Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 18/01/2023

Vichwa vya Habari:

Saudi Arabia Yafungua Biashara ya Sarafu kando na Dolari ya Marekani

Marekani Yafungua Kambi nchini Morocco

Idadi ya Watu wa China Yapungua

Maelezo:

Saudi Arabia Yafungua Biashara ya Sarafu kando na Dolari ya Marekani

Saudi Arabia itazingatia kufanya biashara kwa sarafu nyengine kando dolari ya Marekani, waziri wa fedha wa nchi hiyo amesema. "Hakuna masuala ya kujadili jinsi tunavyotatua mipango yetu ya biashara, iwe ni kwa dolari ya Marekani, iwe ni euro, iwe ni riyal ya Saudi," waziri wa fedha wa Ufalme huo, Mohammed al-Jadaan, aliiambia Bloomberg TV katika mahojiano huko Davos, Uswisi. Wakati wa ziara yake katika Ghuba mwezi Disemba, Rais Xi Jinping wa China aliwaambia viongozi wa nchi za Kiarabu kwamba Beijing itashinikiza kununua mafuta na gesi kwa Yuan, kwa kuwa inatazamia kuweka nafasi ya sarafu yake kwa matumizi ya biashara ya kimataifa. Uuzaji wa mafuta kote ulimwenguni unauzwa kwa dolari za Kimarekani. China inachangia zaidi ya mahuruji ya mafuta ghafi ya Saudi Arabia. Iwapo ufalme huo utaelekea kwenye "petroyuan", inaweza kudhoofisha hadhi ya dolari kama sarafu ya akiba ya dunia. "Tunafurahia uhusiano wa kimkakati na China na tunafurahia uhusiano huo wa kimkakati na mataifa mengine ikiwemo Marekani na tunataka kuendeleza hilo na Ulaya na nchi nyingine ambazo ziko tayari na zina uwezo wa kufanya kazi nasi," Jadaan alisema. Urusi pamoja na Uchina zimejaribu kama dola za kisasa kufikia mataifa mengine ili kubadilisha mpangilio wa kiulimwengu, kwa kugeukia Uturuki na sasa Saudi Arabia, hawatambui kuwa mataifa yote mawili yana uhusiano wa kina na wa karibu na Amerika na kuna uwezekano wa kuchukua hatua kama farasi wa trojan katika chochote ambacho Urusi na China zitaasisi.

Marekani Yafungua Kambi nchini Morocco

Rais wa Marekani Joe Biden amemuagiza Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin kuandaa mpango wa dharura wa kuanzisha kituo cha kijeshi cha Marekani katika Ufalme wa Morocco, gazeti la New York Daily News limeripoti. Biden amemwambia Austin kuishinikiza Pentagon kuwepesisha masuala ya vifaa na sheria ya uwekezaji wa sekta ya ulinzi ya Marekani nchini Morocco. Kuimarishwa kwa dori kuu ya Rabat katika kupambana na ugaidi, pamoja uoanishwaji wake katika mlingano wa kijeshi wa kimataifa, utapatikana kwa kukuza uwezo wake wa kiufundi wa kijeshi, unakusudiwa. Morocco inawakilisha chaguo hatari kwa kambi ya kijeshi ya Marekani. Huko Afrika Kaskazini Marekani imefanya kazi pamoja na Uturuki na Urusi nchini Libya ili kufikia maslahi yake na kuwa mbali na Aegean na Bahari Nyeusi kutafanya kambi hii kuwa na faida ndogo dhidi ya Urusi.

Idadi ya Watu wa China Yapungua

Mamlaka za China zilichapisha takwimu wiki hii ambazo zilithibitisha kwamba idadi ya watu nchini humo ilipungua kwa mara ya kwanza tangu rekodi zilipoanza mwaka 1953. Taifa hilo lenye watu wengi zaidi duniani liliona idadi ya watu ikipungua kwa watu 850,000 huku kiwango chake cha ubadilishaji kikipungua hadi watoto 1.15 kwa kila mwanamke, kiwango cha chini zaidi ya kiwango cha ubadilishaji cha watoto 2.1 kwa kila mwanamke kinachohitajika kwa idadi ya watu stahiki.

Nguvu Kazi kubwa ya China iliipa usambazaji usio kwisha wa wafanyikazi na hii ikawa uti wa mgongo wa ukuaji wake wa uchumi kwa miongo kadhaa. Ijapokuwa China imekuwa ikitazamia kuachana na utengenezaji wa bei nafuu na wa hali ya chini hadi uundaji wa hali ya juu na wa bei ya juu ambao utategemea zaidi teknolojia badala ya wafanyikazi, China inahitaji idadi kubwa ya watu kutumia sehemu kubwa ya kile itakachozalisha. Huku idadi ya watu wa China sasa ikipungua, hii itamaanisha kuwa wateja wake pia watapungua na hii pengine italeta changamoto kubwa zaidi kwa Chama cha Kikomunisti cha China.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu