Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Vichwa vya Habari 22/07/2022

Vichwa vya Habari:

  • Chuki dhidi ya Uislamu: Waislamu Waelezea Unyanyasaji Waliopitia Kazini
  • Waafghani katika Sokomoko ya Uhamiaji Marekani Wawatazama Waukraine Wakipatwa kwa Shuari
  • Huku Rupia ya Pakistan Ikirekodi Kushuka Chini Zaidi, Waziri wa Fedha Alaumu Siasa

Maelezo:

Chuki dhidi ya Uislamu: Waislamu Waelezea Unyanyasaji Waliopitia Kazini

Shirika moja la kutoa misaada lenye makao yake makuu jijini London linalowasaidia Waislamu wanaokabiliwa na chuki dhidi ya Uislamu lasema watu wanahangaishwa na kunyanyaswa kazini kwa sababu ya dini yao. Kitengo cha Kukabiliana na Chuki dhidi ya Uislamu kinasema wateja huibiwa miswala yao na kushambuliwa kwa maneno na kimwili. Faiza Mukith, ambaye anafanya kazi katika shirika hilo la kutoa misaada, alisema wafanyikazi wenza wa mtu mmoja "walimvuta ndevu zake kwa nguvu". Pia walimwita kwa jina la "Jafar" - mpinzani mkuu katika filamu ya Disney Aladdin. Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo cha Kukabiliana na Chuki dhidi ya Uislamu Bi Mukith alisema mwanamke mmoja aliwekewa nyama ya nguruwe kwenye kisanduku chake cha chakula na wenzake alipokuja kufungua saumu alipokuwa akifanya kazi wakati wa Ramadhan. Katika miaka minne iliyopita shirika hilo la kutoa misaada lilisema limeshughulikia kesi 387 za ubaguzi. “Hapo mwanzo tuliona kesi nyingi za uhalifu wa chuki, unyanyasaji wa kijinsia, matusi, unyanyasaji mabarabarani, lakini sasa tunaona ubaguzi zaidi hasa katika maeneo ya kazi,” alisema. "Unaongezeka - haubadiliki." Hivi majuzi, uchunguzi wa Waislamu 1,503 wa Uingereza uliofanywa na Savanta ComRes kwa jukwaa la mtandaoni Hyphen ulipata 69% ya Waislamu wa Uingereza walioajiriwa kwa sasa walisema wamekumbana na aina fulani ya chuki dhidi ya Uislamu kazini. Tatizo hili haliko tu kwa London - wakati wa janga hilo, Polisi wa Midlands Magharibi walibaini zaidi ya matukio 9,000 ya chuki za ubaguzi wa rangi yaliripotiwa kwa jeshi hilo la polisi. [Chanzo: BBC].

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَتَّخِذُواْ بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لاَ يَأْلُونَكُمْ خَبَالاً وَدُّواْ مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاء مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الآيَاتِ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.” [3:118].

Waafghani katika Sokomoko ya Uhamiaji Marekani Wawatazama Waukraine Wakipatwa kwa Shuari

Kuna makumi ya maelfu ya Waafghani ambao wametuma maombi ya Viza Maalumu za Wahamiaji (SIV) ambao maombi yao yangali yanashughulikiwa karibu mwaka mmoja baada ya kushindwa kwa Marekani kujiondoa Afghanistan, afisa mkuu wa utawala alisema Jumatatu, akiongeza kuwa mchakato huo sasa utasimamiwa kikamilifu na Wizara ya Kigeni. Kulingana na afisa huyo, kufikia wiki iliyopita, kulikuwa na waombaji wakuu 74,274 katika utayarishaji wa SIV, visa iliyokusudiwa kwa wale waliofanya kazi kwa serikali ya Marekani wakati wa miongo miwili ya kuhusika katika vita nchini Afghanistan. Idadi hiyo inajumuisha wale ambao bado hawajapitisha awamu ya mkuu wa misheni (COM) ya maombi -- jambo muhimu katika iwapo visa itaidhinishwa au la -- na afisa mkuu wa utawala alisema kuwa 40-50% ya wale walio katika hatua ya kabla ya COM imekataliwa "kwa kutokuwa na nyaraka zinazofaa au kutostahiki kwa sababu mbalimbali." Kuna waombaji wakuu wapatao 10,000 ambao wana idhini ya mkuu wa misheni "na kimsingi wanajiandaa kupata hati zao ili kuweza kuhamishwa," afisa huyo alisema kwenye simu na wanahabari. Idadi hiyo haijumuishi karibu wanafamilia 40,000-50,000. Mpango wa SIV kwa raia wa Afghanistan umekuwa ukikumbwa na matatizo ya usimamizi na ukomo wa chini wa kila mwaka kwa miaka na kusababisha kujiondoa kwa majeshi ya Marekani. Mara nyingi ni mchakato mgumu na wa kina na unaweza kuchukua miaka kukamilika. Afisa huyo alisema utengezaji wa SIV unaendelea haraka kuliko hapo awali, akibainisha kuwa Wizara ya Kigeni imeongeza rasilimali kushughulikia utengezaji huo. Sasa, baada ya kuwatazama wakimbizi wa Kiukraine wakipata utengezwaji wa haraka - kwanza chini ya mpango jumla wa dhamana na baadaye chini ya ule ambao Amerika iliweka mahususi kwa Waukraine mnamo Aprili - Waafghani wengi wameelezea kuchanganyikiwa na kile wanachoona kama kutendewa kwa ubaguzi na mashirika ya uhamiaji ya Amerika, ambapo imeongeza mfadhaiko mkubwa wa kisaikolojia ambao wengi walikuwa tayari wanapitia wakati wanasubiri kuhamishwa. [Chanzo: CNN na Al Jazeera].

Sababu inayowafanya Waafghani kudhulumiwa na Marekani ni kwamba Waafghani hawako tena mstari wa mbele dhidi ya Urusi na sio Wazungu.

Huku Rupia ya Pakistan Ikirekodi Kushuka Chini Zaidi, Waziri wa Fedha Alaumu Siasa

Waziri wa fedha wa Pakistan amelaumu kudorora kwa rupia kutokana na msukosuko wa kisiasa, akisema anatarajia msukosuko wa soko kutokana na kushuka kwa kasi kwa sarafu hiyo kupungua hivi karibuni. "Kushuka kwa rupia hakutokani na misingi ya kiuchumi," Miftah Ismail aliambia shirika la habari la Reuters Jumatano. "Hofu hiyo kimsingi inatokana na machafuko ya kisiasa, ambayo yatapungua katika siku chache." Rupia ilishuka kwa asilimia 2 Jumatatu, na asilimia 3 Jumanne, licha ya makubaliano ya kiwango cha wafanyikazi ya wiki iliyopita na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ambayo yangefungua njia ya kutolewa kwa $ 1.17 bilioni chini ya malipo yaliyorejeshwa ya kifurushi cha uokoaji. Mnamo siku ya Jumatano asubuhi, rupia ilikuwa ikiuzwa kwa 225 kwa dolari, huku Jumanne ikimalizikia 221.99 baada ya Fitch Ratings kurekebisha mtazamo wake wa deni kuu la Pakistan kutoka kuwa thabiti hadi kuwa chini ya sifuri - ingawa ilithibitisha Ukadiriaji wa Muda Mrefu wa Fedha za Kigeni (LTFC) na Utoaji Kiwango Msingi (IDR) kwa “B-“. Sarafu za soko ibuka zinahisi joto huku Hifadhi ya Majimbo ya Amrika Shirikisho ikivutia mtaji kuelekea Marekani. Hofu katika soko la Asia Kusini pia inatokana na hatari zinazoongezeka baada ya ushindi wa waziri mkuu wa zamani Imran Khan katika uchaguzi mdogo ulioongeza wasiwasi juu ya mpango wa kuiokoa nchi hiyo na IMF, ambao unahitaji kuepusha kushindwa. "Kuna hofu sokoni, ninahofia [rupia] itashuka zaidi," Zafar Paracha, katibu mkuu wa Kampuni za Ubadilishanaji za Pakistan, chama cha kubadilisha fedha za kigeni, aliiambia Reuters mapema Jumatano. Paracha alisema haoni sababu yoyote ya kushuka kwa thamani ya Rupia zaidi ya uwezekano wa masharti ya IMF. Si serikali wala IMF iliyosema lolote kuhusu haja ya kushuka kwa thamani zaidi ya sarafu hiyo, ingawa Pakistan hivi karibuni ilipitisha kiwango cha ubadilishaji wa soko chini ya ushauri kutoka kwa mkopeshaji chini ya ajenda ya mageuzi ya kiuchumi. Waziri wa fedha alisema uagizaji wa bidhaa, ambao uliweka shinikizo kwa rupia, umepunguzwa na nakisi ya sasa ya akaunti imedhibitiwa katika siku 18 za kwanza za Juni. Shinikizo juu ya Rupia litapunguza kusonga mbele, alisema, akiongeza kuwa Pakistan tayari ilikuwa imetafuta vyanzo ili kukidhi mapungufu yake ya kifedha. [Chanzo: Al-Jazeera].

Kutochukua hatua kwa Benki Kuu ya Pakistan (SBP) kuunga mkono Rupia kunaashiria kushuka kwa thamani kwa amri ya IMF, kinyume na Rupia kuanguka kwa sababu ya mzozo wa kisiasa. Kwa mara nyingine tena IMF imedhihirisha kuwa imekamilisha udhibiti wa uchumi wa nchi hii.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu