Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali:

Hadith za "Khilafah kwa Njia ya Utume"

Kwa: Mamoon Soofi

(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalaamu alaikum Warahmatullahi Wabarakatuhu Ewe Shaykh Ata ibn Khalil Abu Rashta Nataraji umzima, familia yako na Mashababu wote katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Namuomba Mwenyezi Mungu (swt) atukirimu katika kurudisha Khilafah kwa Njia ya Mtume Wetu Kipenzi Muhammad (saw).

Jina langu ni Mamoon Soofi na mimi ni katika mashababu wa Canada. Nilitaka kuuliza juu ya usahihi wa hadith iliyopo katika Musnad ya Imam Ahmad (nambari 18596) juu ya "Khilafah kwa njia ya Utume"

Mijadala yangu yote kufikia hivi sasa hunipelekea kutaja tu hadith hii na nisiongeze kitu chochote zaidi. Mpaka hivi karibuni, niliombwa kuchunguza usahihi wa hii hadith yenyewe. Ni muhimu kutaja hapa kuwa Kiarabu sio lugha yangu ya mama kwa hivyo nina kikomo katika kupata yale ninayoweza kuyatafuta na kuyatafiti.

Kwa hayo nimekumbana na nakala moja inayodai yafuatayo:

Hii hadith tuitumiayo iliopo katika Musnad ya Imam Ahmad (nambari 18596) ni mojawapo ya riwaya nyingi ambapo inasema "Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume..." Hiki kipande cha mwisho kimesimuliwa na mtu mmoja pekee (Ibrāhīm al-Wāsiṭī) ambaye kwamba mapokezi yake ni matruk ("hukataliwa") kumaanisha hayategemeki kabisa kiasi ya kutoweza kunukuliwa.

Hii hapa nakala ya pdf ya Kiarabu inayoeleza hayo:

https://hawramani.com/wp-content/uploads/2018/12/idlibi_hadith_five_ages_islamic_state_prophethood.pdf

Nitashukuru sana kama utabainisha hili jambo kwangu ili niweze kufahamu hapa paliponiacha njia panda.

Mwenyezi Mungu Akubariki Ewe Shaykh Ata!

Namuomba Mwenyezi Mungu (swt) Azidi kutusaidia katika kutia juhudi kufuata njia iliyonyooka.

Ameen Ameen Ameen!!

Mamoon Soofi

Jibu:

Waalaykum salam Warahmatullahi Wabarakaatuhu

1- Hakika umetaja katika swali lako:

(Hadith hii tuitumiayo iliopo katika Musnad ya Imam Ahmad (nambari 18596) ni mojawapo ya riwaya nyingi ambapo inasema "Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume...)

Na katika Musnad ya Ahmad hakuna chini ya nambari (18596) Hadith yoyote inayozungumzia Khilafah kwa njia ya Utume! Bali Hadith ya nambari hiyo inaambatana na mambo mengine yasiyo na mahusiano na Khilafah kwa njia ya Utume na Hadith iliokusudiwa iko katika mlango wa (Hadith ya Abdillah bin Abi Awfaa radhi za Allah zimwendee).

2- Ama Hadith za Khilafah kwa njia ya Utume zimepokewa katika vyanzo vingi:

A- Katika Musnad ya Ahmad: 17680 - (Ametuhadithia Suleiman bin Daud Attwalisiy amenihadhia Daud bin Ibrahim Al-waasitiy amenihadhia Habib bin Saalim kutoka kwa Nua'man bin Bashir asema: Tulikuwa tumekaa katika Msikiti pamoja na Mtume (saw), na Bashir alikuwa ni mtu anayeacha kuongea akaja Abu Thaa'laba Al Khushaniy akasema ewe Bashir bin Saa'd je, umehifadhi Hadith yoyote ya Mtume (saw) kuhusu viongozi? Akasema Hudhaifa mimi nimehifadhi Khutba yake, Abu Thaa'laba akaketi.  Hudhaifa akasema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

»تَكُونُ النُّبُوَّةُ فِيكُمْ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً عَاضّاً فَيَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ «ثُمَّ سَكَتَ.

"Utume utakuwa kwenu kwa muda atakao Mwenyezi Mungu kisha atauondoa atakapo kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume itakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu kisha ataiondoa atakapo kuiondoa, kisha utakuwepo ufalme wa kurithishana utakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu kisha atauondoa atakapo kuuondoa, kisha utakuwepo utawala wa kiimla utakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu kisha atauondoa atakapo kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa Njia ya Utume" kisha akanyamaza.)

B- Na katika Dalailu Nubuwwah ya Al Bayhaqiy 2842- ( Ametuhadithia Abubakri Muhammad bin Al Hassan bin Furik Mwenyezi Mungu amrehemu, ametupa habari Abdullah bin Jaa'far Al Aswbihani, ametuhadithia Yunus bin Habib, ametuhadithia Abu Daud Attwiyaalisiy, ametuhadithia Daud Al Waasitiy, asema: Na alikuwa ni mtu wa kutegemewa (Thiqah), amesema: Nimemsikia Habib bin Saalim, amesema: Nimemsikia Al Nuu'man bin Bashir bin Saa'd, Katika Hadith aliyoitaja asema: Akaja Abu Thaa'laba akasema: Ewe Bashir bin Saa'd, Je umehifadhi Hadith yoyote ya Mtume (saw) kuhusu viongozi?, Na Hudhaifa alikuwa ameketi na Bashir, Hudhaifa akasema: Mimi nimehifadhi Khutba yake, Abu Thaa'laba akaketi, Hudhaifa akasema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

»إنكم في النبوة ما شاء الله أن تكون، ثم يرفعها إذا شاء، ثم يكون خلافة على منهاج النبوة تكون ما شاء الله أن تكون ثم يرفعها إذا شاء، ثم تكون جبرية تكون ما شاء الله أن تكون، ثم يرفعها، إذا شاء أن يرفعها، ثم تكون خلافة على منهاج النبوة«.

"Hakika nyinyi muko katika kipindi cha Utume kwa muda atakao Mwenyezi Mungu, Kisha atauondoa atakapo kuuondoa, Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume itakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu kisha ataiondoa atakapo kuiondoa, Kisha utakuwepo utawala wa Kiimla, utakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu, Kisha atauondoa atakapo kuuondoa, Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume").

C- Na katika Musnad ya Attwiyaalisiy 433- (Ametuhadithia Abu Daud asema: Ametuhadithia Al Waasitiy, Na alikuwa ni mtu wa kutegemewa (Thiqah), Amesema: Nimemsikia Habib bin Saalim, Amesema: Nimemsikia Al Nuu'man bin Bashir bin Saa'd, Asema: Tulikuwa tumekaa katika Msikiti pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na alikuwa Bashir ni mtu anayeacha kuongea, Akaja Abu Thaa'laba akasema: Ewe Bashir bin Saa'd, Je, umehifadhi Hadith yoyote ya Mtume (saw) kuhusu viongozi?, na Hudhaifa ameketi na Bashir, Hudhaifa Akasema: Mimi nimehifadhi Khutba yake, Abu Thaa'laba akaketi Hudhaifa akasema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«إِنَّكُمْ فِي النُّبُوَّةِ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ، فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً عَاضّاً، فَيَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ جَبْرِيَّةً، فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

"Hakika nyinyi muko katika kipindi cha Utume kwa muda atakao Mwenyezi Mungu, Kisha atauondoa atakapo kuuondoa, Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume itakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu kisha ataiondoa atakapo kuiondoa, Kisha utakuwepo ufalme wa kurithishana utakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu, Kisha atauondoa atakapo kuuondoa, Kisha utakuwepo utawala wa Kiimla, utakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu, Kisha atauondoa atakapo kuuondoa, Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume").

D- Na katika Ittihaaf Al khyra Al Mahra utunzi wa Shihabu Din Ahmad bin Abi Bakri bin Ismai'l Al Buusiriy (aliyekufa: 840H): [4264/1] asema Abu Daud Attwayaalisiy: Ametuhadithia Daud Al Waasitiy- Na alikuwa ni mtu wa kutegemewa (Thiqah)- Nimemsikia Habib bin Saalim, Nimemsikia Nuu'man bin Bashir bin Saa'd asema: Tulikuwa tumekaa katika Msikiti (pamoja na Mtume (saw) Na Bashir alikuwa ni mtu anayeacha kuongea, Akaja Abu Thaa'laba akasema: Ewe Bashir bin Saa'd,Je umehifadhi Hadith yoyote ya Mtume (saw) kuhusu viongozi?: Na Hudhaifa alikuwa yupo pamoja na Bashir, Akasema Hudhaifa: Mimi nimehifadhi Khutba yake, Akaketi Abu Thaa'laba, Hudhaifa Akasema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

»تكون فيكم النبوة ما شاء اللّه أن تكون، ثم يرفعها إذا شاء أن يرفعها، تم تكون خلافة على منهاج النبوة، ثم تكون ما شاء اللّه أن تكون، ثم يرفعها إذا شاء أن يرفعها، ثم تكون ملكاً عاضّاً فتكون ما شاء اللّه أن تكون، ثم يرفعها إذا شاء أن يرفعها، ثم تكون ملكاً جبرية فتكون ما شاء اللّه أن تكون، ثم يرفعها إذا شاء أن يرفعها، ثم تكون خلافة على منهاج نبوة «ثم سكت.

"Utakuwepo kwenu utume kwa muda atakao Mwenyezi Mungu, Kisha atauondoa atakapo kuuondoa, Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume, Kisha itakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu kisha ataiondoa atakapo kuiondoa, Kisha utakuwepo ufalme wa kurithishana, Utakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu kisha atauondoa atakapo kuuondoa, Kisha utakuwepo utawala wa Kiimla, Utakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu, Kisha atauondoa atakapo kuuondoa, Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume" Kisha akanyamaza.)

3- Ni wazi katika Hadith hizi kuwa Daud bin Ibrahim Al-waasitiy ni mtu wa kutegemewa (Thiqah). Ahmad amemtaja katika Musnad yake na Al Bayhaqiy katika Dalailu Nubuwwah na Attwayaalisiy katika Musnad yake na Buusiriy katika Ittihaaf Al khyra Al Mahra na hii yatosha kuswihi kwa Hadith... Na kadhalika ibn Hibbaan amemtia uzito (Daud bin Ibrahim Al-waasitiy) akamtaja kuwa ni miongoni mwa wenye kutegemewa (Thiqaat) katika kitabu chake (Al Thiqaat) cha Imam Hafidh Abi Hatim Muhammad bin Hibbaan bin Ahmad Attamimiy Al bastiy aliyekufa mwaka 354 H - 965M.

4- Lakini Swalahudin Al Idlibiy katika tovuti yake kupitia link ulioituma anatafuta kuhusu Abu Daud na kusema je, ndiye Al Waasitiy au Al U'qayliy kisha anazungunzia kuhusu Daud bin Ibrahim Al Uqayliy na kutaja riwaya nyingi kuwa huyo ni hazichukuliwi riwaya zake (Matruuk) na kusema: (Daud bin Ibrahim Kadhi wa Qazawin ndiye Uqayliy) na kuongezea (Al Azadiy alisema kuwa ni hajulikani tena ni muongo)... na kuongezea (Huenda ikasemwa kuwa hakika Daud bin Ibrahim Al-Waasitiy ambaye amepewa uzito na mpokeza kutoka kwake, Abu Daud bin Ibrahim Attwayaalisiy mwenye Musnad je itakubaliwa kupewa kwake thiqa kwa anayepokea kutoka kwake!) Kana kwamba Al Idlibiy hakubali kupewa kwake thiqa! Bali wala hakubali ibn Hibbaan kumfanya yeye thiqah!

Na anaongezea: (Na ikiwa Daud bin Ibrahim Al-Waasitiy aliyekuja katika Sanad ndiye anayetuhumiwa kwa uongo basi Sanad hiyo imeharibika, Na ikiwa ni mwengine basi Sanad hiyo iko sawa, Na ikiwa kumetokea shaka basi kwa uchache wajibu ni kuwacha).!

Na kwa nini kutokee shaka? Kwani imetajwa kutoka kwake na Al Bayhaqiy katika Dalailu Nubuwwah, Na Attwayaalisiy katika Musnad yake, Na Al Buusiriy katika Ittihaaf Al khyra Al Mahra, Imetajwa katika Sanad yao kuwa yeye ni Thiqah na wakaipokea Hadith hiyo, Na kadhalika ameipokea Ahmad katika Musnad yake, Na ibn Hibbaan akamtaja katika Al Thiqaat.. Vipi itokee shaka?!

Na mwisho hakika Hadith ya Khilafah kwa njia ya Utume imetajwa na wanachuoni wa kubwa hadith na Sanad yake ni sahih...

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Rashtah

15 Muharram Al Haraam 1443H

23/08/2021 M

Link ya jibu hili katika ukurasa wa Amiri (Mwenyezi Mungu amhifadhi) wa Facebook

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu