Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki wa Habari 15/02/2023

Pakistani Yajizatiti kwenye Mikopo ya IMF

Waziri wa Fedha wa Pakistan Ishaq Dar alisema Islamabad imekubali matakwa ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) kuhusu mageuzi ya kiuchumi baada ya ziara ya siku 10 ya mfuko huo nchini Pakistan. Mageuzi haya yataileta Pakistan karibu na kufungua fedha kutoka kwa mpango wa uokozi wa IMF, ambao Pakistan inauhitaji ili kusaidia akiba yake ya fedha za kigeni iliyopungua na kuepuka kushindwa kulipa. Lakini utekelezwaji wa hatua mbalimbali za kubana matumizi, ambazo serikali inatarajiwa kutunga huku kukiwa na mzozo wa kiuchumi unaoendelea kunahatarisha kuenea kwa machafuko ya kijamii dhidi ya serikali. Mnamo Februari 14 Islamabad iliongeza ushuru wa gesi asilia kwa 16% -112% kwa watumiaji wa nyumbani na wa viwandani kama sehemu ya juhudi zake za kufufua uokoaji wa dolari bilioni 6 kutoka kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF). Islamabad pia inatarajiwa kutangaza ongezeko mithili hilo la bei ya umeme katika siku zijazo. Waziri wa Fedha wa Pakistan Ishaq Dar alisema Islamabad imekubali matakwa ya IMF ya mageuzi ya kiuchumi licha ya kushindwa kukamilisha makubaliano ya uokoaji mpya wakati wa ziara ya maafisa wa IMF. Pakistan sasa iko kwenye kifurushi chake cha 23 cha IMF, cha kwanza kilikuwa mwaka 1958, baada ya kutegemea mikopo ya IMF kwa miongo kadhaa, ni mambo yaliyoimarika nchini humo ni kidogo.

Waziri wa Masuala ya Ndani wa Taliban Akashifu Uongozi

Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Taliban ya Afghanistan Sirajuddin Haqqani alitoa ukosoaji uliofichika mnamo Februari 11 dhidi ya uongozi wa Taliban, akielezea hali ya nchi hiyo kuwa isiyovumilika na kukosoa harakati hiyo kwa kutobadilika na kuwatenganisha wananchi. Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid alijibu mnamo Februari 12 kwa kusema kwamba ukosoaji wa wale walio mamlakani unapaswa kutolewa kwa faragha na sio kudhalilisha utu wa mtu. Maoni ya Haqqani yanawakilisha ukosoaji wa hali ya juu zaidi wa umma kutoka ndani ya Taliban wa utawala wa kundi hilo tangu ilipochukua mamlaka ya Afghanistan mwezi Agosti 2021. Maoni ya Haqqani na majibu ya Mujahid yanasisitiza kuendelea kwa mfarakano ndani ya vuguvugu la Taliban huku kukiwa na kutoelewana juu ya utawala na sera ambako kumeendelea kwa kipindi cha mwaka na nusu uliopita. Ripoti pia zinathibitisha kutoelewana ndani ya uongozi wa kundi hilo kumekuwa mbaya zaidi baada ya serikali kutoa maagizo ya kuwapiga marufuku wanawake katika vyuo vikuu. Haqqani aliripoti kuwa "Hali ya sasa haivumiliki. Ikiwa hali ya umma itakuwa mbaya zaidi na isiyo na utulivu, ni jukumu letu kuwaleta karibu nasi." Haqqani pia alibainisha umuhimu wa mahusiano ya kimataifa ya Taliban, akisema, "Tunataka maingiliano na jumuiya ya dunia kwa ajili ya watu wetu, tunataka wepesi kwa ajili ya watu, tunataka kuponya majeraha ya watu." Taliban walishinda kwenye uwanja wa vita lakini wamejitahidi kufanya mabadiliko kutoka kwa vuguvugu la upinzani hadi kutawala Afghanistan. Migawanyiko inazidi kuongezeka huku baadhi ya wanachama wa vuguvugu hilo wakitaka kupata uhalali wa kimataifa, ilhali wengine wanahisi kuwa kundi hilo linalegeza msimamo sana.

Siasa za Maputo

Jeshi la Marekani lilidungua vyombo vitatu visivyojulikana vyenye kuruka juu ya Amerika Kaskazini tangu Februari 10, tangu puto la kijasusi la China kutambuliwa katika bara la Amerika. Mkuu wa Kamandi ya Ulinzi wa Anga ya Amerika Kaskazini (NORAD) alisema ni mapema mno kuviainisha vyombo hivyo, huku Kiongozi wa Wengi katika Seneti ya Marekani Chuck Schumer akisema Mshauri wa Usalama wa Taifa Jake Sullivan aliyaita maputo ya UFO. Matukio hayo yanaonyesha kuwa Marekani inaongeza unyeti wa uchujaji wao wa data ya anga ili kuashiria vyombo vidogo zaidi vyenye umbo la maputo katika anga ya Amerika Kaskazini. Matukio hayo pia yanafichua kuwa Marekani imebadilisha baadhi ya vigezo vyake kuhusu kitambulisho cha UFO na sheria za ushiriki, ikimaanisha kuwa matukio ya mbeleni yanawezekana. Iwapo mojawapo ya UFO tatu itaamuliwa kuwa ya Kichina - mithili ya puto lililodunguliwa mnamo Februari 4 - itatatiza zaidi uhusiano wa Amerika na China na kutoa mwanga juu ya jinsi gani mpango wa China wa puto ni mchangamfu na mpana zaidi juu ya Amerika Kaskazini. Ikiwa hii ndiyo njia ya China ya kujibu chokochoko za Marekani juu ya Taiwan na upanuzi wake katika Bahari ya China Kusini, basi Wachina wanafikia athari za matamanio yao.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu