Alhamisi, 16 Rajab 1446 | 2025/01/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa Vya Habari 31/08/2022

Vichwa vya Habari:

Iran Imeipa Urusi Droni

Bodi ya IMF Yaachilia Zaidi ya Dolari Billioni 1.1 nchini Pakistan kama Fedha za Uokozi

Maelezo:

Iran Imeipa Urusi Droni

Ndege zisizo rubani za Iran (UAV) zenye uwezo wa kubeba silaha kwa ajili ya mashambulizi zimewasili nchini Urusi kwa ajili ya kuingia kwenye uwanja wa mapambano hivi karibuni. Aina za ndege hizo ni Shahed-129 na Shahed-191, pamoja na Mohajer-6. Kuwasili kwa ndege hizo kuna ongeza uwezo wa droni za Urusi, hii ni baada ya Urusi kuwa na droni chache za mashambulizi zinazoweza kushambulia maeneo yaliyolengwa ndani ya eneo la adui. Majaribio ya hivi karibuni ya droni hizo yameonyesha kufeli kwingi na imebaki kuonekana zitakuwa imara jinsi gani kwa Urusi. Ni miezi sita sasa tangu Urusi ianzishe mashambulizi dhidi ya Ukraine lakini bado haijaweza kupiga pigo kubwa kwa adui wakati ambapo vita hivyo havijageuka kuwa mzozo mpana.

Bodi ya IMF Yaachilia Zaidi ya Dolari Billioni 1.1 nchini Pakistan kama Fedha za Uokozi

Bodi ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) imepitisha uhakiki wa saba na wa nane wa mpango wa kuiokoa Pakistan, unaoruhusu kuachiliwa kwa zaidi ya Dolari billioni 1.1 kwenye uchumi unauokumbwa na ulitima wa fedha, hayo yalisemwa na IMF pamoja serikali ya Pakistan mnamo siku ya Jumatatu. Fedha hizo zitakuwa ni muokozi wa nchi hiyo ya kusini mwa Asia ambayo kwa sasa pia inakumbwa na mafuriko mabaya ambayo tayari yameshaua zaidi ya watu 1,100 na kuharibu mali zenye thamani ya dolari billioni 10 kwa mujibu wa waziri wa mipango wa nchi hiyo. Katika taarifa moja, Naibu Meneja Mkurugenzi wa IMF Antoinette Sayeh alisema kushikamana na ongezeko lililopangwa la ushuru wa mafuta na nishati ni "muhimu" huku uchumi wa Pakistan "ukisukwa sukwa na hali mbaya za nje". Huku watu wengi wa Pakistan wakiathirika kutokana na mafuriko mabaya, serikali ya Pakistan imekuwa ikienda mbio kuiomba IMF pesa. Ukweli kwamba hakuna pesa zozote za deni zilizotumika kuboresha miundombinu au katika maendeleo ya nchi inaibua swali kwamba ni kwa nini serikali mtawaliwa za Pakistan zinaendelea kutafuta mikopo hiyo.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu