- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Vichwa vya Habari 08/06/2022
Vichwa vya Habari:
Katiba Mpya ya Tunisia Kuondoa Maregeleo ya Uislamu
Pakistan Yahitaji $41 Bilioni katika Miezi 12 Ijayo
Imran Khan: Pakistan Huenda Ikasambaratika
Maelezo:
Katiba Mpya ya Tunisia Kuondoa Maregeleo ya Uislamu
Mtu aliyepewa jukumu la kuandika upya katiba ya Tunisia na Rais Kais Saied amesema kwamba atawasilisha rasimu iliyoondolewa maregeleo yoyote ya Uislamu, akisema ilikuwa ni kwa ajili ya kuzuia "itikadi kali" za kisiasa. Ibara ya kwanza ya katiba iliyopitishwa miaka mitatu baada ya mapinduzi ya 2011 nchini humo inasema ni "dola huria, huru na inayojitawala, Uislamu ni dini yake na Kiarabu ni lugha yake". Lakini Sadeq Belaid, mtaalam wa sheria aliyeteuliwa mwezi uliopita kuongoza kamati ya kuandaa rasimu ya katiba mpya, amesema: “Asilimia 80 ya Watunisia wanapinga itikadi kali na wanapinga matumizi ya dini kwa malengo ya kisiasa.” Belaid, 83, alisema anataka kukabiliana na vyama vyenye msukumo wa Uislamu kama vile Ennahda, ambayo ilikuwa na idadi kubwa ya viti katika bunge kabla ya kuvunjwa. "Ikiwa unatumia dini kujihusisha na siasa kali, hatutaruhusu hilo," alisema.
Pakistan Yahitaji $41 Bilioni katika Miezi 12 Ijayo
Waziri wa Fedha wa Pakistan Miftah Ismail amesema kuwa nchi hiyo inahitaji dolari bilioni 41 katika muda wa miezi 12 ijayo, vyenginevyo inakabiliwa na kufilisika. "Tunapaswa kulipa $21 bilioni katika mwaka ujao. Ninakisia kuwa kikomo cha nje cha nakisi ya sasa ya akaunti kitakuwa $ 12bilioni [...] Nadhani tunapaswa kuwa na akiba ya angalau miezi mitatu [...] Kwa hivyo tunahitaji $41 bilioni katika kipindi cha miezi 12 ijayo…” Akihutubia Kongamano la Biashara la Kabla ya Bajeti lililoandaliwa na serikali jijini Islamabad, waziri huyo alieleza matatizo yanayoukumba uchumi wa nchi. Alisema kuwa serikali ya Shehbaz Sharif imeshirikiana tena na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF). "Tulizungumza nao na tuna imani kubwa sana kwamba hivi karibuni tutakuwa na makubaliano na IMF. Tuna uhakika sana na hilo.” Baada ya kufuata mtindo wa kimagharibi au miongo kadhaa uchumi wa Pakistan unasalia katika hali mbaya. Huku kila serikali ikiilaumu serikali iliyopita, mwisho wao wanafuata mtindo ule ule wa kiuchumi wa kukopa, uuzaji bidhaa nje na kutafuta uwekezaji kutoka nje.
Imran Khan: Pakistan Huenda Ikagawanyika
Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan ameonya kwamba endapo utawala hautachukua uamuzi sahihi basi Pakistan ikagawanyika katika sehemu tatu. Katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni cha kibinafsi, waziri mkuu huyo wa zamani aliyeng’atuliwa madarakani kwa njia ya kura ya kutokuwa na imani naye mapema mwaka huu, alisema hali ya sasa ya kisiasa ni tatizo kwa nchi pamoja na utawala wake. “Endapo utawala hautafanya maamuzi sahihi basi nawahakikishia kwa maandishi kuwa wao na jeshi wataangamizwa kwa sababu nchi ikifilisika itakuwaje,” alisema. "Pakistan inaelekea katika hali ya kushindwa kulipa deni. Hilo likitokea basi ni taasisi gani itaathirika [vibaya] zaidi? Jeshi. Baada ya kuathirika, ni maridhiano gani yatakacyochukuliwa kutoka kwetu? Uondoaji wa nyuklia." Pia alikiri kwamba mamlaka yake kama waziri mkuu yamefungwa, akisema kwa kweli nyuzi zilivutwa na "watu fulani" walioshikilia hatamu za uongozi. Pia alikiri kwamba kupanda kwake madarakani kumekuwa kwa hali ya hatari tangu siku ya kwanza kwani alikosa idadi ya wengi. Imran Khan amekuwa akijenga simulizi kwamba Pakistan inamhitaji na kwamba bila yeye nchi hiyo itaangamia. Licha ya kuusambaratisha uchumi chini amepata huruma ya wananchi baada ya kuwaona watawala wakongwe walio na historia ya ufisadi wamerudi tena mamlakani.