Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari: 09/11/2022

Vichwa vya Habari:

• Marekani Yatoa Wito wa Mapatano

• Muungano wa Mrengo wa Mbali Kulia wa Israel Umeshinda Uchaguzi

• India Kuendelea Kununua Mafuta Kutoka Urusi na Ushirikiano Kuzidi Kuimarika 

Maelezo:

Marekani Yataka Mapatano

Taarifa iliyovuja kutoka kwa maafisa wa Amerika kuitaka Ukraine kuanza majadiliano na Urusi, kulingana na ripoti. Ingawa Amerika haijaitisha mazungumzo ila ndio mara ya kwanza kutaka kutoa wazo la kufunguliwa mlango wa mazungumzo kwa umma. Kuvuja huko kwa taarifa hiyo kumekuja wakati ambapo kuna mkutano wa G20 utakaofanyika 15 Novemba, ambapo maraisi wote wa China, Xi Jinping na Putin wa Urusi watakuwepo. Kyiv itapewa masharti ya awali ya kuingia kwenye mazungumzo na Urusi ya kumaliza vita kwa kurudisha ardhi ya Ukraine iliyokwapuliwa, taarifa hiyo ni kulingana na afisa mmoja wa usalama wa ngazi za juu. Ni kana kwamba Amerika inatengeneza rai jumla kwa ajili ya kuanza mazungumzo, lakini haimaanishi kwamba vita vitafikia mwisho. Amerika inatazama vita vya Ukraie kama njia ya kuidhoofisha Urusi na kuilazamisha Ulaya kushikana na maslahi ya Amerika. Vita vinalenga kuidhoofisha Urusi ili Amerika iweze kukabilana na China.

Muungano wa Mrengo wa Mbali Kulia wa ‘Israel’ Umeshinda Uchaguzi

Muungano wa mrengo wa mbali kulia unaoongozwa na waziri mkuu wa zamani Benjamin Netanyahu umepata viti vingi katika bunge la Kiyahudi. Matokeo ya mwisho yanaonesha kwamba Netanyahu na muungano wa wazalendo wenye msimamo mkali – ambao wengi katika wao miaka iliyopita walikuwa hawatiliwi maanani  – wameshinda viti 64 katika bunge lenye jumla ya viti 120, ambapo kati ya viti 32 vimechukuliwa na chama kinchoongozwa na Netanyahu, Likud. Hadi sasa dola ya Kiyahudi imeshafanya uchaguzi mara tano tangu 2019 na vyama tofautu tofauti vilishindwa kufikia muafaka wa kutawala kwa pamoja. Benjamin Netanyahu ambaye alikuwa katika madaraka kwa miaka 12 tangu mwaka  2009 - 2021, ambapo alishtakiwa kwa ufisadi, ataitwa na rais wa Israel ili aunde serikali.  Netanyahu ni sehemu ya chama cha mrengo wa mbali wa kulia kinachomjumuisha Itamar Ben-Gvir, ambaye Wapalestina wanamuita “msaliti” kwa ‘Israel’ anayetakiwa kufukuzwa. Netanyahu atakuwa na siku 28 za kuunda serikali inayotarajiwa kuwa na mrengo wa kulia wa serikali ya Israel katika  historia.

India Kuendelea Kununua Mafuta kutoka Urusi na Hivyo Ushirikiano Kuzidi Kuimarika

India itaendelea kununua mafuta kwa Urusi kwa sasabu inafaidika mno, hayo yalisemwa na waziri wa mambo ya nje Subrahmanyam Jaishankar alipoitembele Urusi tangu kutokea uvamizi nchini Ukraine, ikiwa ni katika  kupambana na vikwazo vya Magharibi vinavyolenga kuidhoofisha Urusi kiuchumi. “Urusi imekuwa imara na mshirika mwenye kujaribiwa. Malengo yetu ya kimahusiano ni ushahidi wa miongo mingi ya maslahi kwa mataifa yetu,” Jaishankar alisema katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari. “ikwa ni nchi ya tatu kwa utumiaji wa mafuta na gesi dunani huku ikiwa na kipato kidogo, ni wajibu wetu wa kimsingi kuhakikisha kwamba wananchi wa India wananufaika na bidhaa za soko la dunia,” alisema. Maafisa wa Amerika na kutoka katika nchi za G7 wameendelea kufanya mazungumzo ya kuiwekea Urusi kikomo cha bei katika bei ya mafua yanayosafirishwa kupitia njia ya bahari, mchakato ambao utaonyesha matokeo yake 5 Disemba ili kuhakikisha Amerka na Ulya hawaharibu utaratibu wa soko la mafuta duniani. New Delhi na Beijing zimekataa kwa pamoja kuunga mkono vikwazo dhidi ya Urusi.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu