Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari - 20/03/2020

Mwangwi wa Muanguko Mkubwa? Uchumi wa Amerika Unaweza Kupungua Pakubwa

Kambi ya virusi vya Korona nchini Pakistan: ‘Hakuna Vifaa, Hakuna Ubinadamu’

Uchina Inatumana Madaktari na Barakoa Ng’ambo huku Maambukizi ya virusi vya Korona nchini Yakipungua

Maelezo:

Mwangwi wa Muanguko Mkubwa? Uchumi wa Amerika Unaweza Kupungua Pakubwa

Janga linalozidi kukuwa la virusi vya korona linatishia zaidi uchumi wa Amerika kuliko zama nyingine zozote tangu hatua za mwanzo za Muanguko Mkubwa miaka 90 iliyopita. Huku viwanda vingi vikifungwa sehemu au kabisa, uchumi wa Amerika unaweza kupungua pakubwa tangu kwa serikali kuanza kuweka rekodi za kila baada ya miezi mitatu baada ya Vita vya Dunia vya Pili. Madhara yake yanaweza kushindana na hali mbaya za mwanzoni mwa miaka ya 1930, ambapo dunia yote iliingia katika mdororo mrefu. Uchumi wa Amerika ulipungua kwa asilimia 13 mnamo 1932 (makadirio ya Amerika ya GDP ya miaka ya 1930). “Amerika inakabiliwa na lile ambalo linaweza kuwa ni janga kubwa la kiuchumi tangu kwa Muanguko Mkubwa wa miaka ya 1930,” alisema Mbunge Don Beyer, wa chama cha Democrat kutoka Virginia ambaye ni makamu mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi ya Pamoja ya Bunge. Watabiri wa Wall Street wamekuwa wakipunguza makadirio yao katika hali ya kushtusha mno huku madhara yakiendelea. JP Morgan ndiyo yenye wasiwasi zaidi, ikikadiria asilimia 14 ya kudorora kwa GDP ndani ya kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni. Mdororo mkubwa kuwahi kurekodiwa kila baada ya miezi mitatu ndani ya historia ya Amerika ilikuwa asilimia 10 katika miezi mitatu ya kwanza ya 1958 katika kipindi cha muanguko mfupi lakini mkubwa. Takribani watu milioni 2 walipoteza ajira zao chini ya mwaka mmoja. Hata katika kipindi hatari zaidi cha 2007-2009 cha Muanguko Mkubwa, kiwango kikubwa kilichopungua cha GDP kilikuwa asilimia 8.4 katika robo ya nne ya 2008. Ikikaribiana na JP Morgan ni Benki ya Deutsche ambazo zimetabiri kuwa uchumi utapungua kwa asilimia 13 katika robo ya pili. Wanauchumi wa Oxford wanauweka mdororo kuwa asilimia 12 na kupoteza ajira milioni 1. Wanauchumi wa Capital wanaona asilimia 10 ya mdororo wa GDP, TS Lombard asilimia 8.4 na Nationwide asilimia 8. Wanauchumi wamegawanyika kuhusu ni wakati gani ambapo uchumi utarudi kuwa sawa, lakini hakuna mmoja wao anayesambaza mazungumzo ya ujasiri wa Ikulu ya Trump. Rais Trump aliahidi mnamo Alhamisi kuwa uchumi utapaa kama “roketi” punde kuenea kwa virusi kutakapo dhibitiwa. Katibu wake wa Hazina, Steven Mnuchin, naye pia alitabiri mnamo Alhamisi kuwa uchumi utarudi kwa kishindo “kikubwa” ndani ya robo ya nne, akisema “tutaviua virusi hivi” na kurudi katika “dunia ya kawaida.” Utawala wa Trump unalenga kutoa zaidi trilioni dola 1 za msaada kwa biashara na watumizi ili kujaribu kuusaidia uchumi kuhimili dhoruba. Mauzo yameanguka, kufutwa kazi kunazidi na Dow Jones Industrial Average DJIA imepoteza thuluthi moja ya thamani yake ndani ya wiki tatu tu.  [Chanzo:  Market Watch]

Magharibi na hususan Amerika imekosa mbadala wa kupangilia upya uchumi. Zana kama riba za viwango vya chini na urahisishaji viwango zimekuwepo tangu 2008 na uchumi wa nchi za Kimagharibi haujakua kamwe. Huku kukiwa na janga la covid19, si kweli kuwa hatua hizi zitafanyakazi na hivyo dunia itabidi itafute makubaliano mapya ya Bretons Woods.

Kambi ya virusi vya Korona nchini Pakistan: ‘Hakuna Vifaa, Hakuna Ubinadamu’

Ni harufu ndiyo iliyokuwa mbaya mno. Ndani ya kambi hii iliyojaa vumbi katika mpaka wa Pakistan na Iran, ambayo kwa hatua ya mwanzo ilikuwa na watu zaidi ya 6,000, harufu imejaa angani ya jasho, takataka na kinyesi cha mwanadamu. Hakukuwepo na makaazi ya kikweli, watu watano tu katika kila hema, hawana vyoo, tauli wala mablanketi. Kambi iliyoko ndani ya mji wa Taftan mkoa wa Balochistan, ilitakiwa kuwa ndio eneo safi la kutengea watu, ili kuzuia kuenea kwa virusi vya korona kutoka Iran, ambayo imekumbwa na mkurupuko mkubwa mno kiulimwengu. Badala yake, kwa mujibu wa Mohammed Bakir, aliyeshikiliwa huko kwa wiki mbili, ilikuwa zaidi ya “jela… sehemu chafu niliyowahi kuishi maishani mwangu.” “Hizo zilikuwa ni mchana na usiku migumu maishani mwangu,” alisema Bakir. “Tulitendewa kama wanyama. Hakukuwa na vifaa wala ubinadamu na kila kitu kilikuwa mkanganyiko. Hawakuwa wamejiandaa; hakukuwa na chochote kwa ajili yetu kulalia isipokuwa mahema machafu.” Maelfu ya watu wamewekwa katika sehemu karibu karibu zilizo na joto na hali duni ndani ya Taftan, huku wakikosa hata hatua msingi za tahadhari ili kuzuia kuenea kwa virusi. Kwa mujibu wa madaktari walioko katika kambi hiyo, hata wale waliokuwa na dalili hawakupimwa na kutengwa, na kulikuwa na upungufu mkubwa wa madaktari na wauguzi. Kulikuwa na upungufu wa vifaa vya matibabu, madaktari wachache waliokuwepo iliwabidi walipie wenyewe dawa za dharura. Hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba maandamano yalianza miongoni mwa wale waliotengwa. “Si huduma ya utenganishaji wala utaratibu wa upimaji ilikuwa yenye kuridhisha kamwe,” alisema daktari mmoja, aliyeomba asitajwe jina. “Siku 20 za mwanzo, watu wengi walikuwa na dalili, lakini hakukuwa na upimaji kamwe. Hatukuwa na vifaa vya kupimia kwa wiki tatu. Mtoto mmoja alitumwa katika hospitali huko Quetta, na alipatikana mgonjwa. Lakini hakukuwa na utenganishaji wala upimaji kwa mtu mwingine yeyote. “Kulikuwepo na wagonjwa waliokuwa na kisukari, uvimbe wa ini na magonjwa mengine waliotengwa kwa siku 14 pasi na dawa sahihi yoyote. Hali zao zilikuwa mbaya mno na walitendewa kama wanyama.” Mpaka baina ya Pakistan na Iran ni zaidi ya maili 600 na mzunguko baina ya nchi mbili ni jambo la kawaida mno, hususan miongoni mwa wachache katika Waislamu Mashia nchini Pakistan wanaosafiri kwenda Iran kwa ziara za kidini. Pia ni barabara muhimu ya biashara. Lakini ndani ya wiki mbili zilizopita, imekuwa ndio kitovu cha virusi vya korona, huku maambukizi yakizidi pakubwa kila kukicha. Kuna kesi 302 za virusi vya korona nchini Pakistan, idadi kubwa ndani ya Asia kusini. [Chanzo: The Guardian

Serikali ya Khan imefeli katika kila suala ambalo imekabiliwa nalo. Covid19 imefichua zaidi uzembe wa serikali ya Khan na nidhamu inayoisimamia. Kwa matumaini, hili linaweza kuwachochea watu wa Pakistan kuipundua serikali na nidhamu ya kirasilimali na badala yake kuweka dola ya Khilafah.

Uchina Inatumana Madaktari na Barakoa Ng’ambo huku Maambukizi ya virusi vya Korona nchini Yakipungua

Katika wiki zilizopita, Uchina imetumana zana za kupimia virusi vya korona kwa Cambodia, ilitumana ndege zilizokuwa zimejaa viingiza hewa, barakoa na madaktari kwenda Italia na Ufaransa, na kuahidi kuzisaidia Ufilipino, Uhispania na nchi nyingine na kutumana madaktari kwenda Iran na Iraq. Rais wa Uchina Xi Jinping, alitoa matamshi ya faraja, akimwambia waziri mkuu wa Uhispania, Pedro Sánchez, “jua huja baada ya dhoruba,” na kuongezea kwamba nchi mbili hizo lazima zizidishe ushirikiano na mahusiano baada ya mkurupuko. Huku mkurupuko wa virusi vya korona ukienea na nchi zikijitahidi kupambana. Uchina imejitengea nafasi kama kiongozi na mfadhili katika afya ya umma, ikijenga aina fulani ya nguvu nyepesi ambayo Beijing inaihitaji wakati huu ambapo mzozo wa Amerika na Uchina na uchunguzi wa ushawishi wa Uchina duniani unazidi kuendelea. Virusi vya korona vilitokeza katika mji wa katikati wa Uchina wa Wuhan mnamo Disemba na kuisukuma nchi hiyo katika hali ya dharura kwa kuwa zaidi ya watu 80,000 walikuwa wameambukizwa na zaidi ya 3,000 walikuwa wamefariki. Hasira za umma na kuikosoa serikali kutokana na udhibiti wake wa taarifa na majibu yake ya polepole, na kupelekea virusi kusambaa, na kupelekea kuwa tishio kubwa kwa uongozi wa Uchina katika miongo. Wajuzi wanasema kwamba, ilhali juhudi za wanadamu ni za kweli, zina mwisho wa kisiasa unaostahili kuzingatiwa. Katika mazungumzo ya simu na waziri mkuu wa Italia, Giuseppe Conte, wiki hii, Xi alisema ana matumaini ya kuasisi “barabara ya hariri ya afya” kama sehemu ya mpango wa Uchina wa kiulimwengu wa Ukanda Mmoja, Barabara Moja, ambao umepata kukoselewa kutoka kwa nchi ambazo zinachelea kupanuka kwa Uchina na ushawishi wake. “Hakuna tatizo kwa Uchina kuzisaidia nchi za Ulaya na nyingine, hususan wakati huu ambao imepata nguvu kutokana na kudhibiti virusi vya korona nyumbani. Lakini pia iko wazi kwamba [Beijing] inautizama msaada wake kama zana ya kipropaganda,” alisema Noah Barkin, mkuu katika German Marshall Fund. [Chanzo:  The Guardian]

Kujikwamua kwa Uchina kutokamana na virusi vya Covid-19 kumeiwezesha Beijing kubuni mahusiano mapya na nchi za Ulaya, na hili linaashiria kuanguka kwa utaratibu wa Amerika ndani ya Ulaya.

#Covid19

#Korona

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 26 Machi 2020 06:33

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu