Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Wakati Msambazaji Mkuu wa Silaha Anapozungumza juu ya Usitishaji Vita na Amani, Hakika ni Dhihirisho la Udanganyifu na Unafiki

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Malaysiakini iliripoti mahojiano yake na Balozi wa Marekani nchini Malaysia, Edgard D. Kagan, ambapo alizungumzia, pamoja na mambo mengine, msimamo na sera za Marekani katika Asia Magharibi, haswa kuhusiana na Palestina. Alipoulizwa kuhusu mgongano unaoonekana wa wito wa kusitishwa kwa mapigano na upunguzaji kasi ya ghasia nchini Palestina huku wakati huo huo kukisafirishwa silaha kusaidia ‘Israel,’

Soma zaidi...

Utunzaji nchini Yemen ni Dhaifu kuliko Nyumba ya Buibui!

Mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa mnamo Jumamosi tarehe 31/8/2024 katika wilaya ya Bani Musa Al-Jarf huko Wusab As Safil Wilaya ya Dhamar, yalisababisha vifo vya watu 27, kujeruhiwa kwa watu 8, na kupoteza watu 2. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa mafuriko hayo pia yamesababisha kubomolewa kwa nyumba 15, uharibifu wa nyumba 8 katika wilaya ya Wadi Al-Akhshab, na kusombwa kwa magari 4, pikipiki 2 na duka moja.

Soma zaidi...

Malaysia Inaadhimisha Uhuru: Hata hivyo, Uhuru wa Kweli Uko Wapi na Wasaliti Halisi ni kina Nani?

Maadamu serikali itatawala kwa mujibu wa mifumo, nidhamu na sheria zilizorithiwa kutoka kwa wakoloni, uhuru wa kweli utabakia kuwa ndoto. Kwa hakika wale walioko madarakani wanaotawala kwa kufuata mifumo hii ya kikoloni, kimsingi, ni wasaliti wa kweli wa nchi na Ummah, kwani wameshindwa kuisimamia amana waliyopewa na Mwenyezi Mungu (swt), ambayo ni kutabikisha Shariah yote kwa jumla yake.

Soma zaidi...

Kwa kukosekana kwa Mradi wa Kiuchumi wa Mahouthi Kilimo cha Mkataba: Tishio Linalokaribia Kuwasagasaga Wakulima, Kuimarisha Udhibiti wa FAO, na Kushindwa Kufikia Kujitosheleza katika Nafaka nchini Yemen

Mnamo Jumatatu, Agosti 26, 2024, Waziri wa Kilimo, Uvuvi, na Rasilimali za Maji, Dkt. Ridwan Al-Rubai, alifanya mkutano wa mashauriano na wawakilishi wa vyama vya ushirika wa kilimo na wataalam maalum ili kujadili dori muhimu ambayo kilimo cha mkataba kinacheza kama njia madhubuti na ya hali ya juu ya unadi wa bidhaa za kilimo.

Soma zaidi...

Je, Barabara ya kuelekea Quds inapitia Mogadishu?!

Mnamo siku ya Jumamosi, Waziri Mkuu wa Misri Dkt. Mostafa Madbouly alithibitisha uungaji mkono usioyumba wa Misri kwa taifa ndugu la Somalia na kujitolea kwake katika kuimarisha umoja wa nchi hiyo. Alibainisha kuwa “kipindi kijacho kina ahadi kubwa kwa watu wa Somalia.” Madbouly alisema, “Kufikia umoja wa Somalia na kuunga mkono ndugu zetu wa Somalia katika awamu hii ni mojawapo ya vipaumbele vya juu vya dola ya Misri,”

Soma zaidi...

Je, Wananchi na Jeshi la Kifahari la Tunisia Wanakubali Mapokezi ya Waziri wa Ulinzi wa wale Wanaoua Ndugu zao mjini Gaza?!

Mnamo Jumatano, Agosti 28, 2024, Jenerali Michael Langley, Kamanda wa Kamandi ya Amerika ya Afrika (AFRICOM), alisema wakati wa mkutano wake na Waziri wa Ulinzi wa Tunisia Khaled El-Suhaili kwamba Tunisia iko mstari wa mbele katika nchi za Kiafrika zenye ushirikiano wa kihistoria na wa kipekee. Marekani, ikielezea utayari wake wa kuendeleza na kupanua mahusiano haya. Ziara hii inajiri siku tatu baada ya kuapishwa kwa wajumbe wa serikali.

Soma zaidi...

Komesheni Kupigania Vyeo na Marupurupu katika Jeshi la Pakistan. Badala yake, Maafisa wa Jeshi Waislamu Lazima Watoe Nusrah kwa ajili ya Kusimamisha Khilafah Rashida

Katikati ya utakaso wa sasa na kuwekwa kando maafisa ambao wanampinga mkuu wa sasa wa jeshi la Pakistan, ilijiri kutajwa kwa Hizb ut Tahrir. Gazeti maarufu la Kiurdu la “Daily Jang,” liliripoti mnamo tarehe 13 Agosti 2024, katika toleo lake kwa jiji la jeshi la Rawalpindi kwamba, “(2011) Brigedia Ali Khan alifikishwa mahakama ya kijeshi kwa kuwa na uhusiano na shirika lenye itikadi kali la Hizb ut Tahrir. Pia alituhumiwa kwa kueneza uasi ndani ya Jeshi la Pakistan.”

Soma zaidi...

Mamlaka ya Palestina Iliyofungamana na Maadui wa Mwenyezi Mungu Yakamilisha Dori ya Ghadhabu katika Kuwatesa Watu wa Palestina na Kuwakamata Watetezi wa Haki

Siku chache zilizopita, vikosi vya usalama vya Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA) viliwakamata Sheikh Aws Abu Arqoub na Sheikh Muhammad Manasrah, wanachama wa Hizb ut Tahrir. Kwa kuwakamata wale wanaosema ukweli, PA na vikosi vyake vinasisitiza kuwa kiongozi wa Mayahudi, wakidunga visu watu wote wa Palestina.

Soma zaidi...

Mgogoro wa Nishati nchini Jordan na Suala la Ufisadi wa Kiuchumi wa Mradi wa Al-Attarat, Utiifu wa Kisiasa, na Kuongezeka kwa Deni

Ripoti ya habari ya Shirika la Habari la Jordan, Petra, ya tarehe 6 Agosti 2024, ilisema kwamba “Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi iliamua kwamba serikali wala Kampuni ya Kitaifa ya Umeme hazihitajiki kulipa sehemu yoyote ya gharama kwa Kampuni ya Umeme ya Al-Attarat.” Habari hizi za upotoshaji zinakusudiwa kuficha hasara inayotarajiwa ambayo serikali ya Jordan itaipata kutokana na ukweli wa hukumu hiyo, inayosema: “Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi inaamuru kwamba mkataba huo ni halali na hauhusishi ukosefu mkubwa wa haki.”

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu