Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari - 26/02/2020

Tukio lisilo la kawaida katika Kasri la Kifalme la Saudi

Marekekebisho ya Sheria ya Uraia itawafanya Waislamu kutokuwa na Dola, asema Katibu Mkuu wa UN

Trump Anaishambulia Mahakama Kuu

Maelezo:

Tukio lisilo la kawaida katika Kasri la Kifalme la Saudi

Mfalme wa Saudi Arabia Salman mnamo Alhamisi, 20 alipokea ujumbe, kutoka Kituo cha Mazungumzo ya Dini mseto na Thaqafa mseto cha Mfalme Abdullah bin Abdulaziz (KAICIID) ulijumuisha Mzayuni rabbi, David Rosen. Tangazo la uwepo wa Mzayuni rabbi katika kasri la kifalme la Saudi ni tukio lisilo la kawaida katika historia ya ufalme huo. Ingawa tukio liliangaziwa na Shirika la Habari rasmi la Saudi, orodha ya majina ya wahudhuriaji haikutolewa bali picha pekee ndizo zilizotolewa. Akaunti ya Twitter inayomilikiwa na jeshi la Kizayuni “Israeli kwa Kiarabu” ilifurahia tukio hili, likisema limefanyika ndani ya mchakato wenye “juhudi nzuri za kujenga madaraja ya kuvumiliana baina ya dini tofauti.” Waziri wa Ndani Aryeh Deri wa umbile la Kiyahudi alisema mwezi uliopita kwamba “Waisraeli” wanaruhusiwa kusafiri kwenda Saudi Arabia kwa ajili ya biashara au mambo ya kidini. Kauli hiyo ilitoa nafasi kwa Waisraeli kwenda Saudi Arabia kisiri kwa mara ya kwanza. Ufalme wa Saudi umekuwa na mahusiano kwa muda mrefu na umbile la Kiyahudi, sasa inajaribu kuyaweka wazi na miezi michache iliyopita imeshuhudia kuongezeka kwa vitendo hivyo vya kufikia hili.

Marekekebisho ya Sheria ya Uraia itawafanya Waislamu kutokuwa na Dola, asema Katibu Mkuu wa UN

Sheria mpya ya uraia ya India itapelekea idadi kubwa ya Waislamu kutokuwa na dola, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisema. Katika mahojiano na Gazeti la Dawn nchini Pakistan, alielezea wasiwasi wake kuhusiana na Mabadiliko ya Sheria ya Uraia, na kusisitiza kwamba nchi zinapokuwa zinaandaa sheria mpya zizingatie ubinadamu. “Kuna hatari ya watu kutokuwa na dola,” aliyasema hayo alipoulizwa kuhusu athari ya sheria hiyo mpya kwa jamii ya Waislamu. Mataifa na taasisi za Kimagharibi zinatambua yanayofanywa na India, lakini zimebakia kimya tu. India imekumbatiwa na jamii ya kimataifa, hususan Amerika ambayo inaiona kama nchi muhimu katika vita vyake vinavyokuja dhidi ya Uchina. Kila kinachoiimarisha India, Magharibi imeusaidia uongozi wa India wa BJP.

Trump Anaishambulia Mahakama Kuu

Donald Trump amechukua hatua ya kuwashambulia mahakimu wawili wa Mahakama Kuu kupitia Twitter na kwa matamshi katika vyombo vya habari. Hakimu Sonia Sotomayor aliukosoa utawala wa Trump kwa kukata rufaa aghalabu mbele ya Mahakama Kuu ili iingiliekati maamuzi yaliyotolewa na mahakama za chini, na mahakama hiyo kukubali mapendekezo aina hiyo. Kupitia Twitter, akijibu kipindi kilichorushwa hewani na Fox News’ The Ingraham Angle, Trump alizungumza maneno makali dhidi ya Sotomayor na Ruth Bader Ginsburg, ambaye aliwahi kumkosoa rais hapo awali. “Hili ni jambo baya kulizungumza,” Trump aliandika. “Kujaribu ‘kumuaibisha’ mtu kwa namna alivyopiga kura? Hakumkosoa Ginsberg aliponiita mimi ‘mtu bandia’. Wote wajitoe katika mambo yote yanayomhusu Trump!” Trump amekua akizidhoofisha taasisi zote za Amerika ili kudumisha nafasi yake binafsi, lakini analifanya hili wakati ambapo demokrasia na nidhamu ya Amerika inang’ang’ana ili kujihalalisha kwa watu wake.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 19 Machi 2020 09:19

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu