Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali
Ni Kipi Kilicho Nyuma ya India Kufutilia Mbali Hadhi Maalumu ya Kashmir
(Imetafsiriwa)

Swali

[Raisi wa Marekani Donald Trump alimwambia waziri mkuu, Imran Khan, katika maongezi ya simu mnamo Ijumaa kuwa ni muhimu kwa India na Pakistan kupunguza taharuki eneo la Kashmir na Jammu kupitia "mazungumzo baina ya pande mbili," Ikulu ya White House ilisema katika taarifa. (Reuters mnamo 17/8/2019)] Mwisho. Trump anasema hili huku Modi akijigamba kuliunganisha rasmi eneo la Kashmir na kwamba halizozaniwi tena kati ya India na Pakistan. (Modi, waziri mkuu wa India alisema katika hotuba yake ya Siku ya Uhuru wa India mnamo 15/8/2019 kuwa serikali yake iliweza kutimiza lile ambalo serikali zote zilizo tangulia zilishindwa.') (Al-Sharq Al-Awsat mnamo 16/8/2019)! Swali ni: Kuna haja gani ya mazungumzo wakati ambapo India tayari imeshaiunganisha rasmi Kashmir? Ni kwa nini Pakistan haikuchukua hatua sahihi ya kuikomboa Kashmir kupitia Jihad, hususan kwa kuwa inayo uwezo wa kufanya hivyo kupitia jeshi lake? Vilevile je, Marekani ina dori yoyote katika hili? Mwenyezi Mungu akulipe kheri.

Jibu

Ili kufafanua jibu hili tunatathmini yafuatayo:

1- Kati ya maeneo yote ulimwenguni, Eurasia ndio eneo muhimu zaidi kwa wapangaji sera ya kigeni wa Marekani, na Marekani inajaribu kuhakikisha kuwa hakuna mshindani anayeibuka katika eneo hilo. Kiuhalisia kuna mahasimu wanne: Urusi, UUchina, Ujerumani na Khilafah, lakini Marekani inaona kuwa kwa sasa hasimu wa kihakika ni Uchina. Tangu kuanguka kwa Muungano wa Kisovieti, wanamikakati wa Marekani wamezitumia nchi za Asia zinazo pakana na bahari ya Pacific kuvuruga kuinuka kwa Uchina kama nguvu baharini,

Wamelitumia bara Hindi ili kupambana na kuinuka kwa Uchina kama nguvu kuu eneo la Eurasia … na huku Marekani ikiimarisha uwezo wake katika eneo la Asia-Pacific kupitia idadi kubwa ya miungano pamoja na Taiwan, Thailand, Vietnam, Ufilipino, Japan, Indonesia na Australia kuhakikisha kuwa hakuna muungano wowote mkuu utakao tokea katika bara Hindi – hususan India – hadi Vajpayee ilipo tawala serikali mwishoni mwa miaka ya tisini: utumizi mbaya wa India ulimalizika baada ya ziara ya Rais Clinton mnamo 2000, na punde tu baada ya matukio ya Septemba 11, 2001, utawala wa Bush ukaangazia juu ya India. Sehemu kubwa ya amali za Marekani zilielekezwa katika kuziba mwanya wa kijeshi baina ya India na Uchina, kwa mujibu wa mipango ya Marekani … miongoni mwa hatua hizi ni makubaliano ya kinuklia pamoja na India.    

2- Marekani iliona kuwa taharuki juu ya Kashmir baina ya India na Pakistan zinaathiri kudhoofika kwa makabiliano ya bara Hindi dhidi ya Uchina … Ili kumaliza taharuki hizi Marekani ilianza mchakato wa upatanishi baina ya India na Pakistan, na lengo la upatanishi lilikuwa ni kuzima vita baina ya majeshi ya India na Pakistan kwa sababu ya Kashmir, na kuelekeza juhudi katika ushirikiano pamoja na Marekani hatimaye kuzuia kuinuka kwa Uchina. Marekani iliamini kuunganishwa kwa Kashmir na India na shinikizo la Marekani juu ya serikali nchini Pakistan ili kuizuia kutokana na amali ya kijeshi na kuhamisha mada ya mazungumzo kutatua kadhia hiyo na kuzuia mzozo wa kijeshi baina yao, kama vile mamlaka ya Abbas nchini Palestina na biladi za Kiarabu pambizoni mwao kutochukua hatua ya kijeshi dhidi ya umbile la Kiyahudi linaloikalia na kudai chochote linalotaka kwa Palestina! Hivyo basi, Modi alianza kwa mpango wa kuunganisha Jammu na Kashmir na kubadilisha sura ya idadi ya wakaazi huko, na kisha kufuatiwa na uamuzi uliochukuliwa na Modi mnamo 5/8/2019 wa kufutilia mbali Kifungu cha 370 cha Katiba yao juu ya Kashmir. Kifungu hiki kililipa eneo hilo kiwango kikubwa cha uhuru wa kujiamulia.

Inairuhusu Kashmir kuwa na katiba yake yenyewe, bendera yake na uhuru wake katika mambo mengi isipokuwa katika mambo ya kigeni, ulinzi na mawasiliano. Azimio halisi lilitolewa chini ya mswada kwa jina "Mpangilio Mpya", unaoigawanya Kashmir iliyo kaliwa maeneo mawili: Jammu na Kashmir na Ladakh na unayaungaisha maeneo haya mawili na serikali ya majimbo ya New Delhi. Bunge kuu la India, Baraza la Majimbo siku iliyo fuatia 6/8/2019 lilipitisha mradi kielelezo kwa kura 125 zilizo unga mkono na kura 61 zilizo pinga. Kifungu cha 35A kinacho wakataza wakaazi wasiokuwa wa Kashmiri kutonunua rasilimali na ardhi eneo la Kashmir, kilifutwa na kuruhusu Wahindi wengine kutoka katika majimbo mengineyo kuja Kashmir na kununua majumba na ardhi ndani yake na kuomba nafasi za kazi za serikali ndani yake, na kusababisha mabadiliko katika idadi ya wakaazi na tamaduni katika eneo hilo lililo na Waislamu wengi …yaani, mithili ya vitendo vya umbile la Kiyahudi vya kuiunganisha Palestina! Kama vile anavyo fanya Netanyahu, kwa idhini ya Marekani na ruhusa yake, Modi ameiga hatua ya Netanyahu kwa Palestina kwa idhini na usaidizi wa Marekani.

3- Pindi India ilipo tangaza uamuzi wake wa hivi karibuni wa kufutilia mbali hadhi maalum ya Kashmir, msimamo wa Pakistan pia ulikuwa wa kuvunja moyo, haikuchukua hatua zaidi tu ya kushutumu, ili kujiondolea lawama. Waziri wa Kigeni wa Pakistan alitoa taarifa iliyo sema: Pakistan inashutumu vikali na kupinga matangazo yaliyo fanywa leo (Jumatatu 5/8/2019) na New Delhi. Hatua ya upande mmoja wa Serikali ya India haiwezi kubadilisha hali hii ya mzozo, kama ilivyo ndani ya maazimio ya Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa (UNSC), Pakistan itatekeleza kila iwezalo kupambana na hatua hizi haramu. (AFP 5/8/2019). Balozi wa Pakistan jijini Moscow, Qazi Khalilullah alisema: "Mamlaka za Pakistan kwa sasa zinaangazia juu ya matayarisho ya hatua za kidiplomasia, kisiasa na kisheria kwa hatua za India za hivi karibuni eneo la Kashmir, kamati maalum imeundwa ambayo itawasilisha kwa serikali mapendekezo kuhusiana na hili."

Kwa maana nyingine, kama vile ifanyavyo Mamlaka (ya Palestina) ya Abbas na biladi za Kiarabu pambizoni mwao, wanapinga na kulalamikia ukiukaji wa umbile la Kiyahudi dhidi ya Ardhi Tukufu ya Palestina pasi na kupeleka majeshi kupigana! Fauka ya hayo, wanazigeukia Umoja wa Mataifa na Marekani ili kuwatatulia kadhia zao, ingawa wao ndio maadui!

4- Hili linaungwa mkono kwa kutolewa kwa tweets za Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan katika mtandao wa Twitter mnamo 11/8/2019 zikiisifu hatua ya India kama ile inayo pelekea "ukandamizaji wa Waislamu nchini India na baadaye kuilenga Pakistan, na jaribio la kubadilisha sura ya wakaazi katika Kashmir kupitia mauaji ya kikabila" na anaomba ule unaoitwa uingiliaji kati wa Jamii ya Kimataifa na kwamba Jamii hii ya Kimataifa ina nguvu ya kuizuia India! Pakistan imesahau kuwa inayo nguvu ya kuizuia India … Hili linajulikana, India ilitangaza shambulizi la angani mnamo 26/2/2019 juu ya kambi za makundi ya Kashmir na "kuuwa idadi kubwa katika kambi hizi." Hili lilitokea baada ya kutangazwa kuwa makundi hayo ya Kashmir yalitekeleza oaeresheni dhidi ya jeshi la India linaloikalia Kashmir, na kuuwa wanajeshi 41 wa India mnamo 14/2/2019. Siku iliyo fuatia shambilizi hilo la India, Pakistan ikatangaza kuwa imetungua ndege mbili za India, kumkamata rubani na kuuwa wawili.

Hii yaonyesha uwezo wa kijeshi wa kuizuia na kuishinda India, lakini serikali ya Pakistan haina haja ya kuchukua hatua zozote kuizuia India, bali inatii maagizo ya Marekani, ilio agiza kuzima uhasama wa tukio hilo la kuangushwa ndege hizo mbili. Iliripotiwa katika habari kuwa: ("Waziri wa Kigeni wa Marekani Pompeo alizungumza kwa simu na wenzake wa India na Pakistan baada ya uvamizi wa India katika kambi ya Jaish-e-Mohammad, alitoa taarifa akizisihi pande hizo kutulia na kuepuka hatua yoyote ambayo itachochea na kuongeza hatari zaidi", hata alisimama na India, pindi alipo ongeza, "Mashambulizi ya angani ya India yalikuwa ni amali za kupambana na ugaidi, na kuisihi Pakistan kuchukua hatua ya umakini dhidi ya makundi ya kigaidi yanayo tekeleza shughuli zao katika eneo lake.") (AFP, Reuters 28/2/2019). Taarifa hii yaonyesha kiwango cha mapendeleo ya Marekani kwa India na usaidizi wake kwa yale inayo yafanya, kama inavyo fanya katika Palestina, ambako daima inalipendelea umbile la Kiyahudi na kulisaidia katika amali zake zote dhidi ya Waislamu wanaoitetea biladi yao na kufanya kazi kuikomboa …

Licha ya hayo, Pakistan, kama vile Mamlaka ya Abbas, na serikali za Kiarabu daima zimekuwa zikiigeukia Marekani na kuwasubiri waingilie kati kutatua tatizo lao, wakijua wazi kuwa Marekani iko upande wa India. Balozi wa Pakistan jijini Washington Majid Khan mnamo 27/2/2019 alisema kuwa ("taarifa ya Waziri wa Kigeni wa Marekani" ilifasiriwa na kufahamika kama uungaji mkono wa msimamo wa India na hili limewashajiisha (Wahindi) zaidi) na akasema: "Labda hakuna nchi nyingine iliyo katika nafasi bora zaidi kuliko Marekani kucheza baadhi ya dori.") (AFP 28/2/2019). Yaani, ingawa anaungama kuwa taarifa hiyo ya Wizara ya Kigeni ya Marekani inaunga mkono msimamo wa India, lakini anaamini kuwa Marekani inastahiki kucheza dori! Hii ndio tabia ya Marekani ya kuwazubaisha kwa Baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa. Hivi ndivyo ilivyo fanya serikali ya Pakistan, ilitangaza kuwa haitaki taharuki na uhasama na India, na kwamba itawasilisha malalamishi rasmi kwa Umoja wa Mataifa dhidi ya New Dehli, na sio zaidi ya hili. Serikali hiyo hata ilitangaza kuwa itamkabidhi rubani muuwaji wa India na kweli ilimkabidhi kama ishara ya amani kama ilivyodai. Baadaye ilipo unganishwa Kashmir, Pakistan ilitoa wito wa (kikao cha dharura cha faragha cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya hali ya eneo la Kashmir baada ya uamuzi wa India wa kufutilia mbali mamlaka huru ya eneo hilo … Balozi wa Pakistan katika Umoja wa Mataifa Maliha Lodhi aliukaribisha uamuzi wa Baraza la Usalama wa kujadili kadhia ya Kashmir wakati wa kikao maalum, akisema kuwa kadhia ya Kashmir imeanza kuibuliwa kiulimwengu na kwamba iko tayari kuitatua pamoja na India kupitia mazungumzo) (Al-Arabi Al-Jadeed mnamo 16/8/2019)!   

5- Msimamo huu unaashiria kuwa serikali ya Pakistan haitachukua hatua za kijeshi kuizuia India na haitachukua hatua za zozote kali dhidi yake, ambapo hili linatilia nguvu uamuzi wa India wa kufutilia mbali hadhi maalum ya Kashmir na kumakinisha uvamizi huo. Katika ziara yake nchini Marekani mnamo 21/7/2019, Imran Khan aliandamana na Mkuu wa Majeshi ya Pakistan Javed Bajwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ujasusi na Huduma za Usalama wa Ndani Hamid, wakati wa mkutano wake na Trump, alimuomba acheze dori ya Marekani nchini Afghanistan kwa kusema kuwa anataraji kuwa Pakistan itasaidia kupatanisha suluhisho la kisiasa ili kumaliza vita vya miaka 18 nchini Afghanistan. Hapo hapo Imran Khan alitii maagizo ya Trump na kusema: ("Nitakutana na Taliban na nitajaribu kila niwezalo kuwafanya wazungumze na serikali ya Afghan" Kisha akajisifu kuisaliti serikali ya Pakistan na kutoa huduma kwa Marekani. Akisema: "Ujasusi wa Pakistan ulitoa habari zilizo wawezesha Wamarekani kujua alipo Osama bin Laden,") (Reuters 22/7/2019).

Aliwapa Wamarekani yote haya huku wao wakiunga mkono India kwa gharama za Pakistan! Pindi India ilipo tangaza kufutilia mbali hali ya Kashmir, Wizara ya Kigeni ya Marekani ilitoa taarifa ikisema: "Tunaendelea kuunga mkono mazungumzo ya moja kwa moja baina India na Pakistan juu ya Kashmir na kadhia nyinginezo zenye umuhimu." (Reuters 7/8/2019). Marekani haikushutumu hatua ya India na kusema kuwa inakiuka maazimio ya kimataifa juu ya Kashmir, bali iliyataja mazungumzo ikimkejeli Imran na serikali yake, ni mazungumzo gani hayo wanayo zungumzia wakati India imetangaza kuiunganisha rasmi Kashmir?! Hili linaashiria idhini ya Marekani kwa hatua hii, bali pia linaashiria Marekani kuijua hatua hii mapema, kwa sababu kamwe India haiwezi kuchukua hatua kama hii kabla ya kuishauri Marekani na kuchukua idhini kutoka kwao … 

6- Katika kitabu chetu, "Kadhia za Kisiasa – Biladi za Kiislamu Zilizo Kaliwa" kilicho chapishwa mnamo 2/5/2004, juu ya kadhia ya Kashmir, yafuatayo yameelezwa: (Hivyo basi Marekani, pamoja na India na Pakistan chini ya ushawishi wake, zinatafuta maelewano baina yao juu ya Kashmir. Imebadilisha mtazamo wake msingi wa suluhisho la kadhia hiyo; ambapo mwanzoni ilitaka kuifanya kadhia hiyo kuwa ya kimataifa lakini sasa inazisihi pande hizo kuitatua wao wawili, mtazamo wa Marekani wa hali hii sasa unahusisha ugawanyaji wa Kashmir, ili Kashmir itakayo kombolewa iwe ya Pakistan, na Kashmir itakayo dhibitiwa na India iwe ya India). Yanayojiri sasa yanakubaliana na yale yaliyo elezwa katika kitabu chetu, India ilichukua hatua hii na kuunda uhalisia mpya unao asisi uvamizi wa India wa Kashmir.

7- Uchina ilishutumu hatua ya India; uamuzi wa kufutilia mbali Kifungu cha 370 chini ya jina "Mswada wa Mpangilio Mpya" ulioigawanya Kashmir inayo kaliwa maeneo mawili: Jammu na Kashmir, na Ladakh, na kuunganisha usimamizi wa maeneo hayo mawili kwa serikali ya majimbo jijini New Dehli. Hususan kwa Ladakh, ambayo iko Kashmir, imo ndani ya muinuko wa Tibetan, ambao uko karibu na Uchina. India haikushauriana na Uchina kabla ya sheria hii kupitishwa. 

["Hivi karibuni India imeendelea kuhujumu ubwana wa kieneo wa Uchina kupitia kubadilisha sheria zake za nyumbani kipeke yake … Kitendo kama hicho hakikubaliki na hakiwezi kutekelezeka." Alisema Hua Chunying, msemaji wa Wizara ya Kigeni ya Uchina. Matamshi ya Ying yanajiri kujibu uamuzi wa New Dehli wa Jumatatu iliyopita wa kutangaza Ladakh kuwa eneo lililo unganishwa, ambalo linajumuisha sehemu ya magharibi ya mpaka wa Sino-India. Chunying alisisitiza kuwa Uchina daima imepinga ujumuishaji wa India wa eneo la Uchina sehemu ya magharibi ya mpaka huo chini ya jina la jimbo la kiidara la Uchina." (Taarifa mnamo 8/8/2019

8- Kutokana na hayo ya juu tunafupisha yafuatayo:

a- Kufutiliwa mbali kwa Kifungu cha 370 na mipangilio iliyo fanywa na ingali inaendelea kufanywa na Modi ya uunganishaji kwa idhini na usaidizi kutoka Marekani ikiamini kuwa uunganishaji huo utawafanya Waislamu kuisahau Kashmir na hivyo basi India na Pakistan hazitakuwa na matatizo baina yao ikizingatiwa kuwa serikali hizo mbili kwa sasa zinatembea pamoja katika msitari wa Marekani … Marekani imesahau au inataka kusahau pamoja na India kuwa Kashmir imo ndani ya moyo wa Waislamu nchini Pakistan na kwengineko kama ilivyo biladi yoyote nyingine ya Waislamu iliyo kaliwa …   

b- Uidhinishaji wa serikali ya Pakistan au kimya chake juu ya uunganishaji wa Kashmir kwa India haimaanishi kimya cha Waislamu nchini Pakistan au kimya cha majeshi yao … na mashambulizi ya jeshi hili yanajulikana na India na tukio la kuangushwa ndege mbili lingali bichi katika kumbukumbu ya India … Mashambulizi haya ya jeshi yanatekelezwa huku serikali ya Imran ikilizuia jeshi hilo kutokana na mashambulizi ya kuikomboa Kashmir. Linaruhusika kujihami pekee, pamoja na vizuizi pia! Hivyo basi itakuaje endapo yatachangamshwa kupigana? Hapo ndipo adui atakapo yaona tu maangamivu yake kutokana nao!

c- Uchina imepinga hatua ya India. Wizara ya Kigeni ya Uchina ilitoa taarifa ikisema: "Uamuzi wa India ni wa upande mmoja na unaathiri pakubwa ubwana wa kieneo wa Uchina na kukiuka makubaliano ya kimataifa. Beijing haitakubali uamuzi wa upande mmoja wa India kubadilisha hadhi halali ya Kashmir na uamuzi huo haukubaliki" (Anadolu 6/8/2019). Uchina inatambua kuwa hili linatilia nguvu msimamo wa India katika eneo hilo, na linaifanya India kushindana na Uchina na kuwa dola yenye nguvu katika eneo hilo sambamba nayo, na hili ndilo inalolenga kufanya Marekani ili kupambana na nguvu ya Uchina ya kieneo … Hususan kwa kuwa Ladakh iliyoko Kashmir imo ndani ya muinuko wa Tibetan karibu na Uchina, na ingawa ina idadi ndogo ya wakaazi ya takriban 270,000, lakini utatuzi wa kadhia ya Kashmir kwa njia hii na kuwekwa parwanja kwa eneo la Ladakh katika mpaka wa Sino-India pasi na mashauriano na Uchina imezua tuhuma kutoka Uchina. Endapo Uchina itaweza kudhibiti hatua zake na kuunda utambuzi wa kisiasa ili kupatiliza kwa manufaa yake msimamo wa Ladakh, huenda ukageuza karata juu ya mipango ya Marekani. Badala ya Ladakh kuwa kambi ya mbele kwa oparesheni za majeshi ya Marekani dhidi ya Uchina, kama inavyo panga Marekani, huenda ukawa uwanja unaoteleza kwa majeshi hayo ambao wataanguka ndani yake na hawataweza kutoka!    

9- Mwisho, janga letu ni watawala katika biladi za Waislamu. Chembechembe za nguvu yetu zinatosha na hata ni zaidi ya kutosha kurudisha fahari yetu na kumfunza adui somo ambalo watabaki nalo hadi makaburini mwao! Lakini watawala hawa ambao wamemsaliti Mweyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) na waumini wanawapigia magoti mabwana zao wakoloni makafiri zaidi ya wanavyomsujudia Mweyezi Mungu, Bwana wa Walimwengu, na wanayazuia majeshi kutokana na kupigana na maadui zao ili kukomboa uvamizi kutoka katika ardhi yao … Kisha watawala hawa wanaomba kwa udhalilifu baadhi ya makombo sakafuni mwa Umoja wa Taifa na Baraza la Usalama … Hii ni ikiwa watapewa hata hayo makombo! Lakini kwa mikasa yote hii, biladi za Waislamu zilizo kaliwa kuanzia Palestina hadi Kashmir hadi Burma, ardhi ya Rohingya, kisha Turkistan Mashariki, Caucasus, Chechnya na pambizoni mwake na Crimea, na kila ardhi ambayo Muadhini anasikika akipiga takbira yake na zilizo vamiwa na maadui wa Uislamu, zitarudi kwa idhini ya Mweyezi Mungu katika nyumba ya Uislamu na kunyanyua juu bendera ya Uislamu … zitarudishwa kupitia ngao (Junna) ya Imamu … na Khalifah mwongofu … zitarudishwa na jeshi la Kiislamu la Jihad …

Yeyote anayependa kupata fahari katika ulimwengu huu na daraja kubwa zaidi Peponi (al-Firdaus) kesho Akhera, basi nawakunje mikono ya mashati yao na wafanye kazi pamoja na wanaofanya kazi kusimamisha Khilafah, na kuruhusu kazi hii kuzunguka ndani ya damu yake, moyo wake na mikono na miguu yake kwa ikhlasi na uaminifu,

 (إِنَّ هَذَا لَهُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ * لِمِثْلِ هَذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ)

“Hakika huku bila shaka ndiko kufuzu kukubwa *Kwa mfano wa haya nawatende watendao” [As-Saffat: 60-61].

17 Dhul Hijjah 1440 H
Jumapili, 18/8/2019 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 02 Aprili 2020 21:05

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu