Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Barua ya Wazi kwa Chama cha Mawakili
(Imetafsiriwa)

Mheshimiwa Rais wa Chama cha Mawakili, Mheshimiwa Ustadh Suhail Ashour

Waheshimiwa, Wanachama wa Baraza la Chama cha Mawakili

Waheshimiwa, Mawakili wanaoheshimika

Assalam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh,

Tuliwajia katika barua yetu ya tarehe 19/7/2022 na tukawashauri kwa dhati nyinyi na Waislamu ndani yake. Tumefuatilia matendo, kauli na misimamo yenu muliyotoa, na tumefuatilia matendo na uhalifu wa Mamlaka dhidi ya watu na kadhia ya Palestina. Mamlaka (PA) na wale walio nyuma yake wanafikiri kwamba watu wa Ardhi Iliyobarikiwa ni mawindo, au watumwa ambao wanaweza kuwadhibiti. Lakini hawatapata wanakichotaka. Hivyo basi, tukaona kwamba tunapaswa kukuhutubieni kwa mara nyingine tena, tukithibitisha wajibu wenu na kuthibitisha ulazima wa kusimama kidete na kithabiti kwa uhalifu unaofanywa na Mamlaka ya Palestina (PA) dhidi ya watu wetu na watu wenu, watu wa Palestina.

Mawakili waheshimiwa: Tangu kuanzishwa kwake, Mamlaka ya Palestina (PA) imekuwa ikifanya kazi kwa chuki, uovu na vitisho ili kuwatiisha watu wa Palestina na kuwafanya kuwa mawindo rahisi kwa maadui zao. Inafinika uhalifu wake kwa sheria wakati mwingine na wakati mwingine inapuuza sheria. Lengo lake ni kutekeleza mipango ya wakoloni, walioianzisha ili kupitisha mipango yao kwa watu wa Palestina; ili kuwaondoa katika kitambulisho chao na Dini. Ni sera ya muda mrefu inayolenga kulipa nguvu umbile la Kiyahudi, kulilinda na kuimarisha uwepo wake, sio tu Palestina, bali pia kupanuliwa matawi katika nchi za Kiislamu.

Watu wa Palestina wameteswa na mazungumzo ya kujisalimisha ya (PA) na majanga, maafa na kupuuzwa kwa ardhi na matukufu, na mradi wake wa "kitaifa" ambao ulibadilika kutoka kuwa mradi wa ukombozi kutoka kwa uvamizi na kuwa chombo cha usalama kwa ajili ya kulinda uvamizi, na kuwa mradi wa uwekezaji kwa viongozi wake ambao wanajali tu kudhibiti marupurupu na kuendeleza uwekezaji wao.

Mamlaka ya Palestina imekuwa chombo madhubuti cha maadui zetu katika kuua uthabiti wa watu wa Palestina. Utiaji saini wake muovu wa makubaliano ya CEDAW hauna lengo lolote zaidi ya kuvunja familia na kuipa tamkini Magharibi juu ya wanawake na watoto wetu. Fahamu ya jinsia imekuuzwa katika taasisi zote, mihadhara na semina hufanyika kwa ajili yake; ilianzishwa katika mitaala ya elimu ili kuwaambia watu wa Palestina na watoto wao kwamba kitambulisho cha kijinsia hakiekwi kwa kuzaliwa; bali, kinaathiriwa na mambo ya kisaikolojia na kijamii, na hubadilika na kupanua chini ya ushawishi wa mambo ya kijamii. Hisia ya mwanamume kwamba yeye ni mwanamke ni hisia ya kimaumbile ambayo lazima iheshimiwe, na mivuto ya mwanamke kwa mwanamke kama yeye ni mivuto ya kimaumbile ambayo lazima ilindwe. Wanadai kuwa ushoga na usagaji ni haki za mtu binafsi ambazo lazima zilindwe. PA imeunda taasisi na vilabu vya mashoga ambavyo vinalindwa na vyombo vyake vya usalama, na mawaziri katika PA wazihami, je huu ni uhalifu wa aina gani? Je, kudumisha na kutunza jamii kunahusisha kueneza ushoga na kuulinda?!

Kisha mamlaka ikathubutu kuwadharau watu kwa kutunga sheria na kuziidhinisha kiholela chini ya jina la “uamuzi wa sheria.” Ilivuruga akiba za watu na kula njama dhidi ya uwezo na ada za wafanyakazi ili kuzikamata kwa kutaka kutunga sheria ya hifadhi ya jamii, pamoja na kuhusiana na mishahara ya majumba ambayo ni mada ya migogoro ya haki za binadamu kati ya watu na ada ilizo lazimisha. Kisha sheria za “uuaji, taratibu za haki za kiraia na za kibiashara na taratibu za kuadhibu” na nyingine nyingi ni sheria za dhulma na kandamizi ambazo zitaathiri amani ya raia na kuwasukuma watu kuchukua haki zao mikononi mwao, na kusababisha fujo na mashambulizi dhidi ya mali na damu, na kugawanyika kwa jamii. Juu ya haya, imetungwa kwa uangalifu mkubwa ili kuwasukuma watu kwenye benki za riba ili wazongwe na madeni na kuzama kwenye kinamasi cha haramu na katika vita na Mwenyezi Mungu (swt) ambavyo hawataweza kuvizuia.

Mawakili Waheshimiwa: "Maamuzi ya sheria" yamekuwa yakilenga nyanja zote za maisha, ili kuimarisha ukusanyaji kodi, kunyonya damu ya watu, na kutekeleza sera za maadui zetu.

Kwa uamuzi wa dhulma, takriban dunum 73 za ardhi ya wakfu ya swahaba mtukufu Tamim Al-Dari, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, zilinyang'anywa ili ziwe chini ya umiliki wa Kanisa la Al-Maskobiya kwa maandalizi ya kuvujishwa kwake kwa umbile la Kiyahudi, kama ilivyotokea katika idadi ya mali za kanisa ambazo zilivujishwa kwa walowezi, na PA bado ingali inatafuta kupitia kwa mkuu wa Baraza la Mahakama "Abu Sharar" kukwepa uamuzi wa mahakama uliotolewa na Mahakama ya Upeo kubatilisha uamuzi wa unyakuzi huo. Hivyo, kwa nini msisitizo huu kwa upande wa PA kuhamisha umiliki wa ardhi ya wakfu ambao uliwakifishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)?

Na kwa amri ya sheria, sheria ya "Ulinzi wa Mtoto" ilitungwa, ambayo haikuwa ya kuwalinda watoto wetu kutokana na uhalifu wa uvamizi huo, wala kuwalinda na mashambulizi ya Magharibi ambayo yanalenga kuwatenganisha na Dini yao. Haikuundwa kwa ajili ya kulinda maadili tukufu ambayo watoto wetu wanapaswa kulelewa kwayo. Badala yake, sheria hii ilikuja katika utekelezaji wa maagizo ya nchi wafadhili za Ulaya kuwanyang'anya ulezi wenu kutoka watoto na familia zenu ili wawe mawindo rahisi kwa maadili ya Kimagharibi, na chombo mikononi mwa maadui zao. Sheria ya Ulinzi wa Mtoto humpa haki mtoto kuchagua Dini yake, mavazi yake, na kuamua mwelekeo wake wa kijinsia mbali na familia yake na maadili yanayoiongoza, na kufanya nidhamu ya baba kwa mwanawe, au nidhamu ya mwalimu kwa mwanafunzi wake kuwa hatia ya unyanyasaji, na kumlazimisha msichana kuvaa mavazi ya Kiislamu ni uhalifu wa ubaguzi na unyanyasaji. Kwa hivyo, ni nani anayefaidika na sheria hii, watoto wetu au maaadui zetu?

Haya yote yanathibitisha kwamba msingi wa PA ni uangamizi wa jamii na wizi wa pesa za watu, sio ulinzi wa haki zao. Lau msingi ungekuwa utunzaji na ulinzi wa haki za watu, ingefanya kazi ya kupambana na ufisadi na ufujaji wa fedha uliokithiri katika taasisi zake, ambao una ushahidi mwingi; baadhi yao wana mafaili ya wazi, hasa mafaili ya wale wanaovujisha ardhi kwa umbile la Kiyahudi, na dori ya huduma za usalama katika hilo.

Waheshimiwa Wanasheria: Ushahidi huu, na mwengine mwingi, unathibitisha kwamba “maamuzi ya sheria” yamekuwa chombo cha kuibomoa jamii, kuivunja kwake vipande vipande na kupoteza maadili yake. Katika suala hili, maamuzi ya mamlaka lazima yakomeshwe, na inapaswa kuwajibika kwa makosa yake, na kwamba kukataliwa kwa njia hii ya kiburi ni ya dhahiri. Kuilinda ardhi yetu, familia zetu na watoto wetu kunafanya kuwa ni lazima kwa watu wa Palestina kusimama kidete na kwa uthabiti katika kukataa maamuzi yote ya sheria, na kufanya kazi ya kuyafutilia mbali na kuyabatilisha, na kwamba jaribio lolote la kutafuta marekebisho halitamaanishi chochote ila uzembe na kusalimisha haki za watu na hasara yao, na usaliti wa watu, bali ni njama dhidi yao.

Kwa hiyo, tunawaomba mukabiliane na utawala wa PA, ama sivyo utakuleteeni hatari na utakuvisheni vazi la aibu na hasara.

Kadhia hii inahusiana na hatima ya watu wote, kwa sababu walengwa ni watu wote. Vyombo vya ulinzi na usalama vinataka kuwakamata watu na kuwaweka kizuizini bila ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili kuwanyanyasa na kuwatesa katika makao makuu yake ili kuvunja utashi wao na kuweka mazingira ya kigaidi kwa wananchi ambayo yanawawezesha viongozi wa mamlaka hiyo na wale walioko nyuma ya kuwasaga saga watu, bila mtu yeyote wa kuwazuia. Ni hatari kwa haki za watu kwa kadhia hii kubaki kuwa suala la umoja, na hairuhusiwi kwa vyovyote vile kuliweka suala la muungano, hivyo tunakualikeni muwe na nguvu zaidi katika kueleza uzito wa mambo ambayo PA inawafanyia watu na haki zao, na kuwaita wawe pamoja nanyi katika kukabiliana na uvurugaji wa mamlaka na kuwakoroga watu na haki zao. Bila watu kusonga mbele, hamutavuna matunda yanayotakikana kutoka kwa harakati yenu.

Waheshimiwa Mawakili: Kilichofanywa na mamlaka ni uhalifu kamili, na kupitia maamuzi yake, haituhumiwi tu kwa upuuzi au udikteta, bali inatuhumiwa kwa uhaini mkubwa kwa sababu ya kutabanni kwake sera za maadui zetu na ushirikiano wake nao katika kuwaangamiza watu wa Palestina na kuwafanya wapoteze ukakamavu wao. Sera jumla ya PA inalenga kuwaangamiza watu, kuua ari yao ya uasi inayokataa miradi ya kikoloni, kuondoa matamanio yao ya Kiislamu na kuwatenganisha na Dini na Ummah wao ili kurefusha uvamizi na kuuwezesha kuitafuna nchi na kupanua makaazi.

Hivyo basi, msimamo wa Chama cha Mawakili kukataa udhalimu wa mamlaka ulikuwa ni msimamo wa kimaumbile na ulitokana na upendeleo kwa watu na masuala yao na katika kutetea uadilifu na haki za watu. Watu wa Palestina wanathamini msimamo wa Chama cha Mawakili na wako pamoja nacho maadamu kinatabanni jambo lao kwa nguvu na ukakamavu bila ya kulegeza msimamo au uzembe.

Ni wajib mwende kwa watu wa Palestina, kwani wao ndio wamiliki wa jambo hili, na wana uwezo wa kukabiliana na ukiukaji wa Mamlaka. Tunatahadharisha dhidi ya kuzigeukia taasisi za kimataifa ambazo hazitashindwa kukufisidini, kwa sababu taasisi za kimataifa ndizo zinazoongoza maafa na shina la ugonjwa huo. Sio sahihi kuzitazama taasisi za kimataifa kama chombo chenye uadilifu na mlinzi wa haki za watu. Hili linathibitishwa vyema na misimamo ya taasisi hizi kuhusu uhalifu wa uvamizi huu. Taasisi hizi zimekuwa kifiniko cha uhalifu wake na chombo cha kutuliza na kuwatia ganzi watu na kuwapotosha kutokana na mwelekeo sahihi ili kutatua jambo lao. Suala la Palestina ni suala la Umma ambao msingi wake ni Uislamu, na ukombozi wake unaweza kupatikana tu kwa mwamko wa Umma na majeshi yake, na hilo ndilo linalowatia hofu na kiwewe maadui zetu. Ndio maana maadui zetu wana nia ya kuwapurukusha watu kutokana na suluhu sahihi ili masuala yao yabaki kutegemea Umoja wa Mataifa na maazimio ya kimataifa ambayo yanaendeleza na kulinda uwepo wa uvamizi huo, na unafanya kazi kulazimisha sera zake katika utekelezaji utashi wa nchi kuu na kulinda maslahi yao; ambayo la hatari zaidi ni mradi wa maendeleo endelevu wa 2030, ambao unawasilisha miradi ya kishetani kama ambayo ndiyo itakayofanikisha ustawi kwa watu wa ulimwengu, ambao kwa kweli ni uangamizi wao.

Watu wa Palestina, na sisi tuko pamoja nao, tutafanya kazi kwa nguvu zetu zote kulinda watoto wetu na familia zetu, na tutaendelea kupambana kunyanyua bendera ya Uislamu na kutafuta nusra kwa majeshi ya Kiislamu ili kuikomboa. Iwapo wale waliopagawishwa na Magharibi wanaona ushindi katika kutaka usaidizi kutoka kwa nchi za Magharibi, zenye uadui dhidi ya Uislamu, ndio njia ya kupata baadhi ya haki, basi kauli hii ya Mwenyezi Mungu (swt) inawafaa wao.

[مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِنْ دُونِ اللَّهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ ‌الْعَنْكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتاً وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ ‌الْعَنْكَبُوتِ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ]

“Mfano wa walio wafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyo jitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua.” [Al-Ankabut: 41]

Kwa kutamatisha: Tunakulinganieni nyinyi na watu wa Palestina pamoja na vipengee vyao vyote, vyama na makundi kusimama imara mbele ya utawala wa Mamlaka ya Palestina. Tunasisitiza umuhimu wa msimamo kuunganishwa, ambao ni kuizuia PA kufanya maamuzi ya sheria na kuyafutilia mbali yote na kutoyajadili au kutafuta marekebisho yake rasmi, kwa sababu madhara ya sheria hizi yatakuwa janga na balaa kwa watu wa Palestina na lengo lao.

Hakika ushindi wa Mwenyezi Mungu uko karibu.

[وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ ‌مُنْقَلَبٍ يَنْقَلِبُونَ]

“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.” [Ash-Shu’ara: 227]

H. 5 Muharram 1444
M. : Jumatano, 03 Agosti 2022

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu