Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jawabu la Swali 

Mzozo wa Gesi ya Mashariki ya Mediterranean
(Imetafsiriwa)

Swali

Tovuti ya Misr Al-Arabi ilichapisha mnamo 28/8/2019 yafuatayo: "kazi ya utafutaji na uchimbuaji inaendelea kwa kazi kubwa na hakuna anayeweza kukwaza kazi yetu hivi sasa au siku za usoni… Haya ndiyo aliyoyasema Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan siku mbili zilizopita kuhusu kazi ya uchimbuaji wa gesi katika mashariki ya Mediterranean katika changamoto mpya kwa vikwazo kwa Misri, Cyprus na Umoja wa Ulaya (EU)." Je inamaanisha kuwa huu ni mzozo kuhusiana na gesi ya Mediterranean baina ya nchi nne? Je viwango vya gesi ndani ya Mashariki ya Mediterranean ni vikubwa kiasi cha kupelekea kuwa mzozo baina ya nchi kwa ajili yake? Mwenyezi Mungu akulipe kheri. 

Jawabu

Naam, viwango ni vikubwa na vyenye umuhimu kwa sababu ya eneo la Mashariki ya Kati ambamo viwango hivi vinapatikana na mzozo uliopo sio tu baina ya nchi nne (Uturuki, Cyprus, Umoja wa Ulaya na Misri) bali pia kuna Amerika, Urusi na umbile la uvamizi la Kiyahudi ndani ya ardhi tukufu ya Palestina… Nchi kubwa zenye ushawishi wa kimataifa zinapora gesi licha ya kuwa zimo katika mzozo wa kiuchumi na kisiasa… Ili kuweka wazi hili tunatathmini yafuatayo:

Kwanza: ugunduzi wa gesi na umuhimu wake katika Mashariki ya Mediterranean

1. Ugunduzi wa gesi katika Eneo la Mashariki ya Mediterranean:

Ugunduzi ulianza mnamo 2000 pale ambapo British Gas, tawi la kampuni ya British Petroleum lilipogundua eneo la Gaza Marine kilomita 36 kutoka katika ufukwe wa Ukanda wa Gaza. Jumla ya hifadhi ya eneo inakadiriwa kuwa takribani trilioni moja ya ujazo wa futi wa gesi… Mnamo Januari 2009, kukagunduliwa eneo la Tamara ambalo kwa mujibu wa takwimu za kijiolojia ina hifadhi ya takribani trilioni 10 za ujazo wa futi. Mwaka huo huo ukashuhudia ugunduzi wa eneo la Aphrodite kilomita 180 kutoka katika kusini-magharibi ya ufukwe wa Cyprus kwa kina cha mita 1700 ujazo wa mita. Eneo linapatikana kilomita 90 kutoka katika ufukwe wa kaskazini ya Palestina iliyovamiwa na kilomita 1650 chini ya maji. Jumla ya hifadhi ya Aphrodite inakadiriwa kuwa ni trilioni 9 ujazo wa futi wa gesi ya kawaida. Mnamo 2012 eneo la Leviathan lililo na hifadhi ya gesi trilioni 17 ujazo wa futi iligunduliwa umbali wa kilomita 135 kutoka katika ufukwe wa kaskazini ya Palestina iliyovamiwa karibu na mji wa Haifa ikiwa na kina cha mita 1600 chini ya bahari.

Mnamo 2015 eneo la Zohr liligunduliwa karibu na pwani ya Misri, liligunduliwa na kampuni ya Kiitali ya Eni ambalo ni eneo kubwa la gesi ndani ya Mediterranean. Eneo hilo ni takribani kilomita 200 kutoka katika pwani ya Bandari ya Said, Misri na imethibitishwa kuwa na hifadhi ya trilioni 30 ujazo wa futi wa gesi. Eni inakadiria kwamba itachimbua bilioni 2.5 ujazo wa futi kwa mwaka mnamo 2019 ambayo itakuwa ni takribani asilimia 40 ya uzalishaji wa gesi wa Misri. Baada ya eneo la Zohr, kampuni ya Kiitali ya Eni ilitangaza mwanzoni mwa mwaka huu ugunduzi wa gesi mpya karibu na pwani ya Misri, eneo la Noor ambalo linapatikana Mediterranean takribani kilomita 50 kaskazini mwa Sinai. Napia kwa mujibu wa Takwimu za Kijiolojia za Amerika mnamo 2010 kuna uwezekano wa kuwepo kwa trilioni 122 ujazo wa mita wa gesi ambayo haijagunguliwa ndani ya Mashariki ya beseni la Mediterranean mbali na pwani ya Syria, Lebanon, umbile la Kiyahudi, Misri na Cyprus kwa kuongezea kwa takribani bilioni 107 ya mapipa ya mafuta.

Kama unavyoona, utajiri ni mkubwa.

2. Umuhimu wa utajiri wa gesi ndani ya Mashariki ya Mediterranean

Umuhimu huu unakuja sio tu kutokana na umuhimu wa ugunduzi wa gesi bali pia kutokana na umuhimu wa mchoro wa kisiasa ndani ya eneo pana ambamo linapatikana; ikimaanisha Mashariki ya Kati ambayo ina takribani asilimia 47 ya hifadhi ya mafuta na asilimia 41 ya hifadhi ya gesi duniani. Umuhimu wake unazidi kutokana na kupatikana kwake ndani ya Bahari ya Mediterranean ambayo inafunguka katika mkutano wa Asia, Ulaya na Afrika na kuunganishwa kwake katika barabara za kibiashara za kimataifa kupitia Chaneli ya Suez, Bosporous na Gibraltar. Kuendelea kwa ugunduzi na makadirio haya yanazidisha matumaini ya nchi za Mashariki ya Mediterranean na kufungua uchu wa kampuni za mafuta na gesi na kuwasha moto wa ushindani wa kieneo kwa ajili ya rasilimali na kuzihusisha dola za kimataifa ili kujipatia utajiri wa ziada na kupelekea kukaribia kutokea kwa mzozo.

Pili: Nchi zilizo na mzozo juu ya Gesi ya Mashariki ya Mediterranean:

1- Nchi zilizo karibu na maji ya Mediterranean

a. Uturuki Cyprus – Ugiriki Cyprus: Uturuki Cyprus inazingatia kwamba utajiri wa kisiwa ni wa watu wake wote na hautakiwi kutumiwa pasina kumtenga mmoja kati ya pande husika. Lakini Ugiriki Cyprus ilipuuza suala hili na kukamilisha kulitenga Eneo Lake Pekee la Kibiashara (EEZ) na kujiwezesha kutumia utajiri wa gesi pekee mnamo 2010 ambayo ilipelekea upande wa Uturuki Cyprus kujibu kwa hatua kama hiyo kwa kuweka mipaka yake ya bahari. (Uturuki ilitiasaini makubaliano ili kutenga rafu ya bara pamoja na Cyprus Kaskazini mnamo 15/9/2011...) (Turkish Ahval news mnamo 8/11/2018). Kutokana na vitendo hivyo kumekuwepo na muingiliano baina ya maeneo yaliyofafanuliwa na “pande za Uturuki na Ugiriki Cyprus.” (Hivyo basi, Jamhuri ya Cyprus Kaskazini inadai kuwa ina haki juu ya maeneo mengi ambayo Ugiriki Cyprus iliyatenga mnamo 2010…) (Turk Press mnamo 11/7/2019). 

b. Muungano wa Ulaya: Kipaombele chake ni kuzidisha usalama wake wa kawi ili kupanua vyanzo vyake vya uagizaji pamoja na kupanua barabara za usambazaji hususan kutokana na kudhoofika kwa mahusiano baina ya Ulaya na Urusi na shinikizo za vikwazo vya Amerika vya miaka ya karibuni. Katika muktadha huu, gesi ya Mashariki ya Mediterranean imechangia katika mchakato huu na kupunguza kukaribia jumla kwa kutegemea gesi ya Urusi hususan kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Ulaya… Hivyo basi, EU inaonekana katika mchakato huu kupitia baadhi ya wanachama wake kama vile Ugiriki Cyprus na Ugiriki na kupitia kampuni za utafutaji mafuta na gesi.

c. Uturuki: Uturuki sio mwanachama wa Makubaliano ya Umoja wa Mataifa juu ya Sheria ya Bahari (UNCLOS) ambayo inairuhusu kutenga maeneo ya bahari, kwa uchache kwa sababu ya mzozo wake na Ugiriki ndani ya eneo la Aegean. Uturuki inazingatia kwamba eneo la pekee la kiuchumi lililofafanuliwa na Ugiriki Cyprus linamuingiliano na rafu ya bara la Uturuki licha ya kwamba haijatangazwa rasmi… Kwa msingi wa matakwa haya, Uturuki haiyatambui makubaliano yaliyowekwa na Cyprus (Ugiriki) ili kutenga eneo lake la pekee la kiuchumi pamoja na Misri na umbile la Kiyahudi na Lebanon na inazingatia kwamba mapendekezo ya kampuni za kigeni kutafuta na kuchimbua gesi ndani ya eneo hili kuwa ni haramu, kwa sababu inakwenda kinyume na haki za Ankara… Erdogan alisema katika hotuba kwa wafuasi wake wa chama tawala cha Haki na Maendeleo ndani ya Uturuki ambacho anakiongoza katika tukio munasaba na miaka 18 ya kubuniwa kwake ndani ya mji wa Ankara (“Tunapatikana ndani ya Mashariki ya Mediterranean kupitia meli za Uturuki na jeshi la wanamaji linalinda meli hizo” Erdogan alisisitiza kwamba Uturuki inaendelea na amali zake za utafutaji ndani ya eneo “imeidhinishwa na Jamhuri ya Uturuki ya Kaskazini ya Cyprus”... (Sawt Al-Imarat 24/8/2019).

d. Dola ya Kiyahudi mvamizi wa Palestina: kuzidi kwa ugunduzi wa gesi kunaisadia umbile la Kiyahudi kuepuka kuitegemea Misri na inaziba pengo kubwa katika sekta yake ya kawi. Sio tu hilo pekee, gesi kwa mujibu wa hesabu za mvamizi imegeuka na kuwa ni udhibiti wa kisiasa na kiusalama na silaha ya kikweli ya kisiasa katika kupangilia mahusiano yake na nchi kadhaa za Kiarabu ndani ya eneo jirani hususan Misri, Lebanon, Mamlaka ya Palestina na Jordan. Napia (“Israel” imeingia katika makubaliano na Ugiriki, Cyprus na Italia ya kujenga bomba kwa gharama ya uro bilioni 6 au dolari bilioni 6.8 ili kusafirisha gesi kutoka “Israel” kwenda kwa nchi tatu…) (Ash-Shurooq News on 25/11/2018), yote kwa sababu Ulaya inataka kupanua vyanzo vyake vya kawi.

e. Misri: Gesi sio tu ndiyo inayobeba thamani ya kiuchumi kwa utawala wa Misri lakini la muhimu zaidi inazingatiwa kuwa ni zana ya kuunganisha utawala na kupata uhalali wa kieneo na kimataifa kwa kukosekana uhalali wa kindani unaoruhusu watu wa Misri kutumia kwa ubora utajiri wa nchi. Mwanzoni mwa mwaka huu, Misri, dola ya Kiyahudi, Cyprus, Ugiriki, Italia, Jordan na Palestina walitangaza Jukwaa la Gesi ya Mashariki ya Mediterranean. (Mnamo Januari, Misri, “Israel”, Cyprus, Ugiriki, Italia, Jordan na Palestina walitangaza ndani ya Cairo kuanzishwa kwa lile linaloitwa Jukwaa la Gesi ya Mashariki ya Mediterranean. Jukwaa hilo halikujumuisha nchi hizi: Uturuki, Lebanon, Syria na Uturuki ya Kaskazini mwa Cyprus katika uanachama wake lilipoanzishwa, licha ya kuwa ni nchi zinazolitazama beseni la Mediterranean…) (Gulf Online on 15/1/2019).

f. Na zipo nchi zinazopakana (eneo la maji) na Bahari ya Mediterranean, lakini hazina athari au ushawishi (Syria ndani ya hali yake ya sasa…Lebanon, licha ya kuwa imetiasaini makubaliano na kampuni za Ufaransa, Italia na Urusi lakini bado hazijaanza na kuna uwezekano wa kuchelewa kutokana na uingiliaji kati wa dola ya Kiyahudi… na kisha mamlaka (Palestina!)

2. Nchi ambazo hazipakani na Mediterranean

a. Amerika: inalitizama eneo kupitia kwa mchakato mpana kwa mujibu wa vipaombele vyake ndani ya Mashariki ya Kati, mara nyingi zinahusiana na kuhakikisha usambazaji wa kawi na ulinzi wa umbile la Kiyahudi. Amerika imo ndani ya eneo la Mashariki ya Mediterranean kupitia makampuni yake na kupitia vibaraka wake ndani ya eneo. Napia usafirishaji wa gesi yake ya majimaji kwenda Ulaya umezidi na hili linaweza kuathiri mtazamo wake juu ya gesi ya eneo siku zijazo.

b. Urusi: Licha ya gesi ndani Mashariki ya Mediterranean kuwa sio mbadala kwa gesi ya Urusi na haishindani nayo, ilhali Moscow inataka kuhakikisha udhibiti wa soko la Ulaya kwa kuwa kujiwasilisha katika miradi ya ziada na mbadala yoyote, ili isiweze kuathiriwa vibaya nayo, na hivi ndivyo haswa inavyofanya… Moscow imo katika mapambano ya gesi ndani ya Mashariki ya Mediterranean kupitia makampuni ya utafutaji gesi (hali ya Lebanon), na ufadhili wa kifedha (hali ya Ugiriki Cyprus na Ugiriki) na kupitia uwepo wa kijeshi na makubaliano ya kibiashara (hali ya Syria).

Tatu: utafutaji wa gesi katika mzozo baina ya nchi zilizo na ushawishi wa kiuchumi na kisiasa

1. Ama kuhusu Muungano wa Ulaya: Mnamo Disemba 20, 2018, Ugiriki, Cyprus na umbile la Kiyahudi walitangaza kwamba walikuwa tayari kusonga mbele na mradi wa bomba unaoungwa mkono na Amerika ili kusafirisha gesi ya kawaida kutoka mashariki ya Mediterranean kwenda Ulaya. Bomba la Mashariki ya Mediterranean litasafirisha gesi kutoka baharini baina ya Palestina iliyovamiwa na Cyprus kwenda masoko ya Ulaya kupitia Ugiriki. Takribani bilioni 10 ujazo wa mita wa gesi ya kawaida zinatarajiwa kusafirishwa kwenda EU kupitia Ugiriki na Italia. Lengo la EU ni kupanua uagizaji wake wa gesi ya kawaida kando na gesi ya Urusi. Mradi wa Mashariki ya Mediterranean unatarajiwa kukidhi takribani asilimia 10-15 mahitaji ya gesi ya kawaida kwa EU kwa hiyo EU itakuwa na uwezo wa kupanua vyanzo vya kawi na Urusi itapoteza ushawishi wake wa bei za gesi juu ya EU. Muungano wa Ulaya inatarajiwa kupunguza bei ya soko la gesi ambayo imepanda zaidi kwa miaka michache iliyopita…

2. Hii ni kuhusiana na upande wa Ulaya ama kuhusiana na upande wa Amerika, Amerika imeishinikiza Urusi kwa kuiwekea vikwazo juu yake na washirika wake hususan Ujerumani ili kusitisha bomba la Nord Stream-2, kwa kudai kuwa mradi huu utaisukuma gesi ya Urusi ndani zaidi katika Ulaya Magharibi na kuiwezesha Urusi kukithirisha ushawishi zaidi juu ya sera ya kigeni ya Ulaya ambayo inairuhusu kutumia kawi kama zana ya kushinikiza nchi yoyote. Hivyo basi, Amerika inafanyakazi kuzisukuma nchi za Ulaya ili kununua gesi ya kawaida ya majimaji (LNG) kutoka kwa Amerika badala ya Urusi kama njia ya kupanua na kuhifadhi usambazaji wa kawi na kubuni mazingira ya ushindani. Hili bila shaka linaathiri mradi wa Nord Stream 2: (inayojumuisha ujenzi wa mabomba mawili ya gesi katika Bahari ya Baltic kwenda Ujerumani itakuwa na kiwango cha bilioni 55 ujazo wa mita wa gesi kwa mwaka, ilhali idadi ya nchi zinazopinga mradi huu kama vile Ukraine, Amerika …) (Sputnik News on 1/4/2019).

3. Ushindani na mizozo baina ya Amerika na Urusi imezidi juu ya usambazaji wa gesi ya kawaida na kwa sababu EU ni mjumuiko wa nchi 28 ikiwa na jumla ya watu milioni 512, ni soko muhimu kwa wasafirishaji wakubwa wa kawi hususan inapokuja kwa gesi ya kawaida. Hii ndiyo sababu Urusi imekuwa na hamu nalo kwa muda mrefu na imekuwa chanzo kikuu na msambazaji mkubwa wa gesi ya kawaida kwa soko la Ulaya na hivi sasa Amerika nayo imeingia katika msitari na inatizama kuipa changamoto Urusi kwa kuzidisha usafirishaji wake wa gesi ya Amerika (LNG) kama nyepesi na salama katika uhifadhi na usafirishaji.

Kwa upande mwengine ni ghali kwa sababu ya juhudi inayohitajika kuifanya kuwa majimaji na kuisafirisha ukilinganisha na gesi iliyosafirishwa kupitia mabomba na vyanzo vingine vya kawi. Lakini lau itakuwa ghali kwa msingi wa ushindani, inaweza kucheza dori ya kuzidisha usambazaji wa gesi ya EU ambayo ni tishio kubwa kwa Urusi… Amerika imeanza kufanya hivyo. Kiwango cha gesi ya kawaida ya majimaji inayosambazwa kutoka Amerika kwenda Muungano wa Ulaya kilitimia takribani asilimia 24 cha jumla ya uzalishaji wa gesi (LNG) ya Amerika mnamo Oktoba 2018, ikilinganishwa na takribani asilimia 10 kutoka kwa usafirishaji wa Amerika uliokwenda kwa Muungano wa Ulaya mnamo 2017; mwaka ambao Amerika ilianza kuibuka kama msafirishaji wa gesi kwa mara ya kwanza. Katika miezi ya mwanzo ya 2019, uagizaji wa EU wa gesi ya Amerika ulikuwa kwa asilimia 13 na kuifanya kuwa msambazaji wa tatu mkubwa kwa EU. Hii ni kwa sababu ya uzalishaji kutokana na shale za mafuta ndani ya Amerika. 

4. Kwa kifupi, Urusi inadhibiti usambazaji wa gesi ndani ya Ulaya na kuutegemea pakubwa, hitajio la kupanua vyanzo vya kawi vinakuwa na EU iko makini kunusuru mradi wa Mashariki ya Mediterranean na kupanua uagizaji wake wa gesi ya kawaida kando na gesi ya Urusi iliyoruhusiwa na Amerika hususan baada ya uzalishaji wa Bahari ya Kaskazini kupungua. Wakati huo huo, Amerika inataka kudhibiti soko la Ulaya kwa kuzisukuma nchi za Ulaya kununua gesi ya kawaida ya majimaji kutoka Amerika badala ya Urusi, hivyo basi kuuzuia moja kwa moja mradi wa Nord Stream 2 ambao unaiunganisha Urusi na Ulaya kupitia Bahari ya Baltic.

5. Hivyo basi, Mashariki ya Kati ambayo kimsingi ni eneo la Kiislamu ambalo limebarikiwa na Mwenyezi Mungu (swt) kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta, gesi, madini n.k., lakini unaporwa na kutumiwa na wakoloni Makafiri pamoja na umbile la Kiyahudi mvamizi wa ardhi tukufu ya Palestina… Yote inatajirisha uchumi wao na kuviendesha viwanda vyao na masoko yao kujaa utajiri… baadhi yake inawafikia watawala, vibaraka wao na kuufanya kuwa ni mali zao binafsi licha ya utajiri huu kuwa ni mali ya umma ya watu, wamiliki wake na sio wezi wake!

Ni jukumu la Ummah kuchangamka na kubadilisha watawala hawa wakandamizaji ambao wamewawezesha wakoloni Makafiri kupora utajiri wetu… na Ummah umebakia katika maisha ya dhiki na haunufaiki na utajiri wake ulioenea: kama ngamia anayefariki kwa kiu katika jangwa lakini amebeba maji mgongoni mwake. 

Kumnyamazia mkandamizaji na kutofanyakazi kumbadilisha kwa ikhlas ya Mwenyezi Mungu (swt) na ikhlas ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw); hakuta muokoa aliyenyamaza kutokana na athari ya ukandamizaji, bali utamshambulia mkandamizaji na yule aliyenyamazia dhuluma.

 (وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْكُمْ خَاصَّةً وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ)

“Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Al-Anfal: 25].

Itamuathiri mkandamizaji kwa dhuluma yake na kuathiri wengine kwa kumnyamazia kimya mkandamizaji na kutofanyakazi ya kumbadilisha…

 (إِنَّ فِي هَذَا لَبَلَاغاً لِقَوْمٍ عَابِدِينَ)

“Hakika katika hii (Qur’an) yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada.” [Al-Anbiya: 106].

2 Muharram 1441 H
Jumapili, 1/9/2019 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 02 Aprili 2020 20:38

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu