Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa

Amiri wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah katika Ukurasa Wake wa Facebook

Jibu la Swali

Hakuna Ziada katika Qur’an Isiyo na Maana

Kwa: Dkt Musab Al-Faroukh

(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalam Alaikum Wa Rahmatullah

Ni kwa kiwango gani kauli hii ni sahihi?

Majadiliano yalifanyika baina ya wanazuoni wa sarufi/sintaksi na mmoja wa wanazuoni wa balagha-ambaye alikuwa ni Ibn Al-Atheer-kuhusu herufi (An) katika kauli ya Mwenyezi Mungu (Swt)

(فَأَصْبَحَ فِى ٱلْمَدِينَةِ خَآئِفاً يَتَرَقَّبُ فَإِذَا ٱلَّذِى ٱسْتَنصَرَهُۥ بِٱلْأَمْسِ يَسْتَصْرِخُهُۥ قَالَ لَهُۥ مُوسَىٰٓ إِنَّكَ لَغَوِىٌّ مُّبِينٌ * فَلَمَّا أَنْ أَرَادَ أَنْ يَبْطِشَ بِالَّذِي هُوَ عَدُوٌّ لَهُمَا قَالَ يَا مُوسَىٰ أَتُرِيدُ أَنْ تَقْتُلَنِي كَمَا قَتَلْتَ نَفْساً بِالْأَمْسِ)

“Akapambazukiwa mjini asubuhi naye ana hofu, akiangalia huku na huku. Mara yule yule aliye mtaka msaada jana akawa anampigia kelele amsaidie. Musa akamwambia: Hakika wewe ni mgomvi kweli kweli. Basi alipo taka kumshika kwa nguvu yule aliye adui wao wote wawili, akasema: Ewe Musa! Unataka kuniuwa kama ulivyo muuwa mtu jana? Wewe hutaki ila kuwa jabari katika nchi, wala hutaki kuwa miongoni mwa wenye maslaha.” [Al-Qasas: 18-19].

Mwanachuoni wa sarufi/sintaksi alisema kuwa (An) ya kwanza katika ayah hiyo ni ziada, na kama itafutwa na kuwa: فلمّا أراد أن يبطش  maana itabaki kuwa sawa… hujaiona kauli yake Mwenyezi Mungu (swt):  (فَلَمَّا أَنْ جَاءَ الْبَشِيرُ أَلْقَاهُ عَلَى وَجْهِهِ)  “Basi alipo fika mbashiri na akaiweka kanzu usoni pake alirejea kuona.”  [Yusuf: 96]. Wanazuoni wa sarufi wamekubaliana kwamba (An) iliyotajwa baada ya ‘lamma’ na kabla ya kitenzi ni ziada. Kwa hivyo Ibn Al-Atheer alijibu vipi? Ibn Al-Atheer alimjibu mwanachuoni wa sarufi na kusema: wanazuoni wa sarufi hawana kauli katika masuala ya umbuji wa hali ya kujieleza kwa ufasaha. Na hawana maarifa ya siri zake, katika suala la kuwa wanazuoni wa sarufi. Hakuna shaka kuwa walipata kwamba (An) imetajwa baada ya ‘lamma’ na kabla ya kitenzi katika Qur’an Tukufu, na katika unenaji wa ufasaha, kwa hivyo wakafikiria kwamba maana ya kupatikana kwake ni sawa na maana bila yake. Kwa hivyo, wakasema: hii ni ziada. Lakini suala hili sivyo. Ikiwa ‘lamma’ imetajwa na (An) ikaifuata kisha kitenzi, hii ni ishara kwamba Musa (as) hakuharakisha kumuua mwanamume wa pili kama ilivyo kuwa katika kumuua mwanamume wa kwanza. Bali alichukua muda kuhujumu. Na ndiyo maana Qur’an ikaeleza haya katika ayah: (فَلَمَّا أَنْ أَرَادَ أَنْ يَبْطِشَ)  “Basi alipo taka kumshika kwa nguvu” kwa (An) ya ziada baada ya ‘lamma’. Ikiwa kitenzi kitakuja baada ya ‘lamma’ kwa kuondoa (An), basi itakuwa ni ishara kwamba kitendo kilikuwa ni cha mara moja. Ibn Al-Atheer akahitimisha mjadala wake kwa kusema: huu ndio utondoti usiochukuliwa kutoka kwa wanazuoni wa sarufi kwa sababu hauwahusu.

Kwa namna hiyo, je, kauli ya Ibn Al-Atheer ni sahihi? Na ikiwa sio sahihi, je, kuna maneno ya ziada katika Qur’an?

Jibu:

Wa Alaikum Assalam Wa Rahmatullahi Wa Barakatuhu.

Yaonekana kuwa kuna suala linalokosekana katika majadiliano kati ya Ibn Al-Atheer na mtu aliyekuwa anajadiliana naye. Naliona suala hili kama ifuatavyo:

Kuna masuala mawili katika ayah adili ambayo lazima yafahamike; nayo ni:

(فَلَمَّا أَنْ أَرَادَ أَنْ يَبْطِشَ بِالَّذِي هُوَ عَدُوٌّ لَهُمَا)  Basi alipo taka kumshika kwa nguvu yule aliye adui wao wote wawili”, (أن يبطش) na :(فلما أن)

1- La kwanza, nayo ni herufi ya nasbi “An” ambayo ilikuja katika hali ya wakati uliopo, ni kitenzi jina, herufi ya nasbi na ya kupokea:

Hufanya kile kinachokuja baada yake kuwa katika shina la neno (Masdar), kwa mfano, (يُرِيدُ اللهُ أَنْ يُخَفِّفَ عَنْكُمْ) inafasiriwa “Mwenyezi Mungu anataka kukupunguzieni taabu”, ni kwa sababu hufanya kitenzi katika hali ya wakati uliopo kuwa nasbi…na kuwa (An) ni herufi ya kupokea, hii ni kwa sababu hufanya kitenzi katika wakati wa sasa kuwa dhati kwa ajili ya kupokea, na “vile vile ukanusho wote katika wakati uliopo”, lakini wakati uliopo bila kutanguliwa na herufi ya nasbi hubakia kuwa hutegemea kielezi cha (Hal) na kupokea. Kwa msingi huu maana ya herufi ya nasbi hapo juu, maana ya  (فَلَمَّا أَنْ أَرَادَ أَنْ يَبْطِشَ بِالَّذِي هُوَ عَدُوٌّ لَهُمَا“Basi alipo taka kumshika kwa nguvu yule aliye adui wao wote wawili”, ni kwamba inawezekana kuwa Musa hakuchukua mpango wa kumshika kwa nguvu kwa haraka, bali alianza kufikiria kwa sababu maandiko ni (أَرَادَ أَنْ يَبْطِشَ) na wala sio  (أراد يبطش) (basi alipotaka kumshika kwa nguvu): vyenginevyo, haingechukua hicho kielezi na kupokea, yaani, uharaka ama fikra ya kufanya maamuzi, na kisha ingehitaji kiashiria (Qareena) kutilia nguvu kitendo, yaani, kielezi au upokezi, na kwa (أَرَادَ أَنْ يَبْطِشَ) “basi alipotaka kumshika kwa nguvu” ni ya kupokea bila ya kielezi (Al-Hal), kumaanisha, baada ya kipindi cha wakati wa kufikiria hata kama ni mchache.

2- Na matumizi ya (An) baada ya ‘lamma’, inamaanisha ziada katika lugha, kwa sababu kwa upande wa muundo wa lugha ni kama  "لما أن أراد" "لما أراد". Lakini ni ziada katika maana, ambayo ni thibitisho la kushika kwa nguvu pole pole, yaani, inathibitisha kinachofuata, "أن يبطش" yaani inathibitisha kukosekana kwa kuuwa kwa haraka, bali kwa kufikiria na kuchelewa hata kwa uchache.

3- Hivyo, “An” ya kwanza katika ayah tukufu, yaani, "أن يبطش" ni ziada katika muundo wa lugha, lakini kwa maana, na ni kusisitiza kule kuchelewa katika kushika kwa nguvu ambako kumetajwa baada yake "أن يبطش" haisemwi kuwa uthibitisho unamaanisha kwamba kithibitisho kinafaa kuwa baada ya kile kinachothibitishwa, katika wakati na muundo, kama vile    (فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِنْ مِثْلِهِ)   “Basi leteni sura moja ya mfano wake” thibitisho la wakati kama ilivyo onyeshwa hapo chini ("جاء جاء علي" أو"لا، لا أبوح بالسر") thibitisho la kimuundo. Ni kweli, isipokuwa msisitizo unatokana na msisitizo wa kisawe, basi inajuzu kwazo kuwa pamoja bila ya kwanza na baada ya kuwa ni sharti katika uthibitisho sawa. Kwa mfano, unaweza kusema: (أتى جاء علي) (Ata na Ja’a) kwa maana ya msisitizo sawa wa ule uliotangulia na ufuatao haukutajwa hapa. Kwa hivyo, (فلما أن أراد) inaashiria kuchelewa na kupungua, yaani, si mara moja, na vile vile ile iliyo baada yake, (أن يبطش) ni wakati uliopo na kitenzi cha nasbi, na inaashiria kwa siku zijazo, yaani, si mara moja. Hii ni katika suala la uthibitisho sawa. Kwa hiyo (An) katika (فلما أن أراد) inaweza kusemwa kuwa ni nyongeza ya lugha, lakini ina maana, ambayo ni msisitizo wa kisawe: (أن يبطش) ikimaanisha kuwa Musa (as) hakumshambulia mpinzani mara moja, lakini badala yake akapunguza kasi na kufikiria juu ya jambo hilo.

4- Ama iwapo kuna herufi za ziada katika Qur’an Tukufu; ikiwa kinachomaanishwa ni herufi za ziada zisizo na maana, basi sioni hilo. Hakuna herufi za ziada katika Qur’an zisizo na maana, na nimeitaja katika kitabu changu, Al-Taysir fi Usuul Al-Tafsir - Surat Al-Baqarah, ambapo imekuja katika tafsiri ya Aya tukufu  فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِنْ مِثْلِهِ)) “Basi leteni sura moja ya mfano wake” [Al-Baqara: 23]. Ilikuja ndani yake: “Hakuna kurudiarudia wala kuongezwa katika Qur’an bila ya maana. Kwa hivyo, kila kinachotajwa ndani ya Qur’an kana kwamba ni marudio au nyongeza kwa hakika ni kuongeza maana, kama vile ‘min’; hapa, imeonyesha ongezeko la maana, ambalo ni uthibitisho, yaani, uthibitisho wa changamoto iliyotangulia.)

Ama ikiwa kinachomaanishwa kwa herufi za ziada kwa maana, basi hii ipo, kauli ya Mwenyezi Mungu (swt) katika Surat Al-Baqara:

(فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِنْ مِثْلِهِ) “Basi leteni sura mfano wake” [Al-Baqara: 23]. Hapa "min" inaweza kusemwa kuwa ni nyongeza katika lugha, lakini si kwamba haina maana. Ni uthibitisho wa wakati, yaani kwa jambo lililotangulia, maana yake ni kwamba changamoto ilikuja kabla ya Aya hii kisha ikaja sasa kuthibitisha changamoto iliyotangulia, na kwa kutafakari Aya za Kitabu, inadhihirika kuwa changamoto hii iliteremshwa kabla ya hapo Makkah katika Surat Yunus (as):

(أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ قُلْ فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِثْلِهِ) “Je! Ndiyo wanasema (Kuhusu Mtume) ameizua? Sema: “Basi leteni sura leteni sura moja mfano wake.” [Yunus: 38] Surat Yunus iliteremka Makkah na Surat Al-Baqara iliteremka Madinah, yaani baada ya Yunus. Basi Aya ya Al-Baqara ni uthibitisho wa Aya ya Yunus kabla yake, kwa kuongeza “min” katika aya ya Surat Al-Baqara ya ziada kwenye aya ya Surat Yunus. Hivyo, imethibitisha yaliyokuwa kabla yake na haikosi maana.

Hivi ndivyo ninavyofahamu kwamba hakuna nyongeza katika Qur’an bila ya maana, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hekima.

Ndugu yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

 

4 Rabi’ Al-Awal 1444 H

30/9/2022 M

 

Link ya jibu hili kutoka kwa ukurasa wa Amiri wa Facebook.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu