Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki wa Habari 30/08/2023

Hukumu ya Kwanza ya Kifo ya Ulimwengu kwa Machapisho ya Mitandao ya Kijamii

Mahakama moja ya Saudia imemhukumu mwalimu mmoja mstaafu kifo kwa kukosoa familia hiyo tawala katika ujumbe kwa wafuasi wake tisa wa mitandao ya kijamii. Kwa mujibu wa shirika la Human Rights Watch, Mohammed al-Ghamdi mwenye umri wa miaka 54 alihukumiwa kifo mnamo Julai 10 kwa makosa kadhaa yanayohusiana na shughuli yake kwenye YouTube na X, ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kama Twitter. Uamuzi huo huenda ukawa hukumu ya kwanza ya kifo kwa machapisho ya mitandao ya kijamii.

Mashtaka hayo yaliripotiwa kupewa dhidi ya mwalimu huyo aliyestaafu ni pamoja na "kumsifia mfalme au Mfalme Mtarajiwa kwa njia inayohujumu dini au haki", "kuunga mkono fikra ya kigaidi", na kusambaza habari bandia "kwa kusudi la kutekeleza uhalifu wa kigaidi". Kakake Mohammed, Saeed al-Ghamdi, aliandika nukuu ya tweet kwamba hukumu ya kaka yake inaweza kuwa jaribio la "kunichafua mimi kibinafsi baada ya majaribio ya kunirudisha nchini kufeli". Saeed, msomi wa Kiislamu, anaishi uhamishoni jijini London na anatafutwa na mamlaka za Saudia.

Pakistan Yateseka kutokana na Matunda ya Mikopo ya IMF

Umma nchini Pakistan umeingia mabarabarani kwa idadi kubwa juu ya bili kubwa za umeme nyuma ya ongezeko kubwa la ushuru wa wastani wa kitaifa. Hasira hiyo ilimfanya Waziri Mkuu wa mpito Anwaarul Haq azingatie na kuita mkutano wa "dharura" wa Jumapili kujadili suala hilo. Waziri mpito wa Habari Murtaza Solangi aliliambia gazeti la ‘Dawn’ kwamba Waziri Mkuu wa mpito alikuwa akizingatia machaguo kadhaa ya kupunguza mateso ya watumiaji wa umeme lakini hakuwez kutoa maelezo kwa vyombo vya habari hadi uamuzi wa mwisho katika suala hili. Akiongea na kituo cha kibinafsi cha Runinga alisema mtazamo kamili wa serikali ulikuwa juu ya kutoa misaada kwa raia katika bili za umeme. Mkuu wa umoja wa wafanyibiashara, Abdul Ghaffar Deshani, alisema serikali ilikuwa ikijaribu kuokoa uso na ilikuwa "inaficha utepetevu wake" kwa kubebesha mzigo watumiaji. Serikali ya Imran Khan na serikali iliyofuata ya Shabaz Sharif ilikubali kuondoa ruzuku za vidhibiti vya bei kwenye nishati ili kupokea mikopo ya IMF, kuondolewa kwa ruzuku hizo kumesababisha bei kupanda.

Mapinduzi Mengine huko Afrika Magharibi

Maafisa wakuu wa jeshi nchini Gabon walichukua mamlaka mnamo Jumatano, Agosti 30, muda mfupi baada ya kuchaguliwa tena kwa Rais Bongo kutangazwa. Wanajeshi kumi na mbili walionekana kwenye runinga ya kitaifa, wakisema wanabatilisha matokeo ya kura ya Jumamosi. Tume ya uchaguzi ilikuwa imempa Bongo 64.27% ya kura na mpinzani wake mkuu Albert Ondo Ossa akichukua asilimia 30.77. Maafisa hao walisema wanavunja taasisi zote za serikali, na kwamba mipaka ya nchi hiyo imefungwa. Kupinduliwa kwa Bongo kumetia kikomo ushikiliaji mamlaka wa familia yake wa miaka 56 nchini Gabon. Haya sasa ni mapinduzi ya nane katika koloni za zamani za Ufaransa barani Afrika katika miaka mitatu iliyopita.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu