Jumamosi, 09 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki wa Habari 22/02/2023

Bunge la Kitaifa la Pakistan Lapitisha Mswada wa Nyongeza ya Fedha

Bunge la Kitaifa la Pakistan lilipitisha Mswada wa Nyongeza ya Fedha uliowasilishwa mnamo Februari 15, ambao utatekeleza ushuru wa juu. Mswada huo unapendekeza ongezeko la ushuru wa mauzo kutoka 17% hadi 18%, ushuru wa uagizaji bidhaa za anasa kutoka 17% hadi 25% na nauli za juu za usafiri wa anga. Kuidhinishwa kwa ushuru wa juu kutaileta Pakistan karibu na kuanza tena kwa mpango wa uokoaji wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa. Kupanda kwa ushuru - pamoja na kupanda kwa bei ya mafuta na gesi hivi karibuni - kutausukuma mfumko wa bei kuwa juu zaidi na kuongeza hatari ya maandamano na machafuko ya kijamii katika miezi ijayo huku kukiwa na hali tete ya kisiasa. Pakistan inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi kutokana na kupungua kwa akiba yake ya fedha za kigeni na kutokuwa na uwezo wa kufadhili uagizaji bidhaa muhimu kutoka nje na kulipa madeni ya nyuma. Kupandishwa kwa bei huku kunasaidia kidogo mno kutatua matatizo ya nchi.

Urusi Yasimamisha Ushiriki katika MWANZO Mpya

Katika hotuba yake kwa Bunge la Federali, Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema nchi yake itasitisha ushiriki wake katika Mkataba wa MWANZO Mpya wa kudhibiti silaha za nyuklia. Putin alikariri kuwa Urusi haijajiondoa kabisa katika mkataba huo na iko tayari kwa makubaliano mapya ambayo yanazingatia silaha za nyuklia za Ufaransa na Uingereza. Urusi inaishinikiza Washington kuingia katika mazungumzo mapana ya usalama juu ya udhibiti wa silaha, pamoja na matakwa yake ya hapo awali ya mazungumzo juu ya msaada wa Magharibi kwa Ukraine. Inaonekana hakuna uwezekano kwamba Urusi itakiuka mkataba huo waziwazi au kushiriki katika mashindano ya kisilaha na Marekani, ambayo yatakuwa ghali na kutoa manufaa kidogo kwa Moscow. Urusi inatumai kuwa vitendo kama hivyo vitachochea uchovu wa kivita katika nchi za Magharibi. Mnamo Januari 31, Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani ilitambua Urusi kama "isiyofuata" Mkataba wa MWANZO Mpya kwa sababu ya kukataa kuregelea tena mazungumzo ya ukaguzi wa nchi hizo mbili. Huko nyuma mnamo Novemba 2022, Moscow ilighairi mazungumzo nchini Misri, juu ya kuanza tena ukaguzi wa MWANZO Mpya, huku Naibu Waziri wa Mambo ya nje Sergey Ryabko akisema Urusi iliachwa ikiwa “haina chaguo jengine” kwa sababu Washington haitaki kujadili “hali nchini Ukraine.”

Iran ina Urutubishaji wa 84% wa Uranium

Wakaguzi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki wamegundua urutubishaji wa 84% wa uranium wakati wa ukaguzi katika wiki ya Februari 13 nchini Iran. Kwa urutubishaji wa 84% wa uranium - lakini bila ya kuhifadhi uranium iliyorutubishwa zaidi - Iran inaonekana kuwa inajaribu kuingiza uzi kwenye sindano kati ya upinzani na kufuata sheria ili kulazimisha Marekani na EU kuanzisha tena mazungumzo ya nyuklia. Kiwango cha juu cha urutubishaji wa uranium kinakaribia kiwango cha 90% kinachojulikana kama daraja la silaha, na maendeleo yake yatachochea mjadala zaidi katika umbile la Kiyahudi na Magharibi juu ya jinsi ya kujibu, kwa uwezekano zaidi wa operesheni za kisiri za kijeshi na kijasusi na ‘Israel’. Iran imekuwa ikiangazia uharakishaji wa mipango yake ya nyuklia na makombora katika miezi ya hivi karibuni huku nchi za Magharibi kimsingi zikizingatia zaidi vita vya Urusi na Ukraine.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu