Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa

Amiri wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah katika Ukurasa Wake wa Facebook

Jibu la Swali
Uzingatiaji Hadith kama Dalili katika Hukmu za Shari’ah
Kwa: Agus Trisa
(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakatuhu

Mwenyezi Mungu akulinde daima na akupe kheri nyingi..

Ningependa kuuliza swali:

Katika kitabu, Shakhsiya ya Kiislamu, imeelezwa kwamba Hadith Al-Ahad haizingatiwi kuwa ni dalili. Hii ni rai iliyo tabanniwa na Hizb.

Kwa hakika, wanazuoni aghlabu huwa na rai tofauti kuhusu usahihi wa Hadith. Wakati fulani mwanachuoni mmoja huiorodhesha Hadith kuwa ni Sahih, na wanazuoni wengine huiorodhesha kuwa ni dhaifu.

Kutokana na hili, nini rai yetu kama wanachama kuhusiana na hili?

Shukran sana kwa kujibu na Mwenyezi Mungu awalipe kheri.

Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakatuhu.

Jibu:

Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakatuhu.

Tumelifafanua suala hili katika Shakhsia ya Kiislamu Juz. I, ukurasa wa 345 (toleo la Kiarabu na ukurasa wa 262 toleo la Kiingereza) kama ifuatavyo:

[Uzingatiaji Hadith kama dalili katika Hukmu za Shari’ah

Dalili kwa ‘Aqidah lazima uwe ya kukatikiwa na yenye usahihi usio na shaka. Ndio maana riwaya ya mtu mmoja mmoja (khabar al-ahad) haifai kuwa dalili kwa ‘Aqidah hata kama ni Hadith Sahih katika maana na upokezi wake. Ama hukmu ya Shari’ah, dalili yake inaweza kuwa  isiyo ya kukatikiwa (thanni).

Hivyo basi, kama vile Hadith mutawatir inaweza kuwa dalili ya hukmu Shari’ah, vivyo hivyo riwaya ya mtu mmoja mmoja (khabar al-ahad) inaweza kuwa dalili ya hukmu ya Shari’ah. Lakini, khabar al-ahad ambayo inafaa kuwa dalili ya hukmu ya Shari’ah ni Hadith Sahih na Hadith hasan. Ama Hadith dhaifu, haiwezi kutumika kama dalili ya Shari’ah hata kidogo. Yeyote mwenye kuitumia hatahesabiwa kuwa ametumia dalili ya Shari’ah. Hata hivyo, kuzingatiwa kwa Hadith kama Sahih au hasan ni kwa mujibu wa yule anayeitumia ikiwa amefuzu kuifahamu Hadith hiyo, jambo ambalo linaweza isiwe hivyo kwa muhadithina wengine. Hiyo ni kwa sababu wapo wapokezi ambao ni waaminifu (thiqa) kwa baadhi ya muhadithina lakini sio hivyo kwa baadhi ya muhadithina wengine, au wanaochukuliwa kuwa wasiojulikana (majhul) kwa baadhi ya muhadithina na wanaojulikana vyema kwa wengine. Kuna Hadith ambazo sio sahih kutoka kwa ngazi moja ya wapokezaji lakini ngazi nyengine ni sahih kuna ngazi za upokezi ambazo ni sahih kwa baadhi lakini sio sahih kwa wengine. Na kuna Hadith ambazo hazitambuliwi na baadhi ya Muhaddithina na zinakanushwa nao lakini zinatambulika na Muhadithina wengine wanaozitoa kama dalili.

Mtu hapaswi kuwa na haraka katika kuitilia shaka au kuikataa Hadith isipokuwa ikiwa mpokezi wake anajulikana na wote kuwa ni si wa kuaminika au Hadithi hiyo inakataliwa na kila mtu au hakuna aliyeitumia kama dalili isipokuwa baadhi ya fuqaha waliokosa elimu ya Hadith hiyo. Hapo ndipo Hadith hiyo inatiliwa shaka na kukataliwa. Mtu anapaswa kuwa mwangalifu na atafakari kabla hajaitilia shaka Hadith au kuikataa.

Yeyote anayewachunguza wapokezi na Hadith atapata tofauti nyingi kuhusu wao baina ya muhadithina. Na mifano ni mingi.

Kwa mfano: Amepokea Abu Daawuud kutoka kwa ‘Amr ibn Shuayb ambaye amepokea kutoka kwa babake, ambaye amepokea kutoka kwa babu yake kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«الْمُسْلِمُونَ تَتَكَافَأُ دِمَاؤُهُمْ، ويَسْعَى بِذِمَّتِهِمْ أَدْنَاهُمْ، وَيُجِيرُ عَلَيْهِمْ أَقْصَاهُمْ، وَهُمْ يَدٌ عَلَى مَنْ سِوَاهُمْ، يَرُدُّ مُشِدُّهُمْ عَلَى مُضْعِفِهِمْ، وَمُتَسَرِّيهِمْ عَلَى قَاعِدِهِمْ»

“Waislamu wako sawa katika suala la damu. Wa chini wao kabisa wana haki ya kupewa dhima kwa niaba yao, na anayeishi mbali anaweza kutoa ulinzi kwa niaba yao. Wao ni kama mkono mmoja dhidi ya wale wote walio nje ya jumuiya yao. Wale walio na vipando vya upesi warudi kwa wale walio na vipando vya polepole, na wale waliotoka pamoja na kikosi (warudi) kwa wale waliobakia”. Mpokezi wa Hadith hii ni Amr bin Shuayb na ‘Amr bin Shu’ayb wamesimuliwa kutoka kwa babake na kutoka kwa babu yake ngazi ya upokezi ni maarufu licha ya kwamba wengi wametumia Hadith yake kama dalili na wengine wameikataa. Tirmidhi amesema: Muhammad bin Isma’il amesema: Nilimuona Ahmad na Ishaq (na akawataja wengine) walioitumia Hadith ya Amr bin Shuayb kama dalili. Akasema: ‘Amr ibn Shu’ayb alisikia Hadith kutoka kwa Abd Allah ibn Umar. Abu Isa alisema: Yeyote aliyezungumza kuhusu Hadith ya Amr ibn Shu'ayb alimtaja kuwa ni dhaifu kwa sababu alikuwa akinukuu Hadith kutoka kwenye vitabu vya babu zake kana kwamba walimchukulia kuwa hakuzisikia Hadith hizi moja kwa moja kutoka kwa babu yake. Ali bin Abi Abd Allah al-Madini amesema kwamba Yahya bin Said amesema: Hadith ya Amr ibn Shuayb kwetu haina mashiko. Pamoja na hayo, iwapo mtu atathibitisha hukmu ya Shari ́ah kwa Hadith ya ́Amr bin Shuayb, dalili yake itazingatiwa kuwa ni dalili ya Shari ́ah kwa sababu Amr bin Shuayb ni miongoni mwa wale watu ambao Hadith zao Muhaddithina wanazitaja kuwa dalili.

Kwa mfano, katika al-Darqutni, al-Hasan amepokea kutoka kwa 'Ubada na Anas ibn Malik kwamba Mtume (saw) amesema:

«مَا وُزِنَ مِثْلٌ بِمِثْلٍ إِذَا كَانَ نَوْعاً وَاحِداً، وَمَا كَيْلَ فَمِثْلُ ذَلِكَ، فَإِذَا اخْتَلَفَ النَّوْعَانِ فَلَا بَأْسَ بِهِ»

‘Chochote kinachopimwa kwa uzani (wuzina) kinabadilishwa sawa kwa sawa ikiwa ni cha aina moja, na kinachopimwa kwa idadi (kayla) kinabadilishwa vivyo hivyo ikiwa ni aina moja. Ikiwa aina zitatofautiana basi hakuna ubaya (ikiwa ubadilishanaji hautafanywa sawa kwa sawa)’ Katika isnadi ya hadith hii kuna al-Rabii bin Subayh, Abu Zur’a amemthibitisha kuwa ni mwaminifu lakini kundi jengine limemdhoofisha. Al-Bazzar ameinakili Hadith hii pia na inachukuliwa kuwa ni Hadith Sahih. Mtu anapoitumia Hadith hii au Hadith ambayo isnad yake ina Al-Rabii bin Subayh, ametumia dalili ya Shari ́ah kwa sababu Hadith hii ni sahih kwa mujibu wa kundi moja (la wanavyuoni wa elimu ya rijal), na kwa sababu al-Rabi’ ni mwaminifu (thiqa) kwa kundi jengine (la wakosoaji wa rijal).

Haipaswi kusemwa hapa kwamba mtu anapotangazwa kuwa ni mwaminifu na pia sio mwaminifu kwamba utiaji ila (jarh) inatangulizwa juu ya uthibitisho wa kutegemewa kwani hiyo inaweza kuwa pale tu wanaporipotia kuhusu mtu mmoja kwa mujibu wa mtazamo wa mtu mmoja. Ama wanaporipotiwa na watu wawili na mmoja akaichukulia kuwa ni kashfa (ta'n) na mwengine asiichukulie hivyo, basi inaruhusiwa. Ni kutoka hapa ambapo baadhi ya wanazuoni wamewatambua baadhi ya wapokezi (kama wa kutegemewa) na wengine hawakuwatambua.

Hivyo, tofauti nyingi zilizo katika Hadith, wapokezi na ngazi za upokezi baina ya muhadithina huwa wazi. Ikhtilafu nyingi kati ya muhaddthina, fuqaha jumla na mujtahidin fulani hutokea. Pindi hadith inapokataliwa kutokana na ikhtilafu hii basi Hadith nyingi zinazochukuliwa kuwa ni Sahih au Hasan zitakuwa zimekataliwa. Na dalili nyingi za Shari’ah zitaondolewa na hili halijuzu. Ndiyo maana Hadith haipaswi kukataliwa isipokuwa kwa sababu sahihi, ambayo inaweza kutambuliwa na wengi wa muhadithina au huenda isitosheleze masharti ya lazima kwa hadith Sahih na hasan. Inajuzu kutumia Hadith inapotambuliwa na baadhi ya Muhadithina na inatimiza masharti ya Hadith Sahih na Hasan. Inachukuliwa kuwa ni dalili ya Shari’ah na hukm iliyotolewa ni hukmu ya Shari’ah.] Mwisho wa kunukuu.

Natumai haya kwako yametosheleza, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Zaidi na Mwingi wa Hekima.

Ngugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

13 Rabbi’ Al-Awwal 1444 H

9/10/2022 M

Link ya jibu hili katika ukurasa wa Amiri wa Facebook

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu