Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari: 08/12/2021

 Vichwa vya Habari:

• Kura ya Maoni ya Harvard Yaonyesha Vijana wa Amerika Waiona Demokrasia ya Amerika kama Inayowafelisha

• Mkutano kati ya Biden na Putin

Maelezo:

Kura ya Maoni ya Harvard Yaonyesha Vijana wa Amerika Waiona Demokrasia ya Amerika kama Inayowafelisha

Wengi wa vijana wa Amerika wana wasiwasi kuhusu hali ya demokrasia nchini Amerika kulingana na kura mpya ya maoni ya Waamerika (umri wa miaka 18-29) iliyofanywa na Kitivo cha Harvard cha Kennedy. Asilimia 52 ya waliohojiwa waliamini kuwa demokrasia ya Amerika iko "matatizoni," kwa asilimia 39, au "imeshindwa," kwa asilimia 13. Sio tu kwamba vijana wana wasiwasi juu ya hali ya demokrasia, wengine pia wana wasiwasi juu ya vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe kuzuka nchini Amerika huku asilimia 35 wakiamini kwamba wataviona vita vya pili vya wenyewe kwa wenyewe katika maisha yao. "Tuna Waamerika wengi maradufu wachanga wanaoelezea hali ya demokrasia yetu kufeli ikilinganishwa na kuwa imara," Mkurugenzi wa Kura wa IOP John Della Volpe alisema. Mitindo hii inajiri wakati Rais wa Amerika Joe Biden akitazamiwa kufanya mkutano wa demokrasia wa mtandaoni wiki hii huku imani katika demokrasia ikishuka katika ulimwengu wa kimagharibi huku wengi wakigeukia vikundi vya kisiasa na watu binafsi wasio wa kawaida kwani wanahisi demokrasia haifanyi kazi kwao. Ukweli kwamba demokrasia inahitaji kongamano inaonyesha matatizo makubwa yanayoikabili.

Mkutano kati ya Biden na Putin

Rais Biden na Rais wa Urusi Vladimir Putin walifanya mkutano wa mtandaoni mnamo Jumanne, 7 Desemba. Mkutano wa mtandaoni ulidumu kwa zaidi ya masaa mawili huku taharuki ikiongezeka kuhusu Ukraine. Amerika imekuwa ikionya tangu Oktoba kwamba Urusi inapanga kuivamia Ukraine, huku Moscow ikikanusha vikali shtaka hilo na kuashiria kuwepo kwa Amerika na NATO katika eneo hilo kama chanzo cha taharuki. “[Rais Biden] alimwambia Rais Putin moja kwa moja kwamba endapo Urusi itaivamia zaidi Ukraine, Amerika na washirika wetu wa Ulaya watajibu kwa hatua kali za kiuchumi. Tutatoa nyenzo za ziada za kujihami kwa Waukraine zaidi ya zile tunazotoa tayari. Na tutaimarisha washirika wetu wa NATO upande wa mashariki kwa uwezo wa ziada,” Mshauri wa Usalama wa Kitaifa Jake Sullivan aliwaambia waandishi wa habari. Katika taarifa ya mkutano huo, Kremlin ilisema Putin aliomba dhamana kwamba muungano wa kijeshi hautasonga mashariki au kupeleka "mifumo ya kujihami ya silaha katika nchi zilizo karibu na Urusi." Alipoulizwa juu ya hamu ya Urusi ya dhamana kama hizo, Sullivan alisema Biden hakutoa "ahadi" wala "makubaliano" yanayohusiana na upanuzi wa NATO. Hakukuwa na mafanikio katika mazungumzo hayo na viongozi wote wawili walishikilia misimamo ambayo mwingine kamwe hataikubali.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu