Jumamosi, 11 Rajab 1446 | 2025/01/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Vichwa Vya Habari 09/05/2020

Vichwa Vya Habari:

Mamluki 1200 wa Urusi wanapigana upande wa Haftar nchini Libya

Watu wa Kashmir waendelea Kuandamana Kupinga Mauaji chini ya Uvamizi wa India

Ripoti Mpya Zaangazia Uharibifu wa Mazingira Unaofanywa na Magharibi

Maelezo:

Mamluki 1200 wa Urusi wanapigana upande wa Haftar nchini Libya

Kulingana na alJazeera:

Kampuni ya kibinafsi ya Urusi ya kandarasi ya kijeshi inayoitwa Wagner imepeleka takriban mamluki 1200 hadi Libya ili kutia nguvu vikosi vya kijeshi vya kamanda wa kijeshi Khalifa Haftar, kwa mujibu wa ripoti iliyo vuja ya Umoja wa Mataifa.

Ripoti hiyo yenye kurasa 57 iliyo andaliwa na waangalizi huru wa vikwazo, iliwasilishwa kwa kamati ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Inayo shughulikia vikwazo vya Libya, taarifa hiyo ilisema Wagner ilipeleka mamluki hao katika kufanya kazi maalumu ya kijeshi, ikiwemo timu za wadenguaji.

"Tumefahamu kwa kipindi kirefu kwamba mamluki wa Urusi wanafanya shughuli zao nchini Libya lakini pengine hatukufahamu kiwango cha operesheni zao," James Bays wa Aljazeera alisema, akiripotia kutoka New York.

Mizozo katika nchi za Kiislamu aghlabu husababishwa na dola za nje. Ni wazi kwamba nyuma ya Urusi kuna Amerika. Kwa uhalisia Mzozo wa Libya ni kati ya Uingereza, inayo unga mkono Serikali ya Makubaliano ya Kitaifa iliyopo Tripoli, na Amerika, ambayo inataka kuiondoa serikali hii kwa kuvitumia vikosi vya Jenerali Haftar.  Baada ya kushindwa Iraq na Afghanistan, Amerika imekuwa ikiepuka kutumia majeshi yake katika ardhi za ulimwengu wa Kiislamu, na hivyo hutumia majeshi ya nchi nyingine kwa aili ya kufikia malengo yake.

Mambo ya Waislamu hayawezi kuwa mazuri hadi Waislamu watakapo shughulikia mambo yao wenyewe, kupinga kuingiliwa na dola za kikafiri za kigeni za kibepari, na kuziregesha ardhi zao katika utawala wa Uislamu kama ilivyo kuwa mwanzo.

Watu wa Kashmir waendelea Kuandamana Kupinga Mauaji chini ya Uvamizi wa India

Kulingana na Dawn:

Waandamanaji wanaoipinga India wameendelea kuandamana na kufanya vurugu kwa siku ya tatu mfululizo katika jimbo la Kashmir siku ya Ijumaa, hii ni kutokana na mauaji ya kiongozi wa juu wa upinzani yaliyo fanywa na vikosi vya kijeshi vya India.

Kiongozi wa Kashmir Riyaz Naikoo na wasaidizi wake waliuwawa katika mapigano ya bunduki na vikosi vya India mnamo Jumatano katika eneo la kusini mwa Awantipora, na kusababisha kutokea kwa vurugu katika maeneo mengi.

Vurugu ziliendelea mnamo ijumaa ambapo waandamanaji wanaopinga India waliyarushia mawe majeshi ya serikali, ambayo yalijibu kwa kuwapiga risasi za mpira na kuwarushia gesi ya kutoa machozi ili kusambaratisha maandamano hayo. 

Upinzani mkali wa Waislamu katika maeneo yaliyo kaliwa, kama vile Kashmir na Palestina, yanaonyesha kwa ujasiri upinzani wao kwa utawala wa makafiri wageni. Huu ni muendelezo wa ukoloni kwa ardhi za Waislamu unaofanywa na mabepari wa Kimagharibi.

Lakini hata baada ya Wamagharibi kuondoa majeshi yao kutoka katika ardhi za Waislamu, ardhi zilibakia zimekaliwa kwa kuendelea kutawaliwa na watu pamoja na nidhamu ambazo zimedumisha tiifu kwa Magharibi. Muda umefika sasa kwa Umma wa Kiislamu kurudisha ubwana wake kikamilifu na kuisimamisha tena Dola ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Mtume (saw).

Ripoti Mpya Zaangazia Uharibifu wa Mazingira Unaofanywa na Magharibi

Kulingana na Reuters:

Joto na unyevu nyevu vinazidi kuongezeka katika ulimwengu, na kutishia maisha ya mamilioni ya watu na uchumi kiasi cha kupelekea hatari kubwa kufanya kazi nje ya majumba, wanasayansi walisema mnamo Ijumaa.

Sehemu za Australia, India, Bangladesh, Ghuba ya Uajemi, China, Mexico na Amerika zimekuwa na uzoefu wa kukumbana na mamia ya matukio kama hayo tangu mwaka 1979, ilisema taarifa kutoka katika jarida la uchunguzi wa kisayansi.

Hali hizi zenye kuumiza zimekuwa zikidumu kwa masaa mawili au moja tu lakini mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha hali hiyo kuongezeka hadi masaa sita kwa mara moja na hivyo kuongeza idadi ya maeneo yanaoathirika, mwandishi Colin Raymond aliuambia Wakfu wa Thomson Reuters.

“Hayo ni makisio ya kihafidhina lakini hilo limekuja mapema mno bila mtu yoyote kutarajia,” alisema Raymond, ambaye alifanya uchunguzi huo akiwa ni mwanafunzi wa uzamifu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Columbia na sasa anafanya kazi na shirika la mambo ya anga la Amerika (NASA).

Uharibifu unaofanywa na makafiri wa Kimagharibi umepanuka zaidi kuanzia kwenye utumizi mbaya wa ustaarabu hadi kufikia kuharibu sayari ambayo sote tunaishi ndani yake. Upigiji debe ovyo wa daima kuongeza ukuaji wa kiuchumi, utiifu katika mambo ya kiuchumi kwa maslahi ya kimada pekee na uporaji wa rasilimali na utajiri wa ulimwengu imesababisha madhara yasio tatulika yasiosemeka kwa mazingira ya mwanadamu ya kiasili.

Mwanadamu na mazingira yake havitapoa hadi pale uongozi wa mambo ya ulimwengu urudi kwa wahusika wenye kujali utu sio kwa ajili ya maslahi kimada ya kibinafsi bali kama jukumu na faradhi ya kidini. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, hivi karibuni wanadamu watashahudia kusimama tena kwa Dola ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Mtume (saw) yenye kutekeleza uangalizi bora sio tu kwa wanadamu pekee bali hata kwa wanyama, miti, mimea, na mazingira yote ya dunia kwa ujumla.

#Covid19    #Korona       كورونا#

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 13 Juni 2020 08:18

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu