Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: 11:14:15 (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa  vya Habari 01/04/2020

Vichwa vya habari:

Ukosekanaji wa uongozi wa Amerika wa Kiulimwengu

Umoja wa Mataifa waonya kuwa Pakistan huenda ikapata pigo kubwa zaidi kwa kuanguka kiuchumi kutokana na Janga la Korona

Amerika Inapendekeza suluhusho lilelile la Venezuela

Maelezo:

Ukosekanaji wa uongozi wa Amerika wa Kiulimwengu

Mwishoni mwa wiki, Amerika iliipiku China kwa idadi ya watu waliofariki kwa mkurupuko wa virusi vya korona, uongozi wa kiulimwengu umeonekana kutokuwepo katika muundo wa utawala wa kiulimwengu. Wakati ambao Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi saba zenye uwezo kubwa duniani [G7] zikielekea kukubali mwito wa kiulimwengu dhidi ya janga la virusi vya korona, juhudi za Amerika za kuinyoshea kidole cha lawama China kwa tishio hili zilikwama. Kusisitiza kuviita virusi hivi virusi vya China na kuilaumu China kupitia kwa Waziri wa Kigeni wa Amerika, Mike Pompeo, kulisaidia kuhakikisha hakutakuwa na juhudi zozote za maana za pamoja kutoka kwa mataifa hayo mawili yenye nguvu zaidi duniani. “kwa upande wangu kile kinacho dhihirika ni kukosekana kwa Amerika katika midahalo ya umma..

Kimsingi Amerika haiko katika ramani, huku China ikijaa ndani ya ramani,” Nathalie Tocci, mkurugenzi wa taasisi ya Italia inayo husika na mambo ya kimataifa na mshauri wa zamani wa sera wa Muungano wa Ulaya, alisema. Kuanzia katika sokomoko juu ya upimaji hadi upingaji wa Trump kwa muda wa mwezi mzima kuhusu uzani wa tishio hili na utafutaji wake wa kudumu wa umaarufu wa kisiasa, Amerika imejionyesha kuwa sio chochote ila ni mfano wa kuigwa na sehemu zote duniani.

Umoja wa Mataifa waonya kuwa Pakistan huenda ikapata pigo kubwa zaidi kwa kuanguka kiuchumi kutokana na Janga la Korona

Mnamo Jumatatu Kongamano la UM juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD) lilisema katika ripoti mpya kuwa nchi zanazo endelea – ambazo kwa mujibu wa orodha ya taasisi moja ya Umoja wa Mataifa ni nambari 170 - mwaka huu zitahitajia msaada wa dolari trilioni 2.5 kwa ajili ya kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi ulio sababishwa na janga hili. “Nchi za Afrika zilizo chini ya jangwa la sahara zitapata pigo kubwa pamoja na nyingine, ikiwemo Pakistan na Argentina,” alisema Richard Kozul-Wright, mkurugenzi wa mikakati ya utandawazi na maendeleo katika UNCTAD, ambaye aliipitia ripoti nzima. Akitaja “mjumuiko wa mambo yenye kuogopesha”, yakiwemo ongezeko kubwa la madeni, kushuka kwa bei za bidhaa, na mgogoro mkubwa wa kiafya, Kozul-Wright alisema kwamba kulingana na makadirio, virusi vya korona vitasababisha upungufu wa kifedha wa zaidi ya dolari trilioni $2-$3 mwaka huu na mwaka ujao.

Amerika Inapendekeza suluhusho lilelile la Venezuela

Kushindwa kukubwa kwa rais wa Amerika Donald Trump mwaka 2019 kulikuwa ni kushindwa kumpindua rais wa Venezuela Nicolas Maduro, baada ya kuonyesha wazi kuunga mkono upinzani. Kufikia mwishoni mwa 2019 Trump aliiwekea vikwazo nchi nzima vilivyo ongezea juu ya asilimia milioni 10 ya mfumko wa bei. Hivi sasa Amerika imetangaza kujiandaa kuipunguzia vikwazo Venezuela ili kuunga mkono mapendekezo mapya ya kuunda serikali ya mpito, ambayo yanayo muhitaji Nicolas Maduro na kiongozi wa upinzani Juan Guaidó kukaa kando kwa ajili ya kulipisha baraza la utawala linalo jumuisha watu watano, maafisa wa Amerika walisema. Chini ya mpango huo, Maduro na Guaidó, ambaye nchi takriban 60 zinamtambua kama kiongozi halali wa Venezuela, wote watakaa pembeni na kuliachia madaraka baraza la nchi linalo jumuisha watu watano ili kuiongoza nchi hiyo hadi wakati uchaguzi wa raisi na ubunge utakapo fanyika ndani ya miezi 6 hadi wa 12.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu