Jumatano, 07 Dhu al-Hijjah 1443 | 2022/07/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari – 25/03/2020

Michezo ya Vita Inaendelea

Zoezi la Jaribio la Mkurupuko Lilionyesha Amerika ilikuwa Haijajiandaa Vizuri kwa Virusi vya Korona

Nidhamu za Afya za Kimagharibi Zinajizatiti dhidi ya Mkurupuko wa Virusi

Maelezo:

Michezo ya Vita Inaendelea

Kuendelea kusambaa kwa virusi vya korona kumepelekea michezo ya kivita kucheleweshwa, lakini sio kwa Amerika na Umoja wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kwani wanajeshi 4,000 wa Amerika na wapiganaji wa UAE walichanganyika na kufanya mazoezi ya kijeshi ya kila mwaka mara mbili ya Ghadhabu Asili. Mazoezi kimsingi yalifanyika katika Kambi ya al-Humra sehemu ambayo walijenga mfano wa jiji la Irani, misikiti n.k kwa lengo la kufanyia mazoezi ya wanajeshi kiuvamia na kuuchukua mji huo. Wanajeshi waliigiza kupita katika njia ndogondogo wakiwatafuta “wanajeshi pinzani.” Wanajeshi wa Amerika walichukua nafasi miongoni mwa UAE na Kuwait, wakiwa sambamba na Diego Garcia. Balozi wa Amerika Rakolta alielezea mazoezi hayo kuwa “ni ya kujilinda” ingawa kiuhalisia yalionyesha wazi kuwa na malengo ya kuvamia na kuuchukua mji wa Iran. Rakolta aliongezea kwamba haoni kuwa ni “uchokozi” kuiambia Iran kwamba “tunakuja.” Ni vigumu kwa Iran, na yeyote yule kuamini kwamba shughuli hizo za kijeshi haziwahusu wao. Ilhali watu wengi wanakufa nchini Amerika kutokana na virusi, Amerika imeipa kipaumbele michezo ya kivita.

Zoezi la Jaribio la Mkurupuko Lilionyesha Amerika ilikuwa Haijajiandaa Vizuri kwa Virusi vya Korona

Serikali ya Trump ilifanya zoezi la jaribio la mrupuko mkali wa mafua yasiyokuwa na chanzo ilibainika kuwa Amerika haijajianda vizuri, kwa mujibu wa na kuonyesha, The New York Times. Matokeo ya ripoti kielelezo yalionyesha kwamba Amerika ilifanya maandalizi hafifu sana ya chini ya kiwango katika kujiandaa na mkurupuko aina ya virusi vya korona, virusi ambavyo vimesambaa katika majimbo yote 50 na bado hayafikia kileleni nchini Amerika, Times iliripoti. Kuanzia Januari hadi Agosti zilizopita, Idara ya Afya na Huduma kwa Binadamu ilifanya zoezi lililoitwa "Crimson Contagion" lilijumuisha washiriki 19 kutoka mashirika ya majimboni, kadhaa kutoka katika majimbo, mataifa ya kikabila, hospitali na mashirika yasiyokuwa ya serikali kwa mujibu wa ripoti kielelezo ya HHS iliyokuwa na Times. Mazoezi hayo ya mkurupuko wa kubuni yalihusisha kundi la watalii wanaozuru Uchina ambao kisha waliambukizwa na kurudi nyumbani nchi tofauti, ikijumuisha Amerika, ripoti hiyo kielelezo ilisema. Katika hali hii, virusi kwanza viligundulika huko Chicago, kwa mujibu wa ripoti. Kisha ripoti iliangazia majimbo ambayo yalipata “changamoto nyingi” yakiomba rasilimali kutoka serikali ya kitaifa “kutokana na ukosefu wa mchakato makinifu uliofahamika wa kufanyiwa kazi unapotaka rasilimali” ripoti ilisema.

Nidhamu za Afya za Kimagharibi Zinajizatiti dhidi ya Mkurupuko wa Virusi

Italia inajizatiti kupambana na athari za kufungiwa ndani kwa muda mrefu. Ingawa idadi ya maambuki ya virusi vya korona inapungua, wafanyakazi muhimu wana wasiwasi kuwa hali zao sio nzuri. Vituo vya mafuta nchi nzima vimeanza kufungwa wakielezea hatari za kiafya kwa wafanyakazi. Wafanyakazi wa benki wanatishia kufanya mgomo lau hatua za kiusalama hazitochukuliwa. Mawaziri wa uchumi na viwanda wa Italia watazungumza na miungano mitatu mikubwa, ambayo imeitaka serikali kupanua orodha ya kazi ambazo sio za umuhimu. Ili kuisaidia Italia kuweza kuziba mapengo yake ya janga la kiusimamizi, Urusi imezidisha juhudi zake za msaada kwa kutumana wajuzi wa kijeshi na vifaa, hususan za kuchunguza na kutibu. Urusi pia imetumana majeshi ya madaktari wa kutembea na takribani wanajeshi wajuzi wa virusi na magonjwa. Ujerumani nayo imeelezea utayari wake kuisaidi Italia kwa kuweka wazo la kuwaboreshea mikopo kupitia Mpango Imara wa Ulaya. Maelezo bado yanajadiliwa; Ujerumani inasukuma kuwepo kwa masharti machache ilhali Italia haitaki masharti. Italia sio ya kipekee, japo imeathirika zaidi kutokana na janga hili, nidhamu nyingi ndani ya ulimwengu ulioendelea zinajizatiti kupambana na mkurupuko baada ya miongo kadhaa ya mapungufu na baada ya muongo mkali uliopita.

#Covid19    #Korona                   كورونا#

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 30 Machi 2020 15:41

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu