharibi ambazo haziwezi kutunza wote ipasavyo licha ya matumizi yao makubwa ya "kijamii" na elimu pana na huduma za afya. Katika Uislamu, serikali ndogo zaidi iliweza kufikia jamii yenye usawa na ustawi zaidi kupitia familia na jumuiya zenye nguvu, ambazo hazingeweza kuwepo bila ya dori zenye nguvu za wanawake katikati yao. Juhudi hizo zinapata kutambuliwa kikamilifu na heshima kamili katika jamii ya Kiislamu. Kwa mujibu wa riwaya moja,

جَاءَ إِلَى النَّبِيِّ ﷺ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ أَرَدْتُ أَنْ أَغْزُوَ وَقَدْ جِئْتُ أَسْتَشِيرُكَ. فَقَالَ: ‏«هَلْ لَكَ مِنْ أُمٍّ»‏. قَالَ: نَعَمْ. قَالَ: «فَالْزَمْهَا فَإِنَّ الْجَنَّةَ تَحْتَ رِجْلَيْهَا»

Mtu mmoja alikuja kwa Mtume (saw) akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nataka kwenda kupigana Jihad nimekuja kutaka ushauri wako.” Yeye (saw) akasema: “Je, unaye mama?” Akasema: “Ndio” Mtume (saw) akasema: “Basi kaa naye, kwani hakika Pepo iko chini ya miguu yake” [an-Nasai]

Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Afghanistan hivi karibuni itaimarishwa na kuungwa mkono kwa kuwa sehemu ya Dola ya Kiislamu ya Khilafah iliyosimamishwa tena ambayo itaingia kwenye safu za madola makubwa ya ulimwengu kwa sababu ya ukubwa wake, idadi ya watu, rasilimali, siasa za kieneo na mfumo wake, wenye uwezo wa kupinga ubeberu zaidi wa Kimagharibi juu ya ardhi za Waislamu, iwe kiuchumi au vyenginevyo.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu