Jumatano, 07 Dhu al-Hijjah 1443 | 2022/07/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 08/04/2020

Vichwa vya habari:

Madaktari Wakamatwa kwa Kufanya Maandamano

Taliban Yajitoa Nje ya Mazungumzo 'Yasiyo na Matunda'

Nafasi Nne kati ya Nafasi Tano za Kazi za Watu Zimepata pigo la Janga la Korona

Maelezo:

Madaktari Wakamatwa kwa Kufanya Maandamano

Polisi wamewakamata zaidi ya madaktari 150 na wafanyikazi wengine wa matibabu nchini Pakistan katika jiji la Quetta, tukio hilo lilitokea baada ya madaktari kuandamana dhidi ya ukosefu wa vifaa vya kisawa sawa vya kujilinda na maambukizi ya virusi vya Korona wakati wa kutibu wagonjwa. Maandamano na msako uliofuata yanaangazia uhalisia wa namna ambavyo Pakistan inang'ang'ana kuzuia janga linaloendelea la Covid-19. Ukamataji huo na muendelezo wa ukosefu wa vifaa vya matibabu vitachochea zaidi maandamano katika sehemu nyingine za nchi, hivyo kupelekea kusambaa zaidi kwa virusi. Maandamano hayo yanajiri, huku kukiripotiwa kwamba zaidi ya makumi ya madaktari wa Pakistan wamekuwa wakiambukizwa Covid-19 wakati wakiwatibu wagonjwa. Hivi sasa Pakistan ina kesi zilizo thibitishwa zaidi ya 3,200 za virusi hivi, na wagonjwa 50 kati yao wameshafariki.

Talibani Yajitoa nje ya Mazungumzo 'Yasiyo na Matunda'

Taliban imejiondoa nje ya mazungumzo ya kihistoria ambayo yalidhaniwa kuwa yangesaidia kutoa njia ya kuelekea katika amani nchini Afghanistan. Msemaji wa kundi hilo alisema mazungumzo hayo ya kwanza ya ana kwa ana na serikali yamethibitisha "kukosa matunda yoyote".

Mazungumzo yamevunjika kutokana na kipengee cha kubadilishana wafungwa kilichokubaliwa kati ya Amerika na Taliban. Kulingana na Matin Bek, ambae ni mwanachama katika timu ya upatanishi ya serikali alisema Taliban inataka kuachiliwa huru kwa makamanda wake 15 ambao wanaaminika kuhusika katika yale yanayo itwa kuwa mashambulizi makubwa. "Hatuwezi kuwaachilia huru wauaji wa watu wetu," alisema. Lakini msemaji wa Taliban aliushutumu utawala wa rais Ashraf Ghani kwa kuchelewesha kuwaachilia huru wafungwa hao "chini ya kisingizio kimoja au chengine". Serikali hiyo imesema ipo tayari kuwaachilia huru wafungwa 400 wa Taliban walio na tishio dogo kama ishara ya nia njema, kwa badali ya kupunguzwa kwa kiwango kikubwa cha ghasia.

Nafasi Nne kati ya Nafasi Tano za Kazi za Watu Zimepata pigo la janga la Korona

Jumla ya asilimia 81 ya nguvu kazi ya kiulimwengu ya watu bilioni 3.3 ima sehemu zao za kazi zimefungwa kikamilifu au zimefungwa nusu. Kuzuiwa kwa harakati za maisha za kila siku kumepelekea kampuni nyingi kufunga shughuli zake au kufuta wafanyakazi kwa muda au kuwafuta kazi kabisa. Shirika la Kimataifa la Wafanyakazi (ILO), ambayo ni taasisi ya Umoja wa Mataifa, limekuwa likiangalia athari ya kiulimwengu kwa msururu wa michoro ya takwimu. Kazi zao zinaonesha mizani ya athari ya mlipuko wa virusi vya Korona. "Wafanyakazi na biashara vinakabiliwa na janga, katika nchi zilizo endelea pamoja na zinazo endelea kiuchumi," alisema mkurugenzi mkuu wa ILO Guy Ryder. "Tunahitajika kusonga mbele kwa haraka, kwa umakini, na kwa pamoja. Hatua sahihi, na za dharura huenda zikaleta tofauti kati ya kubakia hai na kuporomoka” Janga la tiba na afya la kiulimwengu hivi sasa ni rasmi limekuwa ni janga la kiuchumi.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 25 Aprili 2020 12:43

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu