Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  10 Dhu al-Hijjah 1441 Na: 031 / 1441 H
M.  Alhamisi, 30 Julai 2020

Pongezi Kutoka kwa Hizb ut Tahrir za Sikukuu ya Idd ul-Adha Iliyo Barikiwa

Allah Akbar, Allah Akbar, Allah Akbar, La Ilaha illa Allah… Allah Akbar, Allah Akbar, Wa Lillah AlHamdu

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu… Sifa Njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola wa Walimwengu, Mwenye kunakili waliyoyafanya na kuyatanguliza waja, na Mkwasi asiye hitajia dunia wala vilivyomo ndani yake, Mmiliki wa ufalme, Mwenye Utukufu na Heshima.

Na Rehema na Amani kamili zimshukie yule aliyeitakasa Al-Ka'aba kutokana na uchafu wa washirikina, na akairegesha Makkah kwa ajili ya Twawaf za Waumini, Bwana wetu Muhammad (saw) na jamaa zake na Maswahaba zake wote.

Amepokea Al-Bayhaqi katika Sunan al-Kubra kutoka kwa Jubair kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtume (saw) amesema:

«مَا الْعَمَلُ فِي أَيَّامٍ أَفْضَلُ مِنْهُ فِي عَشْرِ ذِي الْحِجَّةِ. قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، وَلا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ؟ قَالَ: وَلا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ إِلا رَجُلٌ خَرَجَ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ فِي سَبِيلِ اللهِ ثُمَّ لا يَرْجِعُ مِنْ ذَلِكَ بِشَيْءٍ».

"Hakuna amali inayofanywa kati siku zengine iliyo bora kuliko inayofanywa katika siku kumi za Dhu al-Hijjah. Maswahaba wa Mtume (saw) wakauliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hata kupigana Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu? Mtume (saw) akasema: Hata kupigana Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa mtu aliyetoka kwa nafsi yake na mali yake katika Njia ya Mwenyezi Mungu kisha kusirudi chochote katika vitu hivyo."

Basi, karibu Idd ul-Adha, furaha ya waumini kwa zile amali walizozitanguliza ndani ya siku kumi za Dhu al-Hijjah.

Basi, karibu Siku Kuu ya Hajj, furaha ya mahujaji kwa kumaliza Sa'yi (mwendo wa Swafaa na Marwa) yao ya faradhi hii kubwa.

Basi, karibu Siku ya Kuchinja, siku ambayo Waislamu hutanguliza vichinjo (udh'hiya) vyao kwa Mwenyezi Mungu kama kiigizo kwa babu yao Ibrahim, amani iwe juu yake.

Basi, karibu siku za takbira ambazo waumini hutamka "Allah Akbar".

Pia ni furaha kwangu mimi kufikisha pongezi zangu na za Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na wafanyikazi wote wanaofanya kazi ndani yake kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir Mwanachuoni Mkubwa, Ata bin Khalil Abu Rashtah na kwa Waislamu wote kwa sikukuu hii ya Idd ul-Adha iliyo barikiwa.

Idd inakuja mwaka huu huku hali ikizidi kuwa mbaya kote ulimwenguni, mfumo wa kirasilimali ambao ndio unaotawala umefeli katika jaribio lake la kuwa mfumo sahihi kwa wanadamu licha ya kuwa umeyajaza maisha katika muonekano wa kimadaniya na maendeleo ya vitu yaliyo oanishwa na Itikadi ya Kisekula inayokataa haki ya Mwenyezi Mungu ya kuweka sheria kwa waja wake. Na matokeo yake leo, ulimwengu umejaa uvumbuzi na ugunduzi huku watu wakiishi kwa kuchanganyikiwa na wasiwasi ndani yake. Watu ambao nyoyo zao zimekata tamaa na maisha baada ya maisha, na watu ambao wamezongwa na lindi la umasikini na kukimbilia nyuma ya mkate wao wa kila siku (pato), na watu ambao wanauwawa na vita bure bure visivyo kuwa na maana wala manufaa, na watu ambao wananyimwa rasilimali wanazotembea juu yake, na watu ambao wanatawala na kukhini kisha wanakirimiwa, na watu ambao wamepoteza vitambulisho vya jinsia zao mtu asijue je, yeye ni mwanamume au mwanamke au hata kuwa ni mwanadamu, na watu ambao wanakula mali za watu wakawafukarisha kisha hawashibi, na watu wanaojiua kwa maelfu baada ya kupoteza dira yao maishani.

Kisha Wamagharibi wanatutaka, kutokana na kufeli na kwa uongo, tuamini kwamba hii ndio thamani ambayo tunapaswa kuilipa kwa mkabala wa kupata teknolojia na utabibi!!

Enyi Waislamu: hakika wengi wenu hawana furaha kuishi ndani ya nchi zao wenyewe, na wale walio na usalama miongoni mwenu inawachoma hali mbaya ya habari za Waislamu, na yule anayelazimishwa miongoni mwenu kuhama kwa kukimbia mateso au ufisadi moyo wake haupumziki kutamani kwake kurudi kwao. Hali yenu ni kama hali ya Maswahaba watukufu, miongoni mwao ni wale waliotafuta hifadhi kwa jamaa zao lakini wakabakia wanaungulika kutokana na maudhi ya Maqureshi kwa ndugu zao, na miongoni mwao ni wale waliohamia Uhabeshi lakini hawakupumzika katika muda wote wa kuishi kwao huko. Na miongoni mwao ni wale walioshambuliwa na jamaa zao wakawaadhibu na kuwatesa. Na hali hii haikuwaondokea Maswahaba hadi nusra ya Mwenyezi Mungu ilipokuja kwa kusimama Dola ya Kiislamu mjini Yathrib, Al-Madina Al-Munawwar, ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliiangaza kwa Uislamu na Dola ya Kiislamu…

Na vilevile nyinyi (Waislamu wa zama hizi) maisha yenu yatabakia bila himaya, mataifa yatayapigania kama vile fisi wanavyopigania windo lao, hadi dola yenu inayo tokamana na itikadi yenu irudi iwahami na kuyahamu maslahi yenu na iwarudishie mambo yenu. Kutoka kwa Thawban mtumwa huru wa Mtume (saw) amesema, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«يُوشِكُ أَنْ تَدَاعَى عَلَيْكُمُ الأُمَمُ مِنْ كُلِّ أُفُقٍ كَمَا تَدَاعَى الأُكَلَةُ عَلَى قَصْعَتِهَا»

"Punde mataifa yataiatana kukushambulieni kutoka kila upande kama ambavyo walaji chakula wanavyoishambulia sahani yao" [Imepokewa na Ahmad]… na shambulizi hili halitaweza kukatwa ila kwa Dola ya Uislamu, Khilafah Rashidah kwa Njia ya Utume… Basi tunawalingania kuirudisha Khilafah, kwani kwayo ndio kuna utukufu wenu na radhi za Mola wenu, na afueni ya dhiki ya maisha ambayo humsibu kila mwenye kuupa nyongo utajo wa Mwenyezi Mungu:

﴿وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى * قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَى وَقَدْ كُنْتُ بَصِيرًا * قَالَ كَذَلِكَ أَتَتْكَ آيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا وَكَذَلِكَ الْيَوْمَ تُنْسَى﴾.

"Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu. Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona? (Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo vivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na kadhaalika leo unasahauliwa."  [Ta-Ha: 124 -126].

Enyi Ummah bora uliotolewa kwa watu:

Hizi hapa sauti zenu zilizo barikiwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu zilizojaza mbingu ya dunia zikisema: "…hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu amesadikisha ahadi yake na akamnusuru mja wake na akalipa nguvu jeshi lake na akayashinda makundi (Ahzab) Yeye peke yake…". Ndio hakika nusra inatoka kwa Mwenyezi Mungu, lakini Mwenyezi Mungu ameifungamanisha nusra hapa duniani na kufanya kazi, na akamharamishia nusra yule aliye sema:

    ﴾فَاذْهَبْ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَاتِلا إِنَّا هَاهُنَا قَاعِدُونَ﴿

"Basi nenda wewe na Mola wako Mlezi mkapigane. Sisi tutakaa hapa hapa." [Al-Maida: 24].

Kisha adhabu yao ikawa:

  فَإِنَّهَا مُحَرَّمَةٌ عَلَيْهِمْ أَرْبَعِينَ سَنَةً يَتِيهُونَ فِي الأَرْضِ فَلاَ تَأْسَ عَلَى الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ﴿

"Basi nchi hiyo wameharimishiwa muda wa miaka arubaini, watakuwa wakitanga-tanga katika ardhi. Basi wewe usiwasikitikie watu wapotovu." [Al-Maida: 26]. Hakika Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu na uwezo huwanusuru wakweli wenye ikhlasi wenye kufanya kazi ya kuinusuru Dini Yake:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُم﴿

Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu. [Muhammad: 7]

Basi jadidisheni azimio lenu katika Idd hii… tunawalingania kufanya kazi nasi katika kusimamisha Khilafah Rashidah ya pili kwa Njia ya Utume, huenda Mwenyezi Mungu akaturuzuku Nusra Yake hakika Yeye ndiye Mwenye kujibu dua.

Allah Akbar, Allah Akbar, Allah Akbar, La Ilaha illa Allah… Allah Akbar, Allah Akbar, Wa Lillah AlHamdu

Idd Mubarak, Wa Assalam Aleykum wa Rahmatullah wa Barakatuh.

Mh. Salah Eddine Adada

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari

Ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu