Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Uhakiki wa Habari 01/10/2022

Magharibi Yalaani Uunganishaji wa Putin wa Majimbo Manne nchini Ukraine

Kwa mujibu wa Washington Post:

Rais wa Urusi Vladimir Putin alitia saini amri Ijumaa ya kuyaunganisha majimbo manne ya Ukraine. Katika sherehe kubwa jijini Kremlin, alisema Urusi itajumuisha rasmi majimbo ya Ukraine ya Donetsk, Luhansk, Kherson na Zaporizhzhia - na kwamba watu wanaoishi huko "watakuwa raia wetu milele."

Marekani na mataifa ya Magharibi yamelaani hatua hiyo na kusema ni ukiukaji wa wazi wa sheria ya kimataifa, huku utawala wa Biden ukitangaza awamu mpya ya vikwazo dhidi ya maafisa wa kijeshi na serikali ya Urusi, pamoja na mitandao ya ununuzi wa ulinzi nchini Urusi na Belarus.

Uvamizi wa Ukraine mwaka huu na Rais Vladimir Putin unathibitisha kuwa ni uamuzi wa kipumbavu zaidi wa miongo yake miwili pamoja na kuitawala Urusi. Putin alikuwa anajigamba tu, akionyesha nguvu ya Urusi maeneo ya Ukraine kwa manufaa ya kisiasa; lakini Amerika iliweza kucheza na hasira dhaifu ya Putin ili kumchokonoa kuingia katika uvamizi kamili wa ardhi ya Ukraine. Bila shaka, bila ya mipango na utekelezaji makini wa kijeshi, na uangalizi mkubwa wa kimkakati, misheni nzima imethibitisha kuwa janga. Kupiga hatua kwa mapema kwa Urusi kumegeuka kuwa ni kushindwa baada ya kushindwa. Sasa, katika kujaribu kuokoa kile anachoweza, Putin ametangaza kuyaunganisha majimbo manne ya Ukraine baada ya kura isiyoaminika iliyofanyika chini ya uvamizi wa kijeshi wa Urusi.

Wakati huo huo, baada ya kuunda hali hiyo nzima, mchochezi halisi wa uvamizi wa Urusi, Rais wa Marekani Joe Biden alichagua kujibu kwa ukali vitendo vya Putin. Kulingana na New York Times:

Saa chache baada ya Bw. Putin kutoa hotuba akisisitiza udhibiti wa Urusi juu ya majimbo hayo manne ya mashariki mwa Ukraine, Bw. Biden aliitaja hatua hiyo kuwa ni ukiukaji wa kidanganyifu wa sheria ya kimataifa ambao unaonyesha kudharau mataifa yenye amani kila mahali.

Marekani kamwe haitatambua hili, na kusema ukweli ulimwengu hautalitambua pia," Bw. Biden alisema kutoka Ikulu ya White House. "Hawezi kunyakua eneo la jirani yake na kisha kusalimika. Kwa ufupi hivyo ndivyo ilivyo.

Maregeleo ya Biden kwa kile kinachojulikana kama sheria ya kimataifa katika wakati huu ni ndiyo ya kinafiki zaidi. Amerika inakiuka sheria za kimataifa wakati wowote inapotaka kufanya hivyo, kama vile uvamizi wake mwingi wa nchi nyingine katika miongo ya hivi karibuni pamoja na mipango yake mingi ya kisiri ya ubadilishaji tawala katika nchi nyingi ambazo Marekani imefanya kazi ili kuziweka chini ya udhibiti wake wa kibeberu. Fauka ya hayo, ni uundaji wa sheria ya kimataifa wenyewe ndio unaobeba lawama kubwa kwa hili. Muundo wa serikali ya kitaifa wa Westphalia hutoa muundo wa kijiografia ulio mgumu kupita kiasi ambao huziacha nchi zenye nguvu pekee kuwa na chaguo la kupindua zile zenye uwezo mdogo. Kabla ya Westphalia, mipaka haikuwa thabiti na nchi zingeirekebisha kikawaida na mara kwa mara baina yazo kwa uharibifu na umwagaji damu mchache, kwa mujibu wa mabadiliko ya uwezo wao wa utawala. Si uunganisha wa ardhi unaopaswa kuharamishwa bali ni kuendelea kutawaliwa kibeberu kisiri na dola kubwa za Kimagharibi ambazo hunyonya mali na rasilimali za mabara makubwa bila ya kuwajibika kwa utawala wao.

Lakini kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt), Ummah wa Kiislamu hivi karibuni utainuka na kusimamisha tena Dola yake ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Mtume (saw) ambayo itakomboa ardhi zilizokaliwa kwa mabavu, kuunganisha ardhi za Waislamu, kutabikisha Sharia ya Kiislamu, kuregesha njia ya maisha ya Kiislamu na kubeba nuru ya Uislamu kwa ulimwengu mzima. Dola ya Khilafah, karibu tangu kusimamishwa kwake, itajiunga na safu za dola kubwa kwa sababu ya ukubwa wake, idadi kubwa ya watu, rasilimali nyingi, jiografia isiyo na kifani na mfumo wa kipekee wa Kiislamu. Dola ya Khilafah itafanya kazi ya kukabiliana, kudhibiti na kutuliza hila za dola kubwa za makafiri, na kuiregesha dunia kwenye amani na ustawi jumla uliokuwepo katika miaka elfu moja wakati Uislamu mara ya mwisho ulipotawala ulimwengu.

Chini ya Kukashifiwa na India, Marekani Inatetea Mauzo ya Silaha kwa Pakistan

Kwa mujibu wa Aljazeera:

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ametetea mauzo ya kijeshi ya Marekani kwa Pakistan huku kukiwa na kukashifiwa kutoka kwa India, ambayo inasema ndiyo mlengwa wa mkataba wa ndege za kivita aina ya F-16 wa $450m kati ya Washington na Islamabad.

Wakati wa mkutano mmoja wa waandishi wa habari katika mji mkuu wa Marekani mnamo Jumanne, Blinken alisema kuwa kifurushi cha kijeshi kilichoidhinishwa mapema mwezi huu kilikuwa kwa ajili ya ukarabati wa ndege zilizopo za Pakistan.

"Hizi sio ndege mpya, mifumo mipya, silaha mpya. Ni kudumisha kile walichonacho,” alisema Blinken, ambaye alizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa India Subrahmanyam Jaishankar.

"Mpango wa Pakistan unaimarisha uwezo wake wa kukabiliana na vitisho vya kigaidi vinavyotokea Pakistan au kutoka kanda hiyo. Sio kwa maslahi ya mtu yeyote kwamba vitisho hivyo vinaweza kuendelea bila kuadhibiwa," alisema.

Licha ya kulalamika kwa India, mpango wa silaha wa Marekani kwa kweli hauinufaishi Pakistan bali unaidhuru. Pakistan kwa muda mrefu imekuwa chini ya maslahi ya Marekani. Vifaa vya kijeshi vya Amerika, na vifungu vyake vya mkataba wa kina, huzifunga nchi zengine tu kwa nguvu zaidi kwa ajenda ya Amerika pekee. Upatikanaji unaoendelea wa kigeni wa vifaa vya kijeshi umezuia maendeleo ya viwanda vya kijeshi vya ndani ya Pakistan ingawa wanasayansi wa Pakistan wamethibitisha uwezo nchini Pakistan kuwa dola ya kinyuklia. Fauka ya hayo, Amerika hurekebisha kwa uangalifu ni kiasi gani na aina gani ya silaha itaipa Pakistan, ili kuunufaisha mkakati wa kieneo wa Marekani. Marekani mara kwa mara imeajiri Pakistan kama fimbo kuiweka India chini ya udhibiti wake; na Amerika imeelekeza mzozo wa kijeshi kwa Pakistan kwa namna ambayo italazimisha India pia kujiandaa kwa mzozo wa kijeshi kwa ukali na hivyo kuileta katika makabiliano na China.

Nchi za Kiislamu hivi leo, licha ya uhuru rasmi, zinaendelea kutawaliwa na tabaka la vibaraka wa kisiasa ambalo linaona kubakia hao kwao kuko katika utiifu wake endelevu kwa mabwana zake makafiri wa kibeberu wa Kimagharibi. Lakini kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt), Umma wa Kiislamu hivi karibuni utainuka na kuzipindua tawala hizi, na kuzibadilisha kwa uongozi wa ikhlasi, wa kiasili, wenye uwezo utakaotumikia ajenda ya Waislamu na Uislamu, na sio ile ya dola za kigeni za makafiri. Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika Qur’an Tukufu:

(لاَّ يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاء مِن دُوْنِ الْمُؤْمِنِينَ وَمَن يَفْعَلْ ذَلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللّهِ فِي شَيْءٍ إِلاَّ أَن تَتَّقُواْ مِنْهُمْ تُقَاةً وَيُحَذِّرُكُمُ اللّهُ نَفْسَهُ وَإِلَى اللّهِ الْمَصِيرُ)

“Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini. Na anaye fanya hivyo, basi hatakuwa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ila ikiwa kwa ajili ya kujilinda na shari zao. Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni naye. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.” [Aali Imran: 28].

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu