- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Vichwa vya Habari: 25/05/2022
Vichwa vya Habari:
• Mkataba wa Majadiliano wa Marekani Kati ya Wasaudi, ‘Waisraeli’ na Wamisri
• Marekani Yatazamia Kuongeza Vikwazo juu ya Mafuta ya Urusi
• Biden Atangaza Kambi Mpya ya Kibiashara ya Pasifiki
Maelezo:
Mkataba wa Majadiliano wa Marekani Kati ya Wasaudi, ‘Waisraeli’ na Wamisri
Utawala wa Marekani umekuwa ukipatanisha kimya kimya kati ya Saudi Arabia, 'Israel' na Misri juu ya majadiliano ambayo, endapo yatafanikiwa, inaweza kuwa hatua ya kwanza kwenye barabara ya kusawazisha mahusiano kati ya Saudi Arabia na 'Israel'. Mpangilio huo unaweza kujenga kuaminiana kati ya pande hizo mbili na kutoa mwanya wa uhusiano wa dhati kati ya umbile la Kiyahudi na Saudi Arabia, ambazo haina uhusiano rasmi wa kidiplomasia. Mkataba huo unahusisha kukamilisha uhamisho wa visiwa viwili vya kimkakati katika Bahari Nyekundu kutoka Misri hadi mamlaka ya Saudi, duru za Marekani na 'Israel' ziliiambia Axios. Rais Biden anapanga kwenda Saudi Arabia kama sehemu ya safari ijayo ya Mashariki ya Kati. Endapo ziara hii itafanyika, itakuwa ya kwanza kwa Biden na Bin Salman. Safari hiyo pia itajumuisha mkutano wa kilele na viongozi wa Saudi Arabia, Imarati, Bahrain, Oman, Qatar, Kuwait, Misri, Jordan na Iraq - mataifa yote muhimu katika kusawazisha msimamo wa umbile la Kiyahudi katika Mashariki ya Kati.
Marekani Yatazamia Kuongeza Vikwazo juu ya Mafuta ya Urusi
Gazeti la New York Times limeripoti kuwa Marekani inatafuta njia zaidi za kuleta uharibifu kwa uchumi wa Urusi, utawala wa Biden unaripotiwa kufikiria kuwalenga wanunuzi wa mafuta ya Urusi. Maafisa wa Marekani wamesema wanatazamia kuumiza mauzo ya mafuta ya Urusi, lakini hawataki kupunguza bidhaa hiyo kutoka soko la kimataifa kwa ghafla mno kwani itasababisha kupanda kwa bei ya mafuta. Iwapo vitatekelezwa, vikwazo hivyo vya pili vinaweza kuilenga China na kuiweka Marekani kwenye mkondo wa mgongano na India, ambayo imeendeleza ununuzi wa mafuta ya Urusi licha ya shinikizo kutoka Washington. Kufikia sasa, Marekani, Uingereza, Canada, na Australia zote zimepiga marufuku uagizaji wa mafuta ya Urusi.
Biden Atangaza Kambi Mpya ya Kibiashara ya Pasifiki
Rais Joe Biden alitangaza wiki hii jijini Tokyo kwamba nchi 13 zimejiunga na mpango mpya wa kibiashara wa Asia na Pasifiki unaoongozwa na Marekani unaotajwa kuwa ni wa kupinga upanuzi mkali wa China katika eneo hilo. Tofauti na kambi za kawaida za kibiashara, hakuna mpango kwa wanachama wa Muundo wa Kiuchumi wa Indo-Pasifiki (IPEF) kujadiliana kuhusu ushuru na kurahisisha ufikiaji wa soko - ala ambayo imezidi kuwa mbaya kwa wapiga kura wa Marekani wanaohofia kuhujumu utengenezaji bidhaa wa bidhaa za nyumbani. Badala yake, mpango huo unatarajia kuunganisha washirika kupitia viwango vilivyokubaliwa katika maeneo makuu manne: uchumi wa kidijitali, misururu ya usambazaji, miundombinu ya nishati safi na hatua za kupambana na ufisadi.
IPEF inakusudiwa kuwapa washirika wa Marekani njia mbadala kwa ongezeko la uwepo wa kibiashara wa China kote Asia-Pasifiki.