Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari: 12/10/2022

Vichwa vya Habari:

• Urusi Yaanzisha Mashambulizi ya Makombora Kote Nchini Ukraine

• Belarus Yafungua Mpaka dhidi ya Ukraine

• Lebanon-‘Israel’ Zatia Saini Mkataba wa Mpaka

Maelezo:

Urusi Yaanzisha Mashambulizi ya Makombora Kote Nchini Ukraine

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza kwamba vikosi vya Urusi vilikuwa vimefanya mashambulizi makubwa ya silaha za masafa marefu, zenye usahihi wa hali ya juu zikilenga vituo vya kawi, maamuzi na mawasiliano vya Ukraine, mnamo Oktoba 10, baada ya kukumbwa na vizingiti vingi katika vita hivyo vya miezi minane. Mashambulizi hayo yamekuwa na athari ya mshtuko na mshangao lakini yamebadilika kidogo tu kwenye uwanja wa vita. Mashambulizi hayo bila shaka yatasaidia kuwafanya wachambuzi wapambe wa mrengo wa kulia wa Urusi wanaotoa wito wa kukoleza mashambulizi dhidi Ukraine. Urusi haikutumia kampeni kubwa kama hiyo ya ulipuaji mabomu ilipovamia zaidi ya miezi 8 iliyopita na tangu wakati huo inakabiliwa na changamoto nyingi sana nchini Ukraine.

Belarus Yafungua Mpaka dhidi ya Ukraine

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amesema amekubali kupeleka kikosi cha pamoja cha majeshi ya Urusi na Belarus kwenye mpaka wa Ukraine kujibu madai ya vitisho kutoka kwa Ukraine. Kikosi hicho cha pamoja huenda kikatumwa kando ya mpaka wa Belarus na Ukraine, na kulazimisha Ukraine kupeleka sehemu kubwa ya akiba yake kuelekea Belarus badala ya katika mpaka wa kusini mwa Ukraine. Ubadilishaji huu wa rasilimali za Ukraine huenda ukasaidia majeshi ya Urusi kukamata mpango huo eneo la kusini. Putin hivi majuzi alikubali mikopo ya dolari bilioni 1.5 ya kubadilisha uagizaji hadi Belarus, ambayo ingeonyesha ufadhili huo ulitokana na Belarus kujiunga na juhudi za vita za Urusi.

Lebanon-‘Israel’ Zatia Saini Mkataba wa Mpaka

Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi Yair Lapid na Rais wa Lebanon Michel Aoun walisema kuwa nchi zao zilifikia makubaliano ya baharini yaliyosimamiwa na Amerika baada ya mazungumzo ya dakika za mwisho ili kukidhi wasiwasi wa Lebanon. Chini ya makubaliano hayo, uwanja wa gesi asilia wa Karish kuna uwezekano mkubwa wa kwenda kwa 'Israel' na uwanja wa gesi asilia wa Qana kwenda kwa Lebanon, huku kukiwa na marekebisho madogo kwenye mpaka wa baharini na baadhi ya fidia kwa umbile la Kiyahudi kwa sababu uwanja wa gesi wa Qana nusu bado utakuwa katika Maji ya ‘Israel’. Hezbollah imeripotiwa kukubali makubaliano hayo, lakini serikali za umbile la Kiyahudi na Lebanon bado lazima ziyakubali rasmi. Ugunduzi wa viwanja vya gesi katika bahari yao yenye mzozo katika miaka ya 2000 uliongeza maslahi ya umbile la Kiyahudi na Lebanon katika kuweka mpaka wa mwisho wa baharini ili uchunguzi wa kawi ufanyike.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu