Jumapili, 27 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  23 Safar 1444 Na: Afg. 1444 H / 04
M.  Jumatatu, 19 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tusipozisukuma Dola za Kikafiri Katika Mwelekeo Sahihi, Zitatusukuma Katika Mwelekeo wa Makosa!
(Imetafsiriwa)

Katika mkutano na waandishi wa habari mnamo Septemba 14, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price alisema: “Tumeeleza waziwazi kwamba hatuangalii kutambuliwa. Tunaangalia ni wapi - yalipo maslahi yetu, ushirikiano wa kivitendo pekee, ushirikiano wa kivitendo ambao tunatumai utaisukuma Taliban katika mwelekeo sahihi, na tutaendelea kushirikiana nao kwa msingi huo hadi tuone maboresho katika maeneo ambayo tunajali zaidi kuyahusu.”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan inazingatia mambo yafuatayo ya kuangaziwa katika suala hili:

1. Sababu kwa nini Marekani inazungumzia "mwelekeo sahihi" ni kwa sababu kila serikali na mfumo unaamini kwamba ni yenyewe tu ndio inayokwenda katika mwelekeo sahihi. Serikali ya Marekani, kwa kuegemea juu ya mawazo yake ya kisekula na maslahi ya kikoloni, pia inachukulia mwelekeo wake kuwa ndio sahihi huku ikiamini ule wa wengine kuwa wa makosa. Marekani inaposema kwamba itaisukuma Imarati ya Kiislamu katika "mwelekeo sahihi", kwa hakika inataka kuisukuma Imarati ya Kiislamu katika "mwelekeo wa makosa", kama vile mwelekeo wa 'usekula', 'mfumo wa kisekula wa kiulimwengu' na 'maadili ya kiliberali' huku pia ikiihimiza Imarati ya Kiislamu kujiunga na klabu ya Magharibi ili kusaidia kupata maslahi yao katika eneo hili.

2. Kwa upande mwingine, msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje amesema kuwa Amerika inaangalia "ushirikiano wa kivitendo" ili kushirikiana na Imarati ya Kiislamu kuwasukuma katika "mwelekeo sahihi". Hakika, neno "ushirikiano wa kivitendo" linamaanisha mkakati na sera zile zile ambazo zimekuwa zikiendeshwa na dola za Kimagharibi, hususan Marekani, dhidi ya Umma wa Kiislamu kwa miongo kadhaa. Vyenginevyo, sera ya "Karoti na Fimbo" inachukuliwa kama hatua za kivitendo ambazo Marekani inajaribu kuisukuma Imarati ya Kiislamu katika mwelekeo wa maadili ya Kimagharibi na maslahi yake ya kikoloni. Usaidizi wa kifedha na ushirikiano wa kisiasa unakusudia sera ya "Karoti" huku shinikizo la kisiasa, vikwazo vya kiuchumi, kuzifungia mali za Afghanistan, kufanya mashambulizi ya angani, milipuko ya kiajabu inayohusiana na ujasusi ikitafsiriwa kama sera ya "Fimbo". Sambamba na hilo, wito wa kuunda serikali jumuishi [ya uwakilishi], inayoheshimu haki za binadamu, haki za wanawake, kupambana na ugaidi, kutoruhusu Afghanistan kugeuka kuwa kimbilio salama kwa magaidi, nk, ni matakwa ya kivitendo ambayo kwayo Amerika inajaribu kuisukuma Imirati ya Kiislamu katika mwelekeo ambao yenyewe unauchukulia ndio "sahihi".

3. Kila serikali ya kimfumo ina masimulizi zake madhubuti [Aqeedah] ambayo kwayo inafafanua lipi jema na lipi ni baya - pia inapima ni nini kinachoinufaisha na kipi kinasababisha madhara. Amerika, ikijidai kuwa kiongozi wa mfumo wa kiliberali wa kiulimwengu, kwa upande mmoja, inaamini kwamba ulimwengu unaongozwa katika mwelekeo sahihi na "usekula" ndio mwelekeo sahihi pekee. Kwa upande mwingine, inapozungumzia mwelekeo sahihi katika sera yake ya kigeni, kwa hakika inakusudia maslahi [mielekeo] yake ya kikoloni ili kuwasukuma wengine kujisalimisha kwao. Ingawa ni lazima ithibitishwe tena kwamba mwelekeo sahihi ndio mwelekeo pekee ambao Mwenyezi Mungu (swt) ametuagiza kupitia risala zilizosambazwa na Mtume wa mwisho, Mtume (saw). Uislamu ndio mwelekeo pekee ulio sahihi (njia iliyo nyooka) ambayo itatabikishwa na serikali ya Kiislamu katika Dar-ul-Islam [jiografia ambayo Uislamu unatawala] na kubebwa kwa Dar-ul-Kufr kwa njia ya Dawah na Jihad.

Hivyo basi, ikiwa hatutatekeleza majukumu yetu kwa kutimiza misheni yetu; ikiwa hatutasimamisha Khilafah kwa njia ya Utume; na ikiwa hatutawaongoza wengine kwenda Jannah [Peponi] na mwelekeo sahihi kupitia sera yetu imara ya kigeni, wengine watatuongoza kwenda Jahannam [Motoni]. Hii ni kwa sababu pindi “haki” inaponuia kuachana na uwanja wa vita, “batili” hupelekea kujiita haki, na husubutu huwalingania wengine kujiunga na klabu yake.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu