Ijumaa, 10 Shawwal 1445 | 2024/04/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari: 20/07/2022

Vichwa vya Habari:

• Imran Khan Ashinda Mkoa wa Punjab

• Marekani Yaiondoa India kutoka kwa Vikwazo

Maelezo:

Imran Khan Ashinda Mkoa wa Punjab

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan ametangaza upya wito wake wa kufanyika kwa uchaguzi wa mapema baada ya msukosuko wa uchaguzi mdogo ulioshuhudia chama chake kikichukua udhibiti wa mkoa muhimu wa Pakistan - Punjab.

Uchaguzi huo mdogo uliitishwa baada ya wabunge kutoka Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) kubatilishwa kwa kubadili utiifu katika kura ya kumchagua Hamza mwanawe Bw Sharif kama waziri mkuu wa Punjab. Chama chake cha PTI kilishinda viti 15 kati ya 20 vya kunyakua huko Punjab, na kuwashinda wapinzani wao wakuu PML-N kwenye uwanja wao wa nyumbani. Matokeo hayo ni kionjo cha kile ambacho kinaweza kutokea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanywa kufikia Oktoba 2023, ambao Imran Khan anadai ufanyike mara moja. Matokeo ya Punjab ni pigo kubwa kwa Waziri Mkuu wa sasa Shehbaz Sharif, ambaye anaongoza PML-N. Hatima ya serikali yake ya muungano ambayo tayari ni dhaifu sasa inaning'inia kwenye uzi. Tangu Imran Khan aondolewe kwa kura ya kutokuwa na imani naye, ameongoza kampeni kali ambapo hata alikashifu uongozi wa kijeshi. Kwa kuishutumu familia ya Sharif kuwa sehemu ya njama za kigeni, uongozi wa kijeshi ulisukumwa nyuma huku Imran Khan akipata huruma ya watu na huku uchumi ukikaribia kuanguka (kulikoanza chini ya Imran Khan) viwango vyake vilifikia janga chini ya Shabaz Sharif. Kwa kushinda Punjab, serikali ya Shabaz Sharif inaning'inia kwenye uzi.

Marekani Yaiondoa India kutoka kwa Vikwazo

Wabunge wa Marekani wamepitisha msamaha ambao uliondoa vikwazo vyovyote dhidi ya India kwa ununuzi wa silaha za Urusi. Kukabiliana na wapinzani wa Amerika kupitia Sheria ya Vikwazo huadhibu mataifa ambayo yanashirikiana na wapinzani wa Amerika. Wabunge wanasema msamaha huo utaruhusu kuimarishwa kwa uhusiano kati ya Marekani na India. Huku vikwazo vikitekelezwa kwa Uturuki kwa ununuzi wa mfumo huo huo wa silaha - S400, kutoka Urusi, Uturuki iliwekwa kwenye orodha ya vikwazo na kufukuzwa kutoka kwa mipango mbalimbali ya ulinzi. Marekani imekuwa ikiichumbia India kwa miongo kadhaa. Tangu kugawanyika Marekani ilitaka India iwe mbele katika Vita Baridi, lakini watawala wa India walitetea kutoegemea upande wowote na kutochukua msimamo wowote katika Vita Baridi. India baadaye iliona uhusiano unaokua ukiimarika na Umoja wa Kisovieti, haswa katika uwanja wa ulinzi ambao uliendelea baada ya Muungano wa Kisovieti kuporomoka. Marekani iliipatia India silaha wakati wa vita vyake vya 1963 na China na kujaribu kukishawishi chama cha Congress cha India lakini haikufanikiwa kujishindia India. Mahusiano yalibadilika tu baada ya Muungano wa Kisovieti kuporomoka na kuibuka kwa BJP katika miaka ya tisiini. Marekani iliwachumbia hapo tu ndipo viongozi wa India walipoona manufaa ya kufanya kazi na Marekani ambayo inataka India iwe polisi katika eneo hilo na hii inalingana na matarajio ya India. Watawala vibaraka wa ulimwengu wa Kiislamu wanachukuliwa kama mahawara wanaonyanyaswa wanapofanya kazi na Marekani. Kwa upande wa India mahusiano ya Marekani na India sio yale ya taifa kibaraka, kwa hiyo inaichumbia kupitia kutoa maridhiano na mikataba ya kijeshi na kibiashara.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu